Vijana wa CHADEMA sasa wawasha taa mchana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijana wa CHADEMA sasa wawasha taa mchana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Technician, Mar 24, 2011.

 1. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  na Stephano Mango, Songea

  VIJANA wasomi wa vyuo vikuu mbalimbali nchini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamezindua rasmi kampeni ya ‘Washa taa mchana’ itakayopitishwa nchi nzima yenye malengo mbalimbali katika kuleta ukombozi wa kifikra kwa Watanzania.
  Akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi uliofanyika jana kwenye viwanja vya soko la samaki la zamani uliohudhuriwa na mamia ya wakazi wa Manispaa ya Songea na viongozi wa ngazi tofauti wa CHADEMA mkoani Ruvuma, Mratibu wa kampeni hiyo mkoani hapa, Likapo Bakari, alisema kuwa taa itawashwa mchana rasmi machi 26 kwenye viwanja vya majengo mjini hapa.
  Alisema kwa sasa inazinduliwa na kupita katika mikoa mbalimbali nchini ikiwa na lengo la kumulika na kuangaza katika kila mkoa na kuleta ukombozi wa kweli kwa Watanzania.
  Bakari alisema kuwa ukombozi huo utakuwa katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa na kwamba wanaanza na Ruvuma kwa kufanya mikutano mbalimbali ya hadhara katika kata zote za Manispaa ya Songea.
  Alisema sanjari na hilo watatoa elimu ya uraia kwa wananchi wote wa eneo husika ili waweze kuzijua haki zao, kuzitetea na kuzidai pale zinaponyang’anywa na viongozi wasio waadilifu.
  Kwa mujibu wa maelezo yake, kampeni hiyo inashirikisha jamii ya Watanzania wote bila kujali itikadi ya kichama, kidini, kikabila, kijinsia na ubaguzi wa aina yoyote ili kukabiliana na kutatua changamoto mbalimbali kama vile huduma za afya, elimu, maji na miundombinu ili Watanzania wapate ukombozi wa kweli katika taifa lao.
  Alieleza kuwa kupitia mikutano hiyo, wataihamasisha jamii namna nzuri ya kutumia rasilimali za taifa katika kujiendeleza na kujiongezea kipato cha kila siku na katika maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
  Kadhalika kuwaelimisha wananchi maana ya katiba ya nchi na umuhimu wa kudai katiba mpya itakayoundwa kwa kushirikisha wananchi wote wa Tanzania.
  Akizindua rasmi kampeni hiyo, Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Ruvuma, Joseph Fuime, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mjini Manispaa ya Songea alisema kuwa CHADEMA ni chama makini ambacho kimejikita kwa watu mbalimbali wenye mapenzi mema na rasilimali za taifa na pia wenye uchungu wa dhati na nchi yao.
  Fuime alisema kuwa moja ya shughuli za chama cha siasa chenye mlengo chanya wa kijamii ni kushirikiana na jamii moja kwa moja katika kukabiliana na kutatua changamoto mbalimbali za kijamii, kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa.
  Alisema kuwa maendeleo yoyote hayawezi kufikiwa bila ya kuwepo kwa siasa safi, hivyo wameanzisha kampeni hiyo itakayoweza kuendeleza, kukuza chama na kukitangaza kila kona ya nchi na kufungua matawi mapya mengi sehemu ambazo hazina matawi.
  Pia kuwajengea imani wananchi kuhusu dhamira ya dhati ya CHADEMA kuwakomboa kutoka mikononi mwa watu wasiolitakia mema taifa hili.
  MY OPINION:

  This is a good move.
  Keep it up you CHADEMAS.
   
 2. l

  luhwege Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 90
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Hapo tupo nyuma yao tunafuata nyayo zao
  Pia tunapongeza kila hatua inayofanywa na uongozi wa chama CDM kwani uko kwa maslahi ya wote wanyonge yeyote anayepinga kwa makusudi malengo ya CDM huyo ni fisadi wa fikra hasi, asante wanamapinduzi. Na huwezi kufanikiwa bila kupita kwenye moto na hii imejionyesha kwa CDM.
  Mungu ibariki CDM
   
Loading...