VIJANA wa CHADEMA Mwanza waja juu, wasema watakilinda chama, viongozi wao

Chief Isike

Chief Isike

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2010
Messages
445
Points
195
Chief Isike

Chief Isike

JF-Expert Member
Joined Jan 17, 2010
445 195
Wana bodi wenzangu hapa jamvini, siku moja baada ya yule kijana anayeitwa Salvatory Magafu kujipatia mamlaka asiyokuwa nayo kuwasemea vijana wa Pipooooooooooz Mkoa wa Mwanza, huku akionekana dhahiri kujivika joho la CHADEMA wakati anafanya kazi za yule ibilisi wa maendeleo, siasa na demokrasia nchini, leo msemaji mkuu na rasmi wa BAVICHA mkoani Mwanza, kijana machachari kabisa, Mulebele, ametoa tamko na kauli rasmi. Cheki mistari hiyo.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KAULI YA VIJANA WA CHADEMA MKOA WA MWANZA

KWA nafasi yangu ya Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) Mkoa wa Mwanza, nimelazimika kutoa ufafanuzi na kuweka kumbukumbu sawa na kutuliza munkari ya vijana wa mkoa huu na nchi nzima kutokana na habari zilizosambazwa kwa njia mbalimbali za upashanaji habari.

Imeripotiwa katika njia hizo za upashanaji habari kuwa BAVICHA wanataka Katibu Mkuu wetu wa Chama, Dkt. Willibrod Slaa, aondoke madarakani na kwamba asipoondoka, wataandaa mandamano ya kumng’oa.

Napenda kutumia nafasi hii kusema maneno machache juu ya upuuzi huo ambao kila mtu anajua umetokana, unaratibiwa na kusimamiwa na CCM, ikiwa eti ndiyo moja ya mikakati ya Sekretarieti ya chama hicho inayoitwa kuwa ni mpya.

Kwa nafasi yangu, mimi ndiye msemaji mkuu wa masuala yote yanayohusu BAVICHA kwa mkoa wa Mwanza. Kwa mamlaka yangu ninaelewa fika vijana wa Mwanza hawajawahi, wala hawana mpango wa kubeba propaganda za CCM dhidi ya CHADEMA na viongozi wetu kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu, akiwemo Katibu Mkuu, Dkt. Slaa.

Natumia fursa hii kuwaondolea wasiwasi vijana wa CHADEMA mahali kokote ndani na nje ya nchi, vijana wa Mwanza tuko imara kukilinda chama chetu na viongozi wetu dhidi ya propaganda za CCM na serikali ambazo zina lengo ya kudhoofisha harakati za kujenga taasisi imara inayobeba matumaini ya Watanzania kwa ajili ya ukombozi wa awamu ya pili.

Natumia nafasi hii pia kuwataka vijana wa CHADEMA Mkoa wa Mwanza watulie, wakisubiri BAVICHA Mkoa ifanye maamuzi kwa kuzingatia maslahi mapana ya umma wa Watanzania na chama chetu dhidi ya hila, njama na uchu wa mtu mmoja mmoja miongoni mwetu ambaye anaamua ‘kufika bei’ na kubeba propaganda za CCM.

Napenda kuwaambia vijana wa CHADEMA kuwa mapambano ambayo chama chetu kinayaendesha kiasi cha kutishia CCM kuendelea kuwepo madarakani mwaka 2014 na 2015, ni mapambano ya haki dhidi ya udhalimu, ni mapambano ya matumaini dhidi ya kukataa tama, ni mapambano ya uadilifu dhidi ya ufisadi.

Katika kusimamia masuala hayo, Katibu Mkuu CHADEMA, Dkt. Slaa akiwa mtendaji mkuu wa chama amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha CCM inadhoofika kabisa na CHADEMA inaendelea kuwa tumaini jipya la huru wa kweli, mabadiliko ya mfumo na utawala, baada ya uchaguzi mkuu 2015.

Vijana wa Mwanza, kama walivyo vijana wote walio wanachama makini wa CHADEMA, tunatambua Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992, inayosimamia shughuli zote za vyama vya siasa nchini inasema wazi mtu aliyekuwa mwanachama wa chama X akiamua kujiunga chama Y, ‘automatically’ anapoteza uanachama wa chama cha awali.

Lakini pia tunatambua kuwa katiba za vyama vya siasa, ikiwemo Katiba ya CCM, zinasema wazi kuwa mwanachama wa chama hicho akijiunga na chama kingine, anapoteza uanachama wake kwa chama hicho cha awali automatically.

Lakini pia vijana wa CHADEMA Mwanza ambao ni makini kama ilivyo kawaida ya vijana wa CHADEMA, tunaelewa wazi na tunaweza kusimamia kauli hii, kuwa Katibu Mkuu Dkt. Slaa tangu alipohama CCM mwaka 1995 hajawahi, kwa maana ya kila mwaka, kwenda ofisi yoyote ya CCM kulipia kadi yake kuhuisha uanachama kwenye chama hicho alichokiacha kinachokufa, kikisubiri kuzikwa rasmi mwaka 2014 na 2015. Tunatambua kwamba Dr Slaa ni mwachama hai wa CHADEMA na si mwanachama wa CCM.

Kwa namna anavyofanya kazi zake, tangu akiwa bungeni, namna alivyotaja “orodha ya mafisadi (list of shame) iliyohusisha viongozi wa Serikali na CCM, alivyoombwa kugombea urais na kuungwa mkono na watanzania, anavyosimamia utendaji wa CHADEMA na kuhakikisha chama chetu kinatekeleza wajibu wake katika kila jukwaa dhidi ya serikali ya CCM, ni kijana mpuuzi na msaliti anaweza kusimama kumnyooshea kidole kwa kutumia propaganda za CCM na vibwagizo vya Nape Nnauye na CCM.

Natangaza rasmi kuwa BAVICHA Mwanza haijafanya maamuzi ya kuendesha harakati zozote za kutaka Dkt. Slaa ajiuzulu, wala haitambui maandalizi ya maandamano kwani ni batili na aliyetoa tamko la jana, Salvatory Magafu si msemaji wa vijana wa CHADEMA Mkoa wa Mwanza, na hivyo baraza litakaa kujadili utovu huu wa nidhamu wa kiwango na kuchukua hatua stahiki.

BAVICHA Mwanza inaheshimu taratibu za kikatiba wa viongozi kutokutuhumiana kwenye vyombo vya habari, hivyo nimetoa kauli yangu kama Msemaji wa BAVICHA ngazi ya Mkoa hapa Mwanza ili kuweka kumbukumbu sahihi kwa umma na maamuzi mengine yataendelea kufanywa kwa mujibu wa katiba, kanuni, maadili na itifaki ya chama.

Liberatus B. Mulebele.

Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Mwanza.
 
Kachanchabuseta

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2010
Messages
7,280
Points
1,195
Kachanchabuseta

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2010
7,280 1,195
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KAULI YA VIJANA WA CHADEMA MKOA WA MWANZA

KWA nafasi yangu ya Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) Mkoa wa Mwanza, nimelazimika kutoa ufafanuzi na kuweka kumbukumbu sawa na kutuliza munkari ya vijana wa mkoa huu na nchi nzima kutokana na habari zilizosambazwa kwa njia mbalimbali za upashanaji habari.

Imeripotiwa katika njia hizo za upashanaji habari kuwa BAVICHA wanataka Katibu Mkuu wetu wa Chama, Dkt. Willibrod Slaa, aondoke madarakani na kwamba asipoondoka, wataandaa mandamano ya kumng'oa.

Napenda kutumia nafasi hii kusema maneno machache juu ya upuuzi huo ambao kila mtu anajua umetokana, unaratibiwa na kusimamiwa na CCM, ikiwa eti ndiyo moja ya mikakati ya Sekretarieti ya chama hicho inayoitwa kuwa ni mpya.

Kwa nafasi yangu, mimi ndiye msemaji mkuu wa masuala yote yanayohusu BAVICHA kwa mkoa wa Mwanza. Kwa mamlaka yangu ninaelewa fika vijana wa Mwanza hawajawahi, wala hawana mpango wa kubeba propaganda za CCM dhidi ya CHADEMA na viongozi wetu kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu, akiwemo Katibu Mkuu, Dkt. Slaa.

Natumia fursa hii kuwaondolea wasiwasi vijana wa CHADEMA mahali kokote ndani na nje ya nchi, vijana wa Mwanza tuko imara kukilinda chama chetu na viongozi wetu dhidi ya propaganda za CCM na serikali ambazo zina lengo ya kudhoofisha harakati za kujenga taasisi imara inayobeba matumaini ya Watanzania kwa ajili ya ukombozi wa awamu ya pili.

Natumia nafasi hii pia kuwataka vijana wa CHADEMA Mkoa wa Mwanza watulie, wakisubiri BAVICHA Mkoa ifanye maamuzi kwa kuzingatia maslahi mapana ya umma wa Watanzania na chama chetu dhidi ya hila, njama na uchu wa mtu mmoja mmoja miongoni mwetu ambaye anaamua ‘kufika bei' na kubeba propaganda za CCM.

Napenda kuwaambia vijana wa CHADEMA kuwa mapambano ambayo chama chetu kinayaendesha kiasi cha kutishia CCM kuendelea kuwepo madarakani mwaka 2014 na 2015, ni mapambano ya haki dhidi ya udhalimu, ni mapambano ya matumaini dhidi ya kukataa tama, ni mapambano ya uadilifu dhidi ya ufisadi.

Katika kusimamia masuala hayo, Katibu Mkuu CHADEMA, Dkt. Slaa akiwa mtendaji mkuu wa chama amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha CCM inadhoofika kabisa na CHADEMA inaendelea kuwa tumaini jipya la huru wa kweli, mabadiliko ya mfumo na utawala, baada ya uchaguzi mkuu 2015.

Vijana wa Mwanza, kama walivyo vijana wote walio wanachama makini wa CHADEMA, tunatambua Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992, inayosimamia shughuli zote za vyama vya siasa nchini inasema wazi mtu aliyekuwa mwanachama wa chama X akiamua kujiunga chama Y, ‘automatically' anapoteza uanachama wa chama cha awali.

Lakini pia tunatambua kuwa katiba za vyama vya siasa, ikiwemo Katiba ya CCM, zinasema wazi kuwa mwanachama wa chama hicho akijiunga na chama kingine, anapoteza uanachama wake kwa chama hicho cha awali automatically.

Lakini pia vijana wa CHADEMA Mwanza ambao ni makini kama ilivyo kawaida ya vijana wa CHADEMA, tunaelewa wazi na tunaweza kusimamia kauli hii, kuwa Katibu Mkuu Dkt. Slaa tangu alipohama CCM mwaka 1995 hajawahi, kwa maana ya kila mwaka, kwenda ofisi yoyote ya CCM kulipia kadi yake kuhuisha uanachama kwenye chama hicho alichokiacha kinachokufa, kikisubiri kuzikwa rasmi mwaka 2014 na 2015. Tunatambua kwamba Dr Slaa ni mwachama hai wa CHADEMA na si mwanachama wa CCM.

Kwa namna anavyofanya kazi zake, tangu akiwa bungeni, namna alivyotaja "orodha ya mafisadi (list of shame) iliyohusisha viongozi wa Serikali na CCM, alivyoombwa kugombea urais na kuungwa mkono na watanzania, anavyosimamia utendaji wa CHADEMA na kuhakikisha chama chetu kinatekeleza wajibu wake katika kila jukwaa dhidi ya serikali ya CCM, ni kijana mpuuzi na msaliti anaweza kusimama kumnyooshea kidole kwa kutumia propaganda za CCM na vibwagizo vya Nape Nnauye na CCM.

Natangaza rasmi kuwa BAVICHA Mwanza haijafanya maamuzi ya kuendesha harakati zozote za kutaka Dkt. Slaa ajiuzulu, wala haitambui maandalizi ya maandamano kwani ni batili na aliyetoa tamko la jana, Salvatory Magafu si msemaji wa vijana wa CHADEMA Mkoa wa Mwanza, na hivyo baraza litakaa kujadili utovu huu wa nidhamu wa kiwango na kuchukua hatua stahiki.

BAVICHA Mwanza inaheshimu taratibu za kikatiba wa viongozi kutokutuhumiana kwenye vyombo vya habari, hivyo nimetoa kauli yangu kama Msemaji wa BAVICHA ngazi ya Mkoa hapa Mwanza ili kuweka kumbukumbu sahihi kwa umma na maamuzi mengine yataendelea kufanywa kwa mujibu wa katiba, kanuni, maadili na itifaki ya chama.

Liberatus B. Mulebele.

Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Mwanza.
Tunajua wamepandikizwa

Hizi ni kilele za mbwa mwitu hazitompata Dr Slaa

THIS IS TOTALLY RUBBISH

NAKALA KWA KIONGOZI WA HILI KUNDI Nnauye Jr
 
Kachanchabuseta

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2010
Messages
7,280
Points
1,195
Kachanchabuseta

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2010
7,280 1,195
Haya matamko ya vichaa hayatasadia chochote

CD imegoma hapa mnakuja na single nyingine

Totally Rubbish
 
Kachanchabuseta

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2010
Messages
7,280
Points
1,195
Kachanchabuseta

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2010
7,280 1,195
Unahitaji akili za MAITI KUMEZA HII propaganda ya Nnauye Jr
 
Last edited by a moderator:
OKW BOBAN SUNZU

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2011
Messages
26,273
Points
2,000
OKW BOBAN SUNZU

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2011
26,273 2,000
....masikini mradi wa kina Mwampamba, Chagulani na Shoza unafeli kabla hata ya kuzinduliwa........tatizo ni nini TUTEMENKE, ni mtaji mdogo au ni kodi ilikuwa kubwa sana
 
Chief Isike

Chief Isike

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2010
Messages
445
Points
195
Chief Isike

Chief Isike

JF-Expert Member
Joined Jan 17, 2010
445 195
Unahitaji akili za MAITI KUMEZA HII propaganda ya Nnauye Jr
Mwanabodi Jeykey, mtu akikusoma kwenye zile posts zako mbili hapo mwanzo ataona au kujua unapingana na tamko la Mulebele hili la leo na hivyo unawasapoti wale traitors. Mpaka aje akutane na hii post yako ya tatu, kama ni mtu makini, atakuwa ameshatoka povu kwa kujiandaa kukujibu katika zile mbili za mwanzo. Ziangalie vyema. Ushauri tu. tuko pamoja for pipoooooooooooooz.
 
Last edited by a moderator:
Kachanchabuseta

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2010
Messages
7,280
Points
1,195
Kachanchabuseta

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2010
7,280 1,195
Welcome tutemenke

Last edited by a moderator:
M

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
13,355
Points
2,000
M

Molemo

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
13,355 2,000
Hawana ubavu wowote wa kutishia nyau hawa mamluki wachache.Tunakushukuru Mkiti kuweka kumbukumbu sawa.
 
N

Ngonini

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2010
Messages
2,024
Points
1,195
N

Ngonini

JF-Expert Member
Joined Sep 1, 2010
2,024 1,195
Imetulia sana maana haijaweka jaziba kwenye namna ya kumshughulikia huyu katibu mchumia tumbo!
 
Kachanchabuseta

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2010
Messages
7,280
Points
1,195
Kachanchabuseta

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2010
7,280 1,195
Hii CD @Tuntemke, Nnauye Jr, Ritz naona imegoma

I think all member group wana DEAD BRAIN

M

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
13,355
Points
2,000
M

Molemo

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
13,355 2,000
....masikini mradi wa kina Mwampamba, Chagulani na Shoza unafeli kabla hata ya kuzinduliwa........tatizo ni nini TUTEMENKE, ni mtaji mdogo au ni kodi ilikuwa kubwa sana
Waseme tuwachangie mkuu wangu.
 
Kachanchabuseta

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2010
Messages
7,280
Points
1,195
Kachanchabuseta

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2010
7,280 1,195
Imetulia sana maana haijaweka jaziba kwenye namna ya kumshughulikia huyu katibu mchumia tumbo!
hII propaganda yenu haijashika imeishakufa haina mashiko
 
E

Earthmover

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2012
Messages
15,283
Points
2,000
E

Earthmover

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2012
15,283 2,000

....Napenda kuwaambia vijana wa CHADEMA kuwa mapambano ambayo chama chetu kinayaendesha kiasi cha kutishia CCM kuendelea kuwepo madarakani mwaka 2014 na 2015,
.....ni mapambano ya haki dhidi ya udhalimu, ni mapambano ya matumaini dhidi ya kukataa tamaa ni mapambano ya uadilifu dhidi ya ufisadi.......

..... nimapambano dhidi ya majangili yaliyopo LUMUMBA....
 
M

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
13,355
Points
2,000
M

Molemo

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
13,355 2,000

....Napenda kuwaambia vijana wa CHADEMA kuwa mapambano ambayo chama chetu kinayaendesha kiasi cha kutishia CCM kuendelea kuwepo madarakani mwaka 2014 na 2015,
.....ni mapambano ya haki dhidi ya udhalimu, ni mapambano ya matumaini dhidi ya kukataa tamaa ni mapambano ya uadilifu dhidi ya ufisadi.......

..... nimapambano dhidi ya majangili yaliyopo LUMUMBA....
Ni mapambano dhidi ya wasomali wasio Raia wanaopewa uongozi kwenye vyama vya siasa
 
mayoscissors

mayoscissors

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2009
Messages
964
Points
250
Age
41
mayoscissors

mayoscissors

JF-Expert Member
Joined Nov 24, 2009
964 250
WAnaccm wana akili za maiti
 
Kachanchabuseta

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2010
Messages
7,280
Points
1,195
Kachanchabuseta

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2010
7,280 1,195
Tatizo la hawa vijana wa Lumumba kwa mgongo wa nyuma
wanaona wakipambana na CDM ndo umaarufu

Hii ndio tatizo la hawa vijana wa Nnauye Jr
 
Last edited by a moderator:
AdvocateFi

AdvocateFi

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Messages
11,355
Points
2,000
AdvocateFi

AdvocateFi

JF-Expert Member
Joined Jan 15, 2012
11,355 2,000
Yeah! Huyo kamanda mwenyekiti wa BAVICHA mwanza nampata vyema kuwa ni mtu makini sana na ndiyo huyu aliyewaumbua wale vijana wanafiki na tuhuma za rushwa that time kwenye uchaguzi wa BAVICHA mwaka jana.
Kamanda umesomeka sana..... Na hakuna mwendawazimu yeyote kama wale vijana tumbo watakaoweza kukitingisha chama na Dr. Wa ukweli....
 
AdvocateFi

AdvocateFi

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Messages
11,355
Points
2,000
AdvocateFi

AdvocateFi

JF-Expert Member
Joined Jan 15, 2012
11,355 2,000
....masikini mradi wa kina Mwampamba, Chagulani na Shoza unafeli kabla hata ya kuzinduliwa........tatizo ni nini TUTEMENKE, ni mtaji mdogo au ni kodi ilikuwa kubwa sana
hao ni mashetwani tu.
 
Forum statistics

Threads 1,285,942
Members 494,834
Posts 30,880,022
Top