Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,096
- 828,928
Kuna tawala na falme za giza! Hizi ni za kuzimu... Yanayotendeka kwenye ulimwengu wa macho asili yake ni kwenye ulimwengu wa roho,. Kwenye ulimwengu wa roho kuna falme mbili!!!
Ufalme wa nuru na ufalme wa giza
Ukifanikiwa kutenda jema jua lina asili na ufalme wa nuru! Ukitenda jambo baya lina asili na ufalme wa giza.
Kuzimu kuna vikao, hakuna jambo linalotokea kwa bahati mbaya HAKUNA... VIikao vya kuzimu viko connected moja kwa moja na ufahamu wako! Na maamuzi yoyote hutolewa na wewe mwenyewe ila kikao na hadidu za rejea hutoka huko.
Iko hivi, unapopanga jambo jema, hupangi pekeyako una washiriki kwenye hilo shauri na unapopanga jambo baya vilevile.
Utekelezaji wake ni matokeo ya mwisho ambayo maamuzi yake yametoka huko kwenye ulimwengu usioonekana! Ulimwengu wa roho.
Shetani yupo kuzimu kupo! Na shetani ndio kapewa milki ya dunia(inabidi kuwa mwamini kuweza kunielewa hapa).
Asilimia kubwa ya binadamu tunaishi kwenye uvutano wa hizi falme mbili, ufalme wa giza na ufalme wa nuru.... Tokea lolote la matendo yako ni ushindi wa ufalme mmojawapo kati ya hizo mbili.
Kila mwanadamu ana viwango husishi kwenye falme zote mbili na haziko stagnant, ndio maana wengi hufanya mabaya kisha wakajutia ama hufanya jema ila tu akajiona hakupaswa kufanya vile.
NGUVU hiyo ya uvutano iko kwenye mizania ya nafsi.. Mizania ya hasi na chanya.
Kuna watu mizania ya uvutano imeegemea zaidi upande wa hasi, yani unakuta ni -20 vs +80! Hawa ndio wale tunaowaita wana roho mbaya ama katili.. Hawaumii kabisa wanapowatendea wengine mabaya, yani maumivu ya wengine mateso ya wengine ni faraja kwao.
Hawa ndio wauaji, hawa ndio wale ambao kuzimu wamesimamia ukucha
Usalama na ustawi wa raia katika falme na tawala za kidunia hutegemea sana mamlaka zake zinavutwa na nguvu gani kwenye ulimwengu wa roho!