Vikao vikuuubwa, maamuzi mabooovu!!!

GreenCity

JF-Expert Member
May 28, 2012
5,620
4,265
ni kuhusu kugawanya mkoa wa Mbeya.


1.JPG


11.JPG
Songwe ndilo jina lililopendekezwa kuitwa kwa Mkoa Mpya utakao gawanywa kutoka Mkoa wa Mbeya ambao utakuwa na Wilaya za Ileje, Chunya, Mbozi na Momba ambapo Makao makuu ya Mkoa huo utakuwa Mkwajuni Wilayani Chunya.


Mkoa wa zamani Mkoa wa Mbeya utabaki na Wilaya za Rungwe, Mbarali, Mbeya na Kyela ambapo Makao makuu yatabaki pale pale Jijini Mbeya.

Kupatikana kwa jina hilo na mwafaka huo umetokana na Mkutano wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa uliofanyika leo katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro.

Jina la Mkoa huo Mpya limetokana na uwepo wa Uwanja wa Ndege wa Songwe na Mto mkubwa unaoitwa Songwe ambao umezipitia Wilaya zote zinazounda Mkoa huo mpya.

Hata hivyo kuhalalishwa kwa jina na Mkoa huo unategemewa na Mamuzi ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete baada ya kupelekewa mapendekezo hayo ya RCC.
---------xxxxxxxxxxxxxxx-----------

MTAZAMO HALISI:
hapo kwenye red bold, kwa wanaoijua jiografia ya Mbeya mtakubaliana nami kuwa hayo ni maamuzi ya kipumbavu kabisa. haiingilii akilini mtu atoke ILEJE akafuate huduma za kimkoa CHUNYA, Yaani aruke mkoa wa MBEYA katikati ndipo aende makao makuu Chunya!

kama hoja ni kusogeza huduma, mbona kwa kikao hicho mnaongeza umbali wa hizo huduma? E.g Ileje na Mbeya mjini ni jirani zaidi kuliko Ileje na Chunya (mnakotaka iwe makao makuu), si hivyo tu, hata Mbozi na Mbeya mjini ni jirani zaidi kuliko huko Chunya.

najiuliza! hivi pamoja na kikao hicho kuwa na hao ma-PHD holders (Dr. Marry Mwanjelwa, Dr. Michael Kadeghe, Dr. Norman Sigalla etc) lakini wanatoa mawazo ya kipuuzi kiasi hiki kweli!

by the way:
wewe Mr PHILIP MULUGO na wenzio, siku ya tar 5 july 2013, mida ya saa nane mchana nimewaona pale Kalembu Bar (Soko Matola) na gari yako ya kazi mchana kweupeee mpo bar tena muda wa kazi! hivi ndio mlikuwa mnajipongeza na maamuzi ya kikao cha Tar 04 (jana yake), kweli!!! najua umefurahi huo mkoa kupewa jina la jimbo lako na makao makuu kuwa hukohuko kwenu lakini mnawafikiaje watu Mbozi Na Ileje kufuata huduma za kimkoa huko Chunya?



source: Mbeya Yetu blog na mimi mwenyewe
 
Hata kama wangekaa maprofesa 500, ili mradi kuna U-CCM hakuna suala la maana litakalo amuliwa.Vikao vilitakiwa vianzie kwenye tarafa,wilaya hadi mkoa ili wananchi watoe maoni yao kwanza!
 
Hata kama wangekaa maprofesa 500, ili mradi kuna U-CCM hakuna suala la maana litakalo amuliwa.Vikao vilitakiwa vianzie kwenye tarafa,wilaya hadi mkoa ili wananchi watoe maoni yao kwanza!

precise observation!
 
Back
Top Bottom