Vijana tuwe makini na tiba mbadala

orangutan

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
757
773
Wiki kama tatu hivi zilizopita alitokea mganga mmoja wa tiba za asili pale Mwenge. Akatukuta vijana kibao tumekaa chimbo pale uwanja wa vinyago pembeni ya jengo la bodi ya mikopo, wengine tunacheki mechi huku wengine wakiwa wamekuja kuchoma wida.

Mganga huyu ni mtu mwenye umri wa makamo na heshima zake afu anabonga kinyama utadhani anatafuna karanga za moto kinywani. Amebeba begi lake kubwa amejaza madawa yake ya asili katika mfumo wa mizizi, ungaunga na mengine yamefungwa kwenye vipakiti vidogo na kwenye vijiboksi.

Akaanza kutiririka na kuinadi bidhaa aliyokuwa anaiuza. Jamaa yuko deep ile mbaya! Anaujua vyema mfumo wa mwili wa binadamu na namna unavyofanya kazi- mshipa kwa mshipa, msuli kwa msuli, kiungo kwa kiungo. Watu kibao tukavutiwa na sera za jamaa tukamzunguka huku tukimsikiliza kwa makini na kumuuliza baadhi ya maswali ambayo aliyajibu kiufasaha kabisa bila kubabaika.

Aisee nimegundua kwamba watanzania wengi ni wagonjwa! Watu zaidi ya sabini pale vijana kwa wazee wengine wameacha na shughuli zao za kuchonga vinyago tukawa tumevutiwa na tiba za jamaa. Huyu anataka dawa ya ngiri, huyu anataka ya kurefusha na kunenepesha, huyu anataka ya kuongeza nguvu, huyu anataka ya kuacha kuvuta sigara, huyu anataka ya presha nk nk nk.

Jamaa akala vichwa vya kutosha, dozi yake anaiuza kwa shilingi elfu kumi ila hata kama una buku tano anakurekebishia. Akauza dawa kibao zingine anadai zinatoa sumu mwilini ati zinasafisha maini, figo, kibofu, damu nk. Akadai ukitumia hizo dawa basi ukienda chooni utajisaidia kinyesi kiroba kizima na utakojoa mkojo mweusi na mchafu kama damu au chai kwasababu ya sumu zilizotujaa watanzania.
P3100910.JPG


Watu tukamwelewa na tukamuomba na contacts zake ili tuweze kumpatia feedback kuhusiana na namna tiba ilivyofanya kazi. Akakusanya fedha zaidi ya laki tatu afu akasepa zake!

MATOKEO YAKE SASA!
Watu tukaenda majumbani mwetu na hatukutaka kuchelewa kuitumia hii dawa mkombozi. Kila mtu akaitumia kulingana na namna alivyoelekezwa. We bwana we! Ilipofika kesho yake kila mtu anakuja pale kijiweni kachoooka. Wengine wameharisha vibaya siku nzima, wengine tumekojoa mkojo kama kahawa, wengine sijui wameuziwa mikuyati wameishia kudindisha siku nzima, wengine hata hawajielewi. Tukampigia simu kwamba dokta vipi mbona watu tunableed tukienda kukojoa jamaa anadai kwamba ati dawa ndo inafanya kazi na kwamba tusubirie matokeo yake baada ya siku kadhaa.

Baada ya kama wiki hivi kila mtu akawa anakuja na stori yake. Hakuna matokeo positive yoyote ambayo vijana wameyapata. Vibamia wamebaki na Vibamia vyao, wale wa kukojoa dakika mbili nao hakuna mabadiliko, wenye presha, visukari nk. Laki tatu zetu zimeenda! Tunampigia simu bwana daktari anasema eti tumekosea masharti!

Sasa vijana wameapa kwamba siku wakija kumtia nguvuni huyo tapeli watahakikisha jamaa anajuta kuzaliwa. Nasikia sasa hivi yuko pande za Kimara anazidi kula vichwa huko, sijui anaelekea wapi Tanga au Morogoro bila shaka.

Huu ni ushuhuda tu na tahadhari kwa wale wote wapenzi wa tiba mbadala hasa kutoka kwa waganga ambao hawana hata leseni wala vyeti. Watakuja kutumaliza hawa watu, badala ya kuponya wanazidi kuongeza ubovu na maradhi mengine kwenye miili yetu. Mtu unataka dawa ya presha yeye anakuuzia Mkuyati what do you expect?
 
Kuna wanaokula vichwa kwenye mabasi ya mikoani huwa nawashangaa sana abiria wanaodanganyika! Tiba mbadala, manabii, waganga, na get rich quick pyramid schemes ...zanavuna sana watanzania wenzetu...nafikiri wengi tumekata tamaa tunatafuta faraja kwenye chochote chenye dalili ya kufariji!
 
Eti wanataka kuukosoa uumbaji wa Mungu.hakuna anayeweza apo sembuse mzungu ameshindwa
 
kuna mmoja anapiga hela kwenye mabas ya mkoa,hada dar to arusha anajiiita dr.yusuf sang hta fb yupo. yan yuko deep sana na hii ni ili awateke watu. ila ni tapel
 
kuna mmoja anapiga hela kwenye mabas ya mkoa,hada dar to arusha anajiiita dr.yusuf sang hta fb yupo. yan yuko deep sana na hii ni ili awateke watu. ila ni tapel
Mkuu hawa jamaa matapeli tu. Na akishawapiga hela sehemu moja harudi tena.
 
Back
Top Bottom