Viko wapi vichwa hivi?

Viko wapi vichwa hivi?

platozoom

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Posts
9,548
Reaction score
11,517
Hivi karibuni nilikutana na mmoja wa Wanajeshi aliyefungwa kifungo cha maisha kwa kosa la uhaini kabla ya msamaha wa Rais Mwinyi 1995.

Tulikutana kwa bahati tu, nilimuuliza mambo mengi yaliotukia wakati huo na hata sasa. Kama nilivyotgemea alinieleza kwa ufasaha malengo yao ambayo aliyaita ya kizalendo, na moja alilonieleza ni mabadiliko waliyotaka kuyafanya hasa kiuchumi. Kimsingi, hata baada ya kukamatwa sehemu ya mapendekezo yalifanyiwa kazi na Waziri mkuu wakati huo; Dr.Salim.

Kinachonifurahisha ni kuwa ana kumbukumbu nzuri na ni very intelligent. Akizungumza unaona ile hali ya uzalendo ndani yake, maneno machache ujumbe mzito.

Nachojiuliza kaliba ya Watu aina hiyo hata katika sekta nyingine imepotelea wapi. Tulikosea/tunakosea nini? Saaa hivi unaweza kumsikiliza afisa mkubwa serikalini akizungumza ukajiuliza kama yuko sawa kichwani!!!

Cc JokaKuu, nguruvi, The Boss, Pasco, Ritz, Jasusi, @elochima
 
Last edited by a moderator:

Mkuu watu wa aina hiyo wapo wengi sana ila ukikubali kufanya kazi kwenye hii serikali ya ccm lazima ukubari kupeleka akili zako likizo pia
 
Ni wachache sana wapo ndani ya serkali, lakini hawana sauti. wengi wapo nje ya serkali. Na kwa TZ huwa akili ndogo hutawala akili kubwa
 
System ya kihuni isiyoruhusu akili kubwa za watu kuonekana.wajinga ndio wanapewa nafasi.
 
Tatizo jengine lililopunguza calibre ya wafanyikazi serikalini ni uajiri wa kujuana, au ndugunization. Nasikia hali ni mbaya zaidi katika taasisi za usalama wa taifa.
Huko ulipopataja hakufai watu wameingizwa na kuchaguliwa bila kufata taratibu.
sana sana hao jamaa wakiwa bar kutwa kuwapiga watu mkwala,ndomana wanaishia kutoa siri za nchi tu.
 
Tatizo jengine lililopunguza calibre ya wafanyikazi serikalini ni uajiri wa kujuana, au ndugunization. Nasikia hali ni mbaya zaidi katika taasisi za usalama wa taifa.

Ulinzi na Usalama kuna matatizo makubwa,vijana na maafisa shupavu wanao openda nchi ni wachache sana. Wengi ni waoga waoga na vitisho vingi kwa wananchi umasikini.
 
Acha majungu wewe mleta mada, wala hujakutana na mwanajeshi yeyote mbona hujamtaja kwa jina na mwaka aliotaka kufanya hayo maasi kwani bado anaogopa nini?
 
Atakuwa Hans poppe maana nae ni wahaini waliotaka kuipindua serikali
 
Pointi Yake Ililenga kwingine kabisaa.. Alitaka kuwaaminisha watu na Kuwashswishi katika Kuyakubali mabadiliko.. Ukitaka kuuangalia huu uzi kwa Jicho la tatu hapa utapata kitu kiitwacho kampeni. Kwani Uhitaji watu wenye uhitaji na uthubutu wa kufanya mabadiliko?
 
Tatizo jengine lililopunguza calibre ya wafanyikazi serikalini ni uajiri wa kujuana, au ndugunization. Nasikia hali ni mbaya zaidi katika taasisi za usalama wa taifa.

CCM wameua nchi.
 
CCM wameua nchi..
 
kuna tatizo pia la elimu
siku hizi kila mtu ana dgree mbili au phd
wakati unawakuta wako watupu zaidi
kinachopatikana kinakuwa kama ni 'forged status ya msomi'
wakati uelewa wake ni mdogo sana
 
Ukijidai unajua zaidi, ukifanya kwa bidii, ukitenda kwa haki haupati ushirikiano. Binadamu wachache sana wanaweza kupambana na hali kama hii nao wanaamua kufanana na kundi lenye wengi.
 
kuna tatizo pia la elimu
siku hizi kila mtu ana dgree mbili au phd
wakati unawakuta wako watupu zaidi
kinachopatikana kinakuwa kama ni 'forged status ya msomi'
wakati uelewa wake ni mdogo sana
Halafu hao ndio unakuta wanapigania leadership positions. Tutaongozwa na vihiyo mpaka lini?:
 
Ni wachache sana wapo ndani ya serkali, lakini hawana sauti. wengi wapo nje ya serkali. Na kwa TZ huwa akili ndogo hutawala akili kubwa
Wako wengi serikqlini ila wanapoozwa kwa kupewa viyengo vinono,safari za nje na ile kitu inaitwa POSHO. Hapo mdomo na ubongo unaenda likizo
 
Back
Top Bottom