Vijimambo vya simu ya kiganja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijimambo vya simu ya kiganja

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Jul 29, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Jul 29, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  VIJIMAMBO KATIKA SIMU

  Miezi 3 iliyopita niliamua kununua simu 2 aina ya ZTE moja nilinunua Zain na Nyingine ni sehemu moja Kariakoo , Lakini zote zilikuwa na Chapa Ya zain ila hii moja Ambayo niliinunua kariakoo ilikuwa naweza kutumia zaidi ya Line moja na kweli nilikuwa naitumia kwa ajili ya kupichika Line Yangu ya Tigo .

  Moja nilinunua kwa shilingi alfu 29 katika moja ya ofisi zao wakati nyingine nilinunua kwa alfu 30 zote nilinunua siku moja sema tulipishana masaa kadhaa tu , mwanzo wakati natumia hii ya kariakoo nilikuwa nahisi kichwa kuuma kila ninapotaka kuongea ikiwa sikioni .

  Mwezi uliofuatia Nilipata nyingine kama hiyo hiyo ya kariakoo ambayo ilikuwa Flashed kama wenyewe wanavyosema , nilichofanya ni kuongea na rafiki yangu mmoja ili aweze kuilock kutumia programu Fulani ili baadaye niirudishe tena pale pale dukani kariakoo nione kama wataweza kuiflash tena , kweli mpaka sasa ni miezi nimeitembeza sehemu nyingi sana wafundi mbali mbali wameshindwa kuflash simu hii , programu zao wanazotumia zinakataa kwahiyo natumia Line hiyo hiyo moja tu .

  Kwahiyo ni miezi 3 imepita sasa , ndio naaza kuona tofauti za kweli kati ya simu iliyokuwa flashed na ambayo haijawa flashed , ile ambayo niliinunua kariakoo kwa sasa inasumbua sana network , mfano ninapotaka kuongeza salio inabidi nizime na kuwasha tena simu hiyo sio kama zamani ambapo ilikuwa inaweza kuingia tu , na sehemu nyingi nikipita inaweza kupoteza mawasiliano kabisa hata inpocharge hiyo battery haikai kwa muda mrefu sana , tofauti na hii ya Zain ambayo nilinunua kwenye duka lao hii haijawahi kunipatia shida yoyote mpaka sasa hivi inafanya kazi kama kawaida haina matatizo ya NETWORK wala matatizo ya Battey kuisha nguvu yake kwa kipindi kifupi .

  Mimi sio Mtaalamu wa mambo ya simu lakini nimegundua jambo hili , Ni vizuri watumiaji wenzangu wa simu nao wajaribu kuangalia na kuona tofauti iko wapi na ni vizuri pia mtu ukanunua simu kutoka kwa kampuni yako inayokupa huduma ya simu hiyo moja kwa moja itakuongezea matumaini na mambo mengine ya kiusalama haswa ya simu hiyo pamoja na ubora wake

  Halafu kwa siku za karibuni nimekuwa napokea matangazo toka Kampuni ya Tigo , hili la leo ndio limenivunja mbavu ( WEWE NI MSHABIKI WA SIMBA ? ANDIKA … PEKELA KWENYE NAMBA ….. , UJIUNGE NA MASHABIKI WENZAKO UTAKUWA UNAPOKEA HABARI MBALI MBALI ZA KLABU YA SIMBA, UTAKATWA TSHS 200 KWA HUDUMA HII ) kwanza sijaomba kujiunga na huduma hizo za kupatiwa matangazo mbali mbali na tigo , halafu wanapotuma Tangazo hili chini hawaweki Tangazo lingine la jinsi ya Kujiondoa katika huduma hiyo ya kupokea matangazo hayo

  Kila siku asubuhi napokea ujumbe wa kuniuliza kama nataka kuwa tajiri nifanye hivi na vile chini hawaweki maelezo ya jinsi ya kujiondoa na huduma hiyo ya kupokea matangazo hayo

  Sijui kama hapa Kwetu tunasheria zinazomlinda Mteja dhidi ya matangazo mbali mbali anayopokea kwenye simu yake ambayo analazimishwa kusoma bila idhini yake ili mradi awe mteja wa Huduma hiyo .
   
Loading...