MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 12,841
- 28,807
Habari JF,
Leo nimeona nitoe maoni yangu katika hili suala la ujasiriamali nikiwa pia mjasiriamali mdogo ninayezikimbiza ndoto zangu.
Mimi ninaongelea suala la ubunifu linalobebwa na ujasiri katika utekelezaji. Kwa kupitia thread nyingi hapa jukwaani nimegundua wengi wetu sio wabunifu au waoga wa kufanya tunachokiamini au tulichojaliwa na Mungu. Humu thread nyingi ni kuhusu ufugaji wa kuku, samaki, mbuzi, utengenezaji wa sabuni, shampoo na kadhalika. Pia na mambo ya biashara za network kama GNLD na nyinginezo. Mimi ninaamini kuna mambo mengi nje ya hayo ambayo yamekuwa kama fasheni. Niwasihi vijana wenzangu kwani pia ninaamini vijana wengi wana vipaji na uthubutu wa kufanya mambo mengi zaidi. Tusiegemee kwenye mambo machache tutakwama. Sio lazima wote tufuge kuku au kujiunga Forever, rifaro.