Kwa waliopata kuishi maeneo ambako uchimbaji dhahabu hufanyika, kuna kitu kinaitwa MARUDIO.
Yale ni mabaki ya dhahabu au niseme mabaki ya mchanga wa dhahabu. Kwa kiasi kikubwa wafanyabiashara wadogo hususani vijana huwekeza fedha zao katika marudio ili wafanye upya uchenjuaji wakibahatika wanapata dhahabu kidogo na mara nyingine hukosa kabisa na kukatika mitaji yao.
Wafanyabiashara wakongwe wa dhahabu hawathubutu kuwekeza fedha zao katika marudio maana wanajua risk ni kubwa zaidi kuliko opportunity ya kupata dhahabu. Bahati mbaya katika hili ni kwamba, hayo marudio yanapatikana kwa urahisi ukilinganisha na mwamba genuine wenye dhahabu hivyo gharama za kuwekeza ndogo sana katika marudio kuliko katika mwamba genuine.
Hiyo ndiyo tafsiri na maana halisi hata katika maisha ya kimapenzi, wazee wanajua thamani ya dogo dogo na gharama ya uwekezaji lakini kina Harmonists wanajua ni rahisi kuwekeza kwa kina Wolperists