Vijana wambana Zitto wakitaka ajira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijana wambana Zitto wakitaka ajira

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Jan 2, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD][​IMG]
  Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe​
  Anthony Kayanda, Kigoma.
  KUNDI la vijana zaidi ya 400 wamemvamia mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe wakimtaka awatafutie ajira katika idara na taasisi mbalimbali za serikali. Vijana hao walimvaa mbunge huyo wakati wa kikao kilichofanyika katika kijiji cha Mwandiga,Wilaya ya Kigoma mkoani hapa.

  Vijana hao waliwasilisha kilio chao wakidai kwamba wamechoka kukaa vijiweni licha ya kuhitimu masomo yao katika shule na vyuo tofauti nchini, jambo linalowakatisha tamaa.

  Akiwasilisha hoja hiyo kwa niaba ya wenzake, Maulidi Mchondo ambaye ni mkazi wa Mwandiga alisema vijana wamechoka kukaa vijiweni kupiga maneno badala ya kufanya kazi zinazoweza kuwaingizia kipato na hivyo kuondokana na utegemezi kwa wazazi na walezi.

  "Sisi vijana unaotuona hapa tumemaliza masomo ya ngazi tofauti, wapo waliomaliza vyuo, wengine kidato cha sita na kidato cha nne, lakini pia wapo waliosoma na kuishia darasa la saba na wote wanatakiwa kupewa ajira zinazolingana na ujuzi na kiwango cha elimu waliyonayo, tunaomba ututafutie kazi ili tukukumbuke kwa hilo," alisema Mchondo.

  Akijibu hoja za Vijana hao, Kabwe alisema tatizo la ukosefu wa ajira ni la kitaifa zaidi na sio tatizo la Jimbo pekee, kiasi kwamba imefikia kipindi hata wasomi wanaohitimu vyuo vikuu wengine hupata shida katika kutafuta ajira serikalini au katika sekta binafsi ambazo pia ni chache na hazina nafasi nyingi za ajira.

  Alisema ili ajira zipatikane kwa wingi ni budi kwanza kuwepo na shughuli za kiuchumi na kiuzalishaji katika Jamii, ambapo kutokana na miradi inayotekelezwa kuwa mingi italazimu nafasi za ajira kuongezeka na hivyo kutoa mianya zaidi kwa vijana kujiajiri wenyewe au kuajiriwa.

  "Mimi mbunge wenu ninakusudia kuendelea kupigania miradi mingi zaidi katika Jimbo letu na Mkoa, ili vijana na makundi mengine katika jamii mpate ajira, hili litafanikiwa zaidi endapo wawekezaji niliowashawishi kuwekeza Kigoma watatimiza malengo yao kama tulivyokubaliana hili linawezekana," alisisitiza Kabwe.

  Alibainisha kwamba baadhi ya miradi inayotarajiwa kujengwa mkoani hapa ni pamoja na ile ya umeme wa vijijini, mashamba ya miwa na Kiwanda cha kusindika sukari, ujenzi wa bandari ya nchi kavu ya Katosho na hata ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami inayoendelea sasa.

  "Uwezekano wa mimi mbunge kuwapatia ajira vijana wote wa Jimbo langu sina, lakini nitajitahidi kwa kushirikiana nanyi wananchi ili tujenge mifumo mizuri ya kuinua uchumi wa Taifa kwa vile ukosefu wa ajira unakwenda sambamba na ukuaji wa uchumi, sasa kama uchumi wetu umedorora msitarajie ongezeko la ajira, litatoka wapi?" alihoji Kabwe.

  Mbunge huyo aliwaeleza vijana hao kwamba miradi inayotakiwa kutekelezwa kwa muda mfupi ataisimamia na hata ile ya kutekelezwa kwa kipindi kirefu bado ataendelea kuipa kipaumbele kwani ikikamilika itatoa tija kubwa kwa maendeleo ya wananchi wote bila kujali majimbo, Wilaya au mikoa wanayotoka.

  Aliwashauri vijana kuwa mfano bora katika Taifa kwa kufanya kazi za halali na hivyo kukuza kipato chao, sambamba na kukuza uchumi wa Taifa utakaosaidia kuongeza fursa za ajira serikalini na katika sekta binafsi.

  Lakini pia aliwaeleza vijana kwamba yeye ni Mbunge wa Jimbo zima hivyo wasilalamike pindi wanapoona baadhi ya Vijiji katika Jimbo wanapata miradi ya maendeleo, kwa vile anawajibika kupigania maendeleo ya kila mmoja ndani ya Jimbo bila kujali itikadi zao za kisiasa.

  Kabwe alisema baadhi ya miradi inayotarajiwa kutekelezwa katika Jimbo ni pamoja na ujenzi wa vituo vya Afya vya Mahembe na Ilagala, miradi ya maji katika vijiji vya Kalinzi, Nyarubanda, Nkungwe na Kagongo ambavyo vimekuwa na shida kubwa ya maji kwa kipindi kirefu.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Chanzo. Vijana wambana Zitto wakitaka ajira


  Haya tena Kaka Zitto Kabwe Watafutie Wananchi wako kazi wamechoka Kukaa Vijiweni.
   
Loading...