Tatizo ni CCM!
Hali ya fedha katika serikali yetu ni mbaya sana kiasi kwamba motisha ya kufanya kazi kwa watumishi wake imeshuka sana kutokana na kukosa vitendea kazi nyeti na muhimu.
- Ukitembelea ofisi nyingi za serikali watumishi wengi wanapiga soga na kusubiri muda wa kuondoka.
- Mahakamani kesi nyingi ama hazijaanza kusikilizwa au zimeahirishwa kutokana na ukata(Rejea maelezo ya jaji mkuu kwa JK siku ya mahakama)
- Wanafunzi wengi wa vyuo vikuu wamekosa mikopo kwa kuwa serikali haijapeleka fedha.
- Wakandarasi wengi wamepunguza kasi ya kujenga miradi mbalimbali kwa sababu ya kutolipwa madai yao kwa wakati.
- Madaktari interns waligoma kwa kucheleweshewa posho zao za miezi miwili.
- Halmashauri nyingi za wilaya hazijapelekewa fedha za maendeleo kwa takribani miaka miwili.
Pamoja na ukata huu, Bunge limekuwa likifanya vikao vyake kama kawaida! Viongozi wakuu wamekuwa wakifanya ziara kama kawaida! Kwa maneno mengine fedha kidogo ambayo imekuwa ikikusanywa inaishia kwa Bunge na ziara za viongozi.
- Orodha ni ndefu sana!
Hii si sawa kabisa!
Kutokana na hoja hizo nadhani wakati umefika nalo bunge likapunguza vikao vyake ili kubana matumizi. Aidha kwa kupunguza vikao wabunge wataelewa kwa uhalisia hali ya kifedha ilivyo na hivyo kutoa miongozo inayoeleweka kwa serikali ili kuongeza mapato ya nchi.
- Bunge lina vikao vinne (4) kwa mwaka ambavyo huchukua miezi takribani minne(4) ( Kikao cha bajeti miezi 2 na ushee, Kikao cha Novemba wiki 2, Kikao cha Februari wiki 2 na Kikao cha Aprili wiki 2). Vikao vyote hivi hufanyika Dodoma.
- Vikao vya kamati za bunge ambavyo havina muda maalumu ambavyo hufanyika kabla na baada ya vikao vilivyoorodheshwa hapo juu. Vikao hivi hufanyika Dar es Salaam.
Wana JF naomba tujadili!
Natambua dhamira njema aliyonayo mleta thread, lakini hoja ya msingi si vikao. Hoja ni bunge kupunguzwa kwa kuondoa; (1) Viti Maalum, (2) Nafasi 5 za BLW. Aidha mtoa thread hajaelewa nini anakusudia kwa tafsiri ya Bunge.
Kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Bunge toleo la 2007, kikao cha bunge ni kila siku ambayo bunge litakutana hivyo mtoa thread alikusudia kusema "BUNGE LIPUNGUZE MIKUTANO YAKE" Ikumbukwe kuwa katika uhai wa miaka 5 Bunge letu lina mikutano 20 ikwa ni mikutano 4 tu kwa mwaka hivyo ili litekeleze kikamilifu majukumu ya kikatiba ya kuisimamia serikali, nidhahili mikutano hiyo si mingi kwani serikali dhaifu kama yetu isipofuatiliwa mara kwa mara ipo siku bunge litakuta nchi imeshauzwa.
Nawsilisha
Watumishi wanaosafiri mara kwa mara wanatumia udhaifu wa usimamizi katika serikali! Endapo serikali itawajibika ipasavyo na pia ikakubali kuwajibishwa, mambo haya yatakwisha!Ndiyo nchi yetu inavyokwenda hivyo hivyo.
Na wanaosafiri kila siku mbona haujawaandika.
Idadi ya wabunge pia ipunguzwe! viti maalum vifutwe ni mzigo!
Ni jambo la kusikitisha kuona serikali yetu inaendelea kuongeza/kubuni mikoa, wilaya, majimbo na kata bila kueleza ongezeko la mapato ya serikali katika kuendesha maeneo mapya. Kitendo cha kuongeza maeneo ya utawala maana yake ni kuongeza gharama za uendeshaji wa serikali.mungu atusaidie tupate kiongozi anayeelewa..hatuna sababu na wabunge wa viti maalum..japo mheshimiwa msekwa anajaribu kuelezea hadi ughaibuni essense yake lakini ni ****** mtupu..na hata idadi ya majimbo ni uchafu mtupu..
matatizo ya wananchi yanaeleweka yote hata tukiongeza majimbo ya uchaguzi na idadi ya wabunge hawataongeza chochote kwani tatizo letu ni mitaji ya kufanyia maendeleo..IKIWA NI PAMOJA NA UONGOZI BOOOORA.