figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Kukwama kwa mradi mkubwa wa maji wa zaidi ya shilingi Bilioni 6 ulioanza mwaka 2009 na kutakiwa kukamilika mwaka 2011 kumesababisha wananchi 32,811 wa vijiji saba wilayani Songea mkoani Ruvuma kukosa maji.
Kukwama kwa mradi huo mkubwa wa maji kunatokana na kampuni ya ukandarasi ya GNMS ya mkoani Iringa iliyokuwa ikitekeleza mradi huo wa maji mririko wa luyehela chini ya mradi wa usambazaji maji vijijini na usafi wa mazingira kufanya kazi kwa kusuasua na kusababisha Halmashauri ya wilaya ya Songea kuvunja mkataba wake.
Mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Pololeti Kamando Mgema amesema kuwa utunzaji wa mazingira ni muhimu kwa mradi huo wa maji kwa kuwa upatikanaji wa maji kwa mji wa peramiho na Halmashauri ya Songea unategemea mradi huo.
Kutokana na changamoto hiyo mkuu wa mkoa wa Ruvuma dkt Binilith Mahenge ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Songea kumtafuta mkandarasi wa kumaliza kazi iliyobakia ndani ya miezi miwili.
Chanzo: ITV