Vijana washauriwa kuchagua taaluma za vipaji

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1574843168400.png

Vijana nchini wameshauriwa kuchagua taaluma zinazoendana na vipaji vyao ili kujiweka kwenye nafasi ya kufanya kazi ambazo watazifurahia siku za baadaye. Mkuu wa Chuo cha Emerson Education, jijini Dar es Salaam, Faizan Hussein amesema jana sasa kuna changamoto katika uwiano wa vyeti vya wahitimu wa chuo na utendaji wao kazini.

Hussein alikuwa akizungumza katika mjadala wa ukuzaji ujuzi na ajira kwa vijana waliomaliza elimu ya sekondari ambapo alisisitiza juu ya umuhimu wa kuwepo na uwiano kati ya uwezo wa mhitimu kazini na uwezo wake darasani.

“Tumeona changamoto iliyopo wanafunzi wanaomaliza elimu ya sekondari kidato cha nne hawapati mwongozo juu ya uwezo wao binafsi na jinsi ya kuchagua masomo yatakayowasaidia kuchagua ajira wanazopenda. Hili jambo lina madhara wanafunzi wanapoanza kazi,”alisema.

Mjadala huo uliofanyika jijini Dar es Salaam uliandaliwa na Emerson Education kwa kushirikiana na kampuni za ubunifu ya Sahara Ventures na ulikuwa unawalenga wanafunzi waliomaliza mitihani ya taifa ya kidato cha nne na sita, wakisubiri kuendelea na masomo ya juu.

Mkuu wa Operesheni wa Sahara Ventures, Musa Kamata amewasihi vijana si tu kufanya uchaguzi sahihi wa taaluma na ajira za baadaye, bali pia kwenda na wakati sasa ambapo dunia ipo katika mabadiliko makubwa ya kiteknolojia.

Mmoja wa wanafunzi aliyehudhuria mjadala, Louis Matemba, ameupongeza uamuzi wa kufanya majadiliano hayo na wanafunzi na kuongeza sasa ameelewa kwa nini kuna watu wana ajira nzuri lakini hawana raha kazini.


Chanzo: Habari Leo
 
Ilitakiwa wao wawe mfano kipindi hawaja ajiriwa waliwahi kutafuta ujuzi gani hukawa unawasaidia uliwasaidia vipi mpaka kufikia hapo ulipo na sio blabla wakati hata ugumu wa changamoto wa kupambania vilivyo.
 
Back
Top Bottom