VIJANA wa CHADEMA Mwanza waja juu, wasema watakilinda chama, viongozi wao

Safi sana sasa hawa mamluki inadhihirisha kale kaasali walicholamba kutoka kwa magamba imekuwa laana na sumu sasa haitemeki! Na sasa watimuliwe!
 
Tunajua wamepandikizwa

Hizi ni kilele za mbwa mwitu hazitompata Dr Slaa

THIS IS TOTALLY RUBBISH

NAKALA KWA KIONGOZI WA HILI KUNDI Nnauye Jr[/QUOTE

SAWA MKUU LKN HAUKUWA NA SABABU YA KUCOPY TAARIFA NZIMA. HII INATUPA SHIDA SANA TUNAOTUMIA SIMU. TAFADHALI SANA UWE MAKINI NA REPY WITH QUOTE.
 
Ndimara!!!!!!!!!!! Ah!!!!!. Yule kada wa CCM?
Mkuu tunaitika ndiyo kwa taswira uliyoonesha hapa juu. Lakini kwa kuwa kiukweli sisi wengine hatutaki hata kusikia harufu ya JAMAA WA KIJANI basi ni vizuri kiongozi wetu na kipenzi Dr wa ukweli na wana CDM wote wenye kadi za Magamba wazikabidhi kadi hizo ili zihifadhiwe kwenye maktaba itakayoanzishwa na CDM makao makuu. Hakika tusidharau wingu linaloendelea maana lina athari zake kisiasa. Pili siungi mkono hata kidogo kwa hao wanojiita viongozi wa BAVICHA na matamko yao, ninafahamu chama kina mfumo wake wa kujadili mambo yake hivyo tulitarajia hao jamaa kufuata nidhamu hiyo. Wakumbuke yaliyowapata NCCR mageuzi na baadaye TLP miaka ya 2007 na kuendelea. Tusingependa yatokee CDM. Ni lazima viongozi wawe na nidhamu. Na wajiulize hayo matamko yanamfaidisha nani hasa???

matamko nowdays it is a simple way of gaining cheap political popularity from majority of the Tanzanians who can easily swayed by politicians with parochial way of outlook.mambo mengine niya kuzungumzia vyumbani mwao na sio kuja kutupigia kelele sie majirani aah!!!
 
Wana bodi wenzangu hapa jamvini, siku moja baada ya yule kijana anayeitwa Salvatory Magafu kujipatia mamlaka asiyokuwa nayo kuwasemea vijana wa Pipooooooooooz Mkoa wa Mwanza, huku akionekana dhahiri kujivika joho la CHADEMA wakati anafanya kazi za yule ibilisi wa maendeleo, siasa na demokrasia nchini, leo msemaji mkuu na rasmi wa BAVICHA mkoani Mwanza, kijana machachari kabisa, Mulebele, ametoa tamko na kauli rasmi. Cheki mistari hiyo.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KAULI YA VIJANA WA CHADEMA MKOA WA MWANZA

KWA nafasi yangu ya Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) Mkoa wa Mwanza, nimelazimika kutoa ufafanuzi na kuweka kumbukumbu sawa na kutuliza munkari ya vijana wa mkoa huu na nchi nzima kutokana na habari zilizosambazwa kwa njia mbalimbali za upashanaji habari.

Imeripotiwa katika njia hizo za upashanaji habari kuwa BAVICHA wanataka Katibu Mkuu wetu wa Chama, Dkt. Willibrod Slaa, aondoke madarakani na kwamba asipoondoka, wataandaa mandamano ya kumng’oa.

Napenda kutumia nafasi hii kusema maneno machache juu ya upuuzi huo ambao kila mtu anajua umetokana, unaratibiwa na kusimamiwa na CCM, ikiwa eti ndiyo moja ya mikakati ya Sekretarieti ya chama hicho inayoitwa kuwa ni mpya.

Kwa nafasi yangu, mimi ndiye msemaji mkuu wa masuala yote yanayohusu BAVICHA kwa mkoa wa Mwanza. Kwa mamlaka yangu ninaelewa fika vijana wa Mwanza hawajawahi, wala hawana mpango wa kubeba propaganda za CCM dhidi ya CHADEMA na viongozi wetu kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu, akiwemo Katibu Mkuu, Dkt. Slaa.

Hongera Kamanda umeonesha ukomavu wa fikra.WACHUKULIENI HATUA KALI ZA KINIDHAMU HAO MAFEDHULI.
 
Mkuu Ndimara hajawahi kuwa mbunge, ila katika uchaguzi wa mwaka 1995 akiwa NCCR Mageuzi alifanya vizuri sana kabla chama hicho hakijafanyiwa umafia na wana magamba kama wanavyotaka kuifanyia CDM. Baadaye alihamia TLP.Ni kweli ni msomi na yuko smart sana katika uandishi.

Mkuu Pangaea.
Nashukuru sana kwa sahihisho lako linalo futa makosa yangu. Nashukuru kwa hilo kaka. Naomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.

Tuendelee kuuchimba na kuupata ukweli nikiamini great thinker hawezi kuuacha upotoshi uendelee bila kuchua hatua stahiki za kuchimbua na kuupata ukweli usio acha chembe ya mashaka.
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru kamanda Libe kwa kauli hii mujarabu. Hawa wapuuzi wametangaza vita na CHADEMA na wala si Dr Slaa, na sisi tutawanyoosha sawasawa. Maana ukweli ni kuwa uwezi ukapambana kwa namna ambavyo hawa watu wanapambana, yawezekana wana hoja ila mtindo huu wa kupamba na wanachama kwa wanachama nje ya chama si unawadhalilisha wanachama wahusika bali unaathiri mwenendo na ukuaji wa chama. Nashukuru namna tamko hili lilivyoonyesha uadilifu wa kamanda Liberatus kwa kutokuonyesha mapambano kwa kusema utaratibu wa chama utafuata kwa watu walikichafua na wanaokichafua chama.

CCM watashindana, lakini hawatashinda
 
Kama CDM ingekuwa imekamata nchi baada ya uchaguzi 2010, nchi ingekuwa inayumba. Thank God ina wabunge na madiwani tu. CDM inahitaji muda zaidi kukomaa. Katika hatua ya ukuaji wa chama, CDM iko katika stage ya pili baada ya FORMING, sasa iko katika hatua ya pili; STORMING, mtatokaje hapo, time will tell very soon. Katika hii hatua tunaangalia, mtawafanyaje waasi na mtayaondoaje makundi.
 
Huyu Magafu achukuliwe hatua za kinidhamu haraka. CHADEMA ni chama cha wananchi, kuna vijana wengi wazalendo na wasionunulika na magamba. Fukuza Mara moja hii Magafu irudi kwa magamba. Aluta continua
 
Ccm siku zako za kutawala zinahesabika, nape bw.mdogo utaficha wapi uso wako novemba 2015? Rage na kinana, somalia kuna amani sasa rudini kwenu jamani hatuwataki!! Mtamaliza wanyama kwenye hifadhi zetu.
 
Mimi nilibatizwa Anglican! Nikapewa cheti cha ubatizo na bado ninacho. Lakini nilibadili dini na kuwa mkatoliki! Sasa nani atanilazimisha kwamba Mimi ni Anglican kwa sababu ya cheti??
 
...Kwa namna anavyofanya kazi zake, tangu akiwa bungeni, namna alivyotaja "orodha ya mafisadi (list of shame) iliyohusisha viongozi wa Serikali na CCM, alivyoombwa kugombea urais na kuungwa mkono na watanzania, anavyosimamia utendaji wa CHADEMA na kuhakikisha chama chetu kinatekeleza wajibu wake katika kila jukwaa dhidi ya serikali ya CCM, ni kijana mpuuzi na msaliti anaweza kusimama kumnyooshea kidole kwa kutumia propaganda za CCM na vibwagizo vya Nape Nnauye na CCM......

Hili tamko linaonyesha kweli ni vijana wa chadema ninayoijua!!
Hawa vijana ndiyo tutakaowabidhi nchi yetu, ambao sio rahisi kurubuniwa kijinga!!!
 
KAULI YA VIJANA WA CHADEMA MKOA WA MWANZA

KWA nafasi yangu ya Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) Mkoa wa Mwanza, nimelazimika kutoa ufafanuzi na kuweka kumbukumbu sawa na kutuliza munkari ya vijana wa mkoa huu na nchi nzima kutokana na habari zilizosambazwa kwa njia mbalimbali za upashanaji habari.

Imeripotiwa katika njia hizo za upashanaji habari kuwa BAVICHA wanataka Katibu Mkuu wetu wa Chama, Dkt. Willibrod Slaa, aondoke madarakani na kwamba asipoondoka, wataandaa mandamano ya kumng’oa.

Napenda kutumia nafasi hii kusema maneno machache juu ya upuuzi huo ambao kila mtu anajua umetokana, unaratibiwa na kusimamiwa na CCM, ikiwa eti ndiyo moja ya mikakati ya Sekretarieti ya chama hicho inayoitwa kuwa ni mpya.

Kwa nafasi yangu, mimi ndiye msemaji mkuu wa masuala yote yanayohusu BAVICHA kwa mkoa wa Mwanza. Kwa mamlaka yangu ninaelewa fika vijana wa Mwanza hawajawahi, wala hawana mpango wa kubeba propaganda za CCM dhidi ya CHADEMA na viongozi wetu kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu, akiwemo Katibu Mkuu, Dkt. Slaa.

Natumia fursa hii kuwaondolea wasiwasi vijana wa CHADEMA mahali kokote ndani na nje ya nchi, vijana wa Mwanza tuko imara kukilinda chama chetu na viongozi wetu dhidi ya propaganda za CCM na serikali ambazo zina lengo ya kudhoofisha harakati za kujenga taasisi imara inayobeba matumaini ya Watanzania kwa ajili ya ukombozi wa awamu ya pili.

Natumia nafasi hii pia kuwataka vijana wa CHADEMA Mkoa wa Mwanza watulie, wakisubiri BAVICHA Mkoa ifanye maamuzi kwa kuzingatia maslahi mapana ya umma wa Watanzania na chama chetu dhidi ya hila, njama na uchu wa mtu mmoja mmoja miongoni mwetu ambaye anaamua ‘kufika bei’ na kubeba propaganda za CCM.

Napenda kuwaambia vijana wa CHADEMA kuwa mapambano ambayo chama chetu kinayaendesha kiasi cha kutishia CCM kuendelea kuwepo madarakani mwaka 2014 na 2015, ni mapambano ya haki dhidi ya udhalimu, ni mapambano ya matumaini dhidi ya kukataa tama, ni mapambano ya uadilifu dhidi ya ufisadi.

NB.
Mbali na tamko hilo wale vijana walionunuliwa na kujiita viongozi wa Bavicha wana safiri kesho kwenda Mara na wengine kwenda Mbeya. Wamepewa pesa nyingi sana kwa nia na madhumuni waliyo tangaza kupitia baadhi ya vyombo vya habari kule Mwanza.
 
maskin hela za rumumba zinavoenda bure si nibora hata wangekopesha vijana wakajiajiri mkasema mmetoa ajira badala ya kuumia hizo pesa eti kuzima kiu ya watanzania tena walio wengi!shame on you magamba
 
Kwa nafasi yangu, mimi ndiye msemaji mkuu wa masuala yote yanayohusu BAVICHA kwa mkoa wa Mwanza. Kwa mamlaka yangu ninaelewa fika vijana wa Mwanza hawajawahi, wala hawana mpango wa kubeba propaganda za CCM dhidi ya CHADEMA na viongozi wetu kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu, akiwemo Katibu Mkuu, Dkt. Slaa.


Ni akili iliyotulia. Inayojua na kuthamini wajibu. Inayojali maslahi na mahitaji ya umma wa Watanzania, inaweza kusema maneno ya busara kama haya. Mulubele kama ninakuona vile na ule uwezo wako wa kujenga hoja na kushawishi. Wasiojua heshima uliyojijengea ndani ya chama, ni vyema wakajua kuwa wewe ndiye ulitoboa siri ya mpango wa rushwa iliyokuwa inagawiwa kwa njia ya Mpesa, tigo pesa na airtel money na mmoja wa wagombea uenyekiti ambaye baadae aliondolewa kwa tuhuma hizo. Pamoja na maisha yako ya kawaida tu, lakini kijana kutoka United Kingdom of Ukerewe, ulionesha umahiri wa kusimamia haki na ukweli, ukawaumbua. Asante mkubwa.
 
Kwa taarifa zaidi ni kwamba vijana wale wasaliti kesho watakuwa Mara na baada ya hapo wataelekea kwa Kinega (Mbeya) wamepewa fedha nyingi kwa ajili ya mpango ambao bila shaka unakufa leo usiku maana nafsi zitakuwa zinawasuta.
 
Back
Top Bottom