Vikao vya kuzimu

Vikao vya kuzimu

Ni kili wazi mr. Mshana wewe ni miongoni mwa watu wenye uelewa mkubwa mno, ukiacha elimu dunia upo uelewa asilia (power of mind) ambayo watu huwa hatuipati kwingine kokote isipokuwa tumezaliwa nayo (hutoka kwa Mungu/hekima).

Maandiko huwa yanasema HEKIMA ni chanzo maarifa/elimu/ujuzi/uelewa hapa hekima anazungumziwa MUNGU mwenyewe si semi kuna watu hawana Mungu la hasha ila UJAZO wa Mungu(ujazo wa Roho Mtakatifu) kwa watu ni tofauti, hatari ya hawa watu huwa ni maadui wakubwa wa shetani maisha yao huandamwa na shetani sana ila kuua ile hekima iliyo ndani mwao.

Ikitokea mtu huyu akawa kiongozi na kama alijinda na kumshinda shetani, huwa kiongozi bora people like late Mandela, Nyerere, Dalali Lama Mahandra Ghandi etc.

Mr. Mshana u kati ya watu hawa, tunza sana nafsi yako maana lazima unawindwa sana na shetani. Binafsi nakutambua sababu ni kundi hili la hawa watu.
 
Hawa -20 vs +80 ndio WATU WASIOJULIKANA Kumbeeee ok
Kuna kitu cha kutisha sana kinaendelea kimyakimya hapa nchini halafu kinasambaa kwa kasi, mauaji ya watu kwa style inayofanana.... Maiti nyingi hazina majeraha lakini zimefungwa kamba kwa mikononi na miguuni, nyingine zinatupwa majini na kufungwa mawe makubwa, pengine ili zizame
Unapotafakari hili kwa makini unaweza kuona kitisho cha dhahiri cha matokeo ya vikao vya kuzimu ambapo shetani baba wa udhalimu wote anachukua ushindi
Wakati mamlaka zikiendelea na taratibu zake kukomesha hii hali, wananchi nasi tuna jukumu letu kubwa, kuomba kusali na kukemea hili pepo la udhalimu, hii ni zaidi ya vita ya damu na nyama hii ni vita kubwa ya kiroho
 
12.png
 
4f8b30c74316a99b281eb2448c557db9.jpg
kuzimu kupo! Kuzimu kuna macho, kunaona! Kuzimu kuna masikio, kunasikia! Kuzimu kuna fahamu.

Kuna tawala na falme za giza! Hizi ni za kuzimu... Yanayotendeka kwenye ulimwengu wa macho asili yake ni kwenye ulimwengu wa roho,. Kwenye ulimwengu wa roho kuna falme mbili!!!

Ufalme wa nuru na ufalme wa giza
Ukifanikiwa kutenda jema jua lina asili na ufalme wa nuru! Ukitenda jambo baya lina asili na ufalme wa giza.

Kuzimu kuna vikao, hakuna jambo linalotokea kwa bahati mbaya HAKUNA... VIikao vya kuzimu viko connected moja kwa moja na ufahamu wako! Na maamuzi yoyote hutolewa na wewe mwenyewe ila kikao na hadidu za rejea hutoka huko.

Iko hivi, unapopanga jambo jema, hupangi pekeyako una washiriki kwenye hilo shauri na unapopanga jambo baya vilevile.

Utekelezaji wake ni matokeo ya mwisho ambayo maamuzi yake yametoka huko kwenye ulimwengu usioonekana! Ulimwengu wa roho.

Shetani yupo kuzimu kupo! Na shetani ndio kapewa milki ya dunia(inabidi kuwa mwamini kuweza kunielewa hapa).

Asilimia kubwa ya binadamu tunaishi kwenye uvutano wa hizi falme mbili, ufalme wa giza na ufalme wa nuru.... Tokea lolote la matendo yako ni ushindi wa ufalme mmojawapo kati ya hizo mbili.

Kila mwanadamu ana viwango husishi kwenye falme zote mbili na haziko stagnant, ndio maana wengi hufanya mabaya kisha wakajutia ama hufanya jema ila tu akajiona hakupaswa kufanya vile.

NGUVU hiyo ya uvutano iko kwenye mizania ya nafsi.. Mizania ya hasi na chanya.

Kuna watu mizania ya uvutano imeegemea zaidi upande wa hasi, yani unakuta ni -20 vs +80! Hawa ndio wale tunaowaita wana roho mbaya ama katili.. Hawaumii kabisa wanapowatendea wengine mabaya, yani maumivu ya wengine mateso ya wengine ni faraja kwao.

Hawa ndio wauaji, hawa ndio wale ambao kuzimu wamesimamia ukucha

Usalama na ustawi wa raia katika falme na tawala za kidunia hutegemea sana mamlaka zake zinavutwa na nguvu gani kwenye ulimwengu wa roho!
Sijaelewa kabisa! Sijui ugali wa muhogo umeniathiri uelewa ama vipi.....bado pia sijaelewa....
 
Mshana hii mada ipo vizuri sana. Mi huwa naamini sana kuwa hivi vitu vipo. Natoa mfano, kuna ndugu yangu mmoja huwa anafanya kila jambo halimaliziki. Na sio kwamba hana hela, la hasha. Hivyo, naamini mambo anayofanya vikao na hadidu rejea zinatoka huko. Sasa mtu afanyeje ili atoke huko.
Tiba ya chumvi kuogea ni kiboko ya yote
 
Shida yako mkuu unafahamu mengi ila unaleta mutasari tu kwa nini malizia basi
 
Hivi naomba niulize swali baada ya kufa tunaenda wapi hizi habari ukifanya mema kuna Mungu na mabaya unaenda motoni ni kweli au ni simulizi tu
Tukifa kuna sehemu mbili tofauti tunakwenda kutegemea matendo ya duniani 1 peponi 2 mangojeo peponi ni mahari pema na furaha na raha lakini mangojeo kuna baridi kali na kiu ya ajabu 1 wanasubili kukaa na mungu hao ni washindi 2 wanasubili muda utimu watiwe kwenye ziwa liwakalo moto pamoja na baba yao shetani
 
Jambo kabla halijatendeka au neno kusemwa hua lianzia katika ulimwengu wa roho,
Roho inashurutisha nafsi,mwili unapokea yale yaliamuliwa kutoka kwenye nafsi,
But huwa wanasema Mungu alimuumba binadam akampulizia pumzi hai,ikawa nafsi hai
Pumzi hai ni Roho,
Mkuu unaweza kufafanua hayo masuala ya nafsi, fikra na roho!
 
4f8b30c74316a99b281eb2448c557db9.jpg
kuzimu kupo! Kuzimu kuna macho, kunaona! Kuzimu kuna masikio, kunasikia! Kuzimu kuna fahamu.

Kuna tawala na falme za giza! Hizi ni za kuzimu... Yanayotendeka kwenye ulimwengu wa macho asili yake ni kwenye ulimwengu wa roho,. Kwenye ulimwengu wa roho kuna falme mbili!!!

Ufalme wa nuru na ufalme wa giza
Ukifanikiwa kutenda jema jua lina asili na ufalme wa nuru! Ukitenda jambo baya lina asili na ufalme wa giza.

Kuzimu kuna vikao, hakuna jambo linalotokea kwa bahati mbaya HAKUNA... VIikao vya kuzimu viko connected moja kwa moja na ufahamu wako! Na maamuzi yoyote hutolewa na wewe mwenyewe ila kikao na hadidu za rejea hutoka huko.

Iko hivi, unapopanga jambo jema, hupangi pekeyako una washiriki kwenye hilo shauri na unapopanga jambo baya vilevile.

Utekelezaji wake ni matokeo ya mwisho ambayo maamuzi yake yametoka huko kwenye ulimwengu usioonekana! Ulimwengu wa roho.

Shetani yupo kuzimu kupo! Na shetani ndio kapewa milki ya dunia(inabidi kuwa mwamini kuweza kunielewa hapa).

Asilimia kubwa ya binadamu tunaishi kwenye uvutano wa hizi falme mbili, ufalme wa giza na ufalme wa nuru.... Tokea lolote la matendo yako ni ushindi wa ufalme mmojawapo kati ya hizo mbili.

Kila mwanadamu ana viwango husishi kwenye falme zote mbili na haziko stagnant, ndio maana wengi hufanya mabaya kisha wakajutia ama hufanya jema ila tu akajiona hakupaswa kufanya vile.

NGUVU hiyo ya uvutano iko kwenye mizania ya nafsi.. Mizania ya hasi na chanya.

Kuna watu mizania ya uvutano imeegemea zaidi upande wa hasi, yani unakuta ni -20 vs +80! Hawa ndio wale tunaowaita wana roho mbaya ama katili.. Hawaumii kabisa wanapowatendea wengine mabaya, yani maumivu ya wengine mateso ya wengine ni faraja kwao.

Hawa ndio wauaji, hawa ndio wale ambao kuzimu wamesimamia ukucha

Usalama na ustawi wa raia katika falme na tawala za kidunia hutegemea sana mamlaka zake zinavutwa na nguvu gani kwenye ulimwengu wa roho!

Mungu na Iblis wanashindania nafsi ya mtu!
MUNGU ananguvu zaidi ya iblis,lakini hakulenga kumfanya binadamu aishi kidikteta! kampa uhuru wa kuchagua!(Free will) na hicho ndio kipimo cha imani!
 
Mshana wewe ni mtaalam wa mambo ya giza. ..na nuru hivi huwezi tuambia wasiojulikana walivaa nguo Gani na walikmbilia wapi baada ya unyama ule wa kumpga Mwanaharakat TL?
 
Back
Top Bottom