Vikao vya kamati za Bunge kuanza Januari 13, 2026 Jijini Dodoma

Vikao vya kamati za Bunge kuanza Januari 13, 2026 Jijini Dodoma

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanza siku ya Jumanne Januari 13 hadi ljumaa ya Januari 23, 2026 katika Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma. Hivyo wanapaswa kuwasili Januari 12, 2026 siku ya Jumatatu.

1767692871456.png
Taarifa iliyotolewa leo Januari 6, 2026 na Ofisi ya Bunge imeeleza kuwa vikao hivyo ni kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano wa Pili wa Bunge unaotarajiwa kuanza
Januari 27, 2026.

Aidha, shughuli zilizopangwa kutekelezwa na Kamati hizo ni uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa kamati za kudumu za Bunge kwa mujibu wa kanuni za Bunge.

Pili, Kamati hizo kuzifahamu Wizara na taasisi zake na baadhi ya Sera na Sheria kulingana na majukumu ya kila Kamati.

Tatu, Kamati kupitishwa kwenye majukumu yake ya msingi na mwisho Kamati kufanya maandalizi ya hoja zitakazojadiliwa na Bunge.

SnapInsta.to_610645103_18108967936657593_4365086668472793714_n.webp
 
Wenzetu wanaenda kulipana hela za ada na sare za watoto wao😂😂
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom