Vijana wa Ughaibuni

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
947
Vijana wengi tumekuwa na mitazamo ya kutaka kuikimbia nchi yetu na kwenda ughaibuni kutafuta maisha na wengine wakitaka kukimbia kabisa kwa nini tuwe na mitazamo kama hiyo kwa nini? Na kwa nini tusiwe na mitazamo ya kuibadilisha nchi yetu? hata kama mifumo ya nchi yetu ni duni tukiungana mimi na wewe, yule na yule tunaweza badilisha mifumo ya nchi yetu, wote tukiwa na mitazamo hiyo hii nchi tutamwachia nani? kuna fahari kuishi katika nchi yako kuliko kuwa mgeni katika nchi za watu. Hii nchi ni yetu na ni fahari yetu na vizazi vyetu, hata nchi zilizokuwa na uchumi mkubwa na teknolojia kubwa huko nyuma katika historia zao walikuwa kama sisi na mifumo kama yetu ila walijipa moyo na kuunga na kufikia hapa walipo sasa, na sisi tunaweza. Tunaweza badilisha mifumo mibovu ya kisiasa iliyopo nchini, tunaweza badili mifumo mibovu ya serikali yetu na tunaweza badili mifumo mibovu ya vyombo vya usalama wetu. Tunaweza ijenga demokrasia tunayoitaka sisi wenyewe. Haya yote yanawezekana kama kila Mtanzania atajitambua yeye ni nani na ana umuhimu gani katika taifa hili teule na pia pale kila mtanzania atapokubali kubadilisha mitazamo yake na kuwa na mitazamo ya kujenga taifa letu.


Watanzania wengi tuna-mitazamo duni tunaamini chama tawala ndio kinaweza kuongoza taifa hili lakini si kweli, hii nchi inawatu wengi wenye mitazamo yenye manufaa na ya kuleta maendeleo katika nchi, hapa tulipofikia tumekwamishwa na chama tawala hakuna asiejua hili, ndani ya chama tawala kuna makundi ya aina mbili wanaotanguliza maslahi ya nchi na wale wanaotanguliza maslahi ya chama na yao binafsi. Kwa mtu mwenye uelewa mpana atakubali hili ila mwenye mitazamo duni hawezi kuelewa hapa. Tukijaribu kujifananisha na nchi tulizopata nazo uhuru miaka ya 1960 wenzetu wako mbali sana kiuchumi,kielimu na kiteknolojia wazee watasema vita ya Iddi Amin ilitukwamisha lakini sio hoja na si tija kwani nchi ngapi tulizopata nazo uhuru katika miaka hiyo zilitoka vitani na sasa ziko mbele kimaendeleo?

Mifumo ya chama tawala ndio iliyotukwamisha sisi na mifumo ya kisiasa kwa ujumla imechangia sana hapa tulipo, ifike hatua tukubali tulikosea, tumekosea na wazee wetu walikosea ila hatima ya kesho yetu tunaweza itengeneza, historia yetu haihusiani na kesho yetu ila inatupa muongozo tusije kosea kama hapo awali.

Vyama vyetu vya siasa vina-asilimia kubwa sana katika kubadilisha mifumo ya nchi yetu na maisha yetu pia, wengi tunashabikia vyama vya siasa kama timu za mpira ambalo si jambo sawa sana. Familia zetu zetu nazo zimekuwa zikitufanyia uamuzi wetu hasa kwenye siasa, baba na mama ni Chadema basi na motto atakaezaliwa hapo nae atalazimishwa kuwa Chadema, ukibisha utaona yatakayo kutokea, hatuwezi enenda hivi huu ni mmoja wa mitazamo inayotukwamisha sisi.

Vyama vya siasa vya hapa nchini havina miongozo au sera za kuduni juu ya namna ya kukwamua uchumi ya nchi hii, mgombea atakae taka gombea ataweka sera yake na anae kuja pia ataweka sera yake pia hili jambo si sawa sana. Jana KILIMO KWANZA kesho tena UCHUMI WA VIWANDA na ELIMU BURE, vyama pinzani navyo ndio hawana muelekeo kabisa. Lazima kila chama kiwe na mtazamo mama ya kukuza uchumi wa nchi, tupate mfano mzuri wa vyama vya siasa nchini marekani kila chama kina mtazamo mama ya namna ya kukuza uchumi wa taifa.

Vijana wa vyama vyote, wa makabila yote na jinsia zote tunaweza badilisha mifumo ya taifa hili teule tukitilia nia na kila mmoja atapoamua kutekeleza majukumu yake hasa kwa wakati stahiki. Maendeleo ya nchi hii hayawezi letwa na utawala wa chama kimoja au chama tawala pekee au vyama pinzani pekee yao kama tunataka kuleta maendeleo ya taifa hili na kama tunataka kubadili mifumo ya nchi yetu lazima tukubali kushirikiana bila kujali itkadi za vyama vyetu, tofauti zetu,dini zetu na jinsia zetu sisi wote ni sawa mbele ya macho ya mwenyezi Mungu, hamna aliejuu ya mwengine na hakuna mwenye haki juu ya mwenzie. Kukimbia nchi sio suluhu ya taifa hili, suluhu ya taifa ni sisi kubaki nchini na kurekebisha mifumo ya nchi hii. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
 
Sasa tuendelee kubaki nchini hadi lini ilhali nchi haijengeki miaka yote tangu tunazaliwa? Hii idea ya nationalism hainiingii akilini.....mimi ni global citizen....acha watu watafute life nchi nyingine maisha mafupi sana haya.
 
Mkuu haya mambo ya kuletewa sms kuwa ndugu, rafiki au jirani yuko central inakera wengi.
Kwanini watu wasiende mimi naona hata mmechelewa, tafuteni pasport msepe hata leo au kama mnaona zinasumbua zamieni tu kama hamjaishia kuolewa kama yule chalii wa arusha
 
Kwa usawa huu ukipata fursa ya kuondoka ondoka kahangaike mbele.
umenena vema sana mkuu "ukipata fursa ya kuondoka ondoka" kama aujapata iyo fursa usi force king
kama huna plan utaenda kufa bure kwenye nchi za watu!
 
Kuliko kuibadilisha hii nchi mifumo yake na kuwa kama Libya,bora nikachunge Ng'ombe za Mzungu,kubadilisha mifumo Tanzania maana yake kufanya mapinduzi ya zamu,bora niwaachie amani yenu tu.HII NCHI INA WANAFKI WENGI..
 
Back
Top Bottom