Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,180
- 7,354
Ndugu wanaJF nimerudi kutoka ban,
Nilikula ban kutokana na kushindwa kudhibiti hisia zangu, kwenye ile thread ya Ben Saanane, ikiwa ya kwanza kati ya hizi threads za masalia. Nilikasirika sana. Hata hivyo nikiwa pembeni kama guest, nimepata muda wa kutafakari kwa kina 'tatizo' la msingi la hawa vijana
Mwaka 2002 nikiwa mwanafunzi SUA, nilipata nafasi ya kuwasoma viongozi wa serikali ya wanafunzi (SUASO). Mara nyingi nilipokuwa sekondari, viongozi walikuwa wanachaguliwa miongoni mwa wanafunzi waliokuwa wanaonekana kuwa makini kimaadili, kimasomo na waliokuwa na uwezo wa kuongoza. Nilitarajia chuo kikuu hali itakuwa kama hiyo, tena ikifanywa kwa umakini zaidi.
Nilichojifunza baadae ni kuwa viongozi wa serikali ya wanafunzi pale SUA walikuwa watu wa hovyo kabisa, wenye uwezo mdogo kiuongozi, wala na watoa rushwa wakubwa na kwamba watu walikuwa wanatafuta uongozi pale kwa sababu ya kufuata hela pale ofisini. Nilifadhaika sana na sikutamani kabisa kuingia kwenye mchakato wa uongozi. Mwaka 2004 'nilijikuta nimechaguliwa kuwa 'waziri' katika SUASO baada ya best yangu mmoja kuwa raisi wa SUASO na kwa kuwa mimi ndiye nilikuwa namsaidia kuandika speech na ushauri mwingine, akanipa uwaziri kama fadhila. Hapo nilipata nafasi ya kukutana na viongozi wa vyuo vingine wakiwemo wa UD. Nilishangaa sana baada ya kugundua kuwa viongozi wa vyuo vingine nao walikuwa watu bogus, 'wapiga dili' za ela tu. Nakumbuka sekondari nilisoma na vijana waliokuwa na uwezo mkubwa sana wa uongozi ambao walikuwa UD by then, lakini aina ya viongozi wa UD niliokuwa nakutana nao kwenye vikao, nilishangaa sana...
Nilikuja kusikitika sana baadae nilipokuja kugundua kuwa vijana hawa bogus, waliokuwa wapiga dili na kupata uongozi vyuoni, ndio baadae walikuwa viongozi wa vyama vya siasa wakienda mtaani. Kwa mfano, nakumbuka kulikuwa na raisi wa SUASO aliyekuwa anaitwa Kenneth Nollo, ambaye baadae nilikuja kushangaa eti alikuja kuwa kiongozi wa UVCCM huko Dodoma!!! Nilishangaa maana nilikuwa namfahamu huyu jamaa kuwa na uwezo mdogo saaaana kiungozi na kiakili!!! Hakuwa hata na akili za kuwa monita wa darasa... Lakini ghafla akaingia UVCCM na akawa kiongozi.
Ndugu wanaJF, baada ya historia fupi hapo juu, nirudi kwenye topic kuwa kwa sasa vyama vya siasa vimejaa vijana wapiga dili. Hawana uchungu wa nchi, hawana uchungu na chama cha siasa, na wako radhi kununuliwa hata kwa sh 10,000 akafanya kitu ambacho hukutarajia. Nilisikitika sana kwamba wakati fulani tulimkabidhi kijana mmoja aliyekuwa anaitwa Darabe uongozi wa CDM pale SUA, lakini ndani ya miezi michache nikamwona Darabe amekuwa mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Manyara.
Vijana wapiga dili wamejaaliwa kipaji cha kuongea na kushawishi na wanatumia vipaji hivyo kujipenyeza kwa haraka sana kwenye uongozi wa vyama vya siasa.
Kwa bahati mbaya kutokana na michezo michafu inayochezwa na vijana na viongozi wengine wapiga dili, ni vijana wachache sana makini walio tayari kutafuta nafasi za uongozi kwenye vyama vya siasa. Wapo maelfu ya vijana makini, wenye uwezo mkubwa wa kuongoza, waaminifu na wenye uchungu na nchi hii, lakini hawapo kwenye vyama vya siasa.
Nini kifanyke?
Hili sio suala la chama kimoja. Wapiga dili wapo kwenye kila chama hususani vile vyenye fursa za 'dili' (ela). Kwa bahati mbaya, kwa chama kama CCM ambacho fursa za dili ni kubwa zaidi na zimekuwepo kwa muda mrefu zaidi, tatizo hili limeshaota mizizi mirefu sana, japo ipo nafasi fulani wanaweza kulidhibiti. "Wazee" wengi waliopo CCM ni wapiga dili ambao wamepata fursa hizi hasa baada ya chama kuwapoteza watu makini kama Nyerere. Tembelea nafasi za walaya, mikoa, na hata taifa utakuwa CCM inaongozwa na watu wenye historia ya kuwa wapiga dili, na ambao wanafanya kila linalowezekana kuhakikisha nafasi za vijana katika chama chao zinachukuliwa na watoto wao ambao wengi ni wapiga dili... Mifano iko mingi na wazi.
CDM nayo kwa bahati mbaya imeshakuwa 'infested' kwa kiasi kikubwa na wapiga dili. Simtaji mtu, lakini sote tunashuhudia vijana waliopewa nafasi mahsusi kabisa ndani ya chama, wakionyesha dalili zote za kununuliwa kwa bei nafuu na 'wazee wapiga dili', kwa maslahi ya kisiasa.
Solution...
Haina maana mtu kulima kwa kukwatua majani, na kuyaacha yamesimama nyuma yako, ukienda hatua kadhaa mbele eneo lote ulilolima limestawi majani. Haina maana kwa chama kama CDM, kutumia mabilioni ya shilingi, masaa mengi na nguvukazi nyingi za viongozi kufanya kazi ambayo haitakuwa na progressors. Wakati sasa umefika, kwa kutumia viongozi wajuu wachache wenye maadili, vyama vi-groom viongozi wenye maslahi na chama na nchi, na kuepuka hawa wapiga dili. Vyama viwe na timu za usajili, kama zilivyo club kubwa za soccer, ambazo kazi zao ni kuwa identify, pursuade, recruit and test 'wachezaji' mahiri miongoni mwa vijana ambao watawasuccess kwa maendeleo ya chama. Naamini kabisa waanzilishi na wajenzi wa chama kama CDM walikuwa na objectives zao za muda mfupi na muda mrefu. Naamini mzee Mtei, mathalani, amefanya kazi kubwa kuhakikisha wanaopata nafasi za kuingoza CDM hata sasa, wana uwezo wa kubeba ile dhamira aliyokuwa nayo alipoakianzisha. Viongozi mliopo sasa, Mbowe, Arfi, Slaa na Zitto na wengine, mna deni la kuhakikisha kuwa kesho kama sio nyie mnaoongoza CDM, then wanaoongoza wana uwezo, nia na dhamira kama mlizo nazo nyie. Wekeni timu za usajili zinazojumuisha watu makini kwenye vyuo na maeneo mengine walipo vijana, ambazo kazi yake ni kuidentify vijana potential na kuwapa taarifa, then kwa heshima kubwa viongozi wa chama wawe wanawaaproach vijana hao wajiunge na chama, na waingie katika michakato ya uchaguzi katika chama.
Demokrasia iwepo ndio, lakini wanachama wapewe fursa ya kuchagua miongoni mwa watu ambao ni tested, ili makosa yasijirudie.
Viongozi wa CDM kama ni wakati ndio huu... lakini mkichelewa hadi nafasi zenu zikashikwa na wapiga dili, mjue kuwa nguvu zenu mlizotumia, ni sawa na kusia mbegu juu ya jiwe.
Asanteni...