Vijana turudi vijijini tununue ardhi ya kilimo

Vijana turudi vijijini tununue ardhi ya kilimo

WEKKI

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2014
Posts
477
Reaction score
146
VIJANA TURUDI VIJIJINI TUNUNUE ARDHI

Na Eng AYUB MASSAU

Habari ndugu watanzania popote mlipo katika kuijenga nchi yetu ya Tanzania na kuhakikisha tunafikia nchi ya uchumi wa kati kama dira ya Taifa ya maendeleo 2000-2025inavyosema, naamini tukifika huko kila mtanzania atajivunia kwa namna alivyofanikisha mchango wake katika Taifa hili na historia ya vizazi na vizazi itamkumbuka.Leo katika tafakuri yangu, nitajikita kuzungumzia umuhimu wa kununua ardhi na namna ilivyonufaisha vijana wengi katika harakati za kujikomboa na umaskini na kuondokana na dhana ya kuamini maisha bora na mazuri yanapatikana mijini tu.

Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoona mbali na kufanikiwa kudhibiti ardhi kuwa mali ya serikali tofauti na baadhi ya nchi ambazo ardhi ni sio mali ya serikali kabisa bali ni ya mtu na huiuzia serikali ardhi pindi serikali itapoitaka kwa ajili ya kufanyia maendeleo, mambo kama haya lazima watanzania wayajue na kutambua umuhimu wa ardhi kuwa chini ya serikali ,japo sisi kama Tanzania tuna matatizo ya migogoro ya ardhi baina ya wawekezaji na wananchi na wakati mwingine wakulima na wafanyakazi , hii haiondoi uhalali wa ardhi ya Tanzania kuwa mikononi salama.

Ardhi ikitungiwa sera mbovu katika umiliki wake husababisha madhara makubwa baadae kwani wenye uwezo wa kifedha ndio watakuwa na uwezo wa kumiliki ardhi kubwa na wananchi wa kipato cha chini itabidi wakodi ardhi kwa wenye ardhi (makabaila )na kufanya shughuli za kilimo na za maendeleo au kuajiriwa katika katika mashamba yao na kufanya kazi kama vibarua.

Hii hali iko nchini kenya ambapo kutokana na sera zao za ubepari ndizo zilizofanya wakafika hapo na kutengeneza tabaka kubwa kati walionacho na wasionacho tofauti na sisi Tanzania ambapo mfumo wa ujamaa ulijenga usawa katika mali za umma na ndio matunda tuyaonayo leo ya kila mtanzania ana haki ya kumiliki ardhi ilimradi afuate taratibu husika, mfano hai ambao wengi mtakuwa na kumbukumbu nao ni ule mvutano uliokuwapo wa kuhusu kujenga bomba la mafuta kutoka uganda , katika mvutano huu Tanzania na kenya zilivutana nani ni nani? na nani anastahili kupata mradi huo?

Kwa Upande wetu Tanzania ardhi haikuwa shida kutokana na sera zetu za ardhi na kila Mtanzania analitambua hilo ,lakini kwa kenya ilikuwa tofauti kidogo kwani ardhi ilikuwa inamilikiwa na makabaila ambao walikuwa wanajipanga kuizia ardhi serikali ya kenya ili ipitishe bomba la mafuta kutoka hoima nchini uganda mpaka bandari ya lamu nchini kenya. Hii ndio tofauti iliyopo katika umilikaji ardhi wa Tanzania na nchi nyingine hasa za kiafrika.

Nimejaribu kueleza kwa mifano ili wasomaji muelewe kwanini ardhi ni muhimu mahala popote pale lakini sera zikiwa mbovu ardhi hugeuka laana isiyokwisha, Vijana wa Tanzania wengi leo wanaamini mijini ndio kuna maisha kuliko vijijini siwalaumu bali haya ndio mazingira tuliyojengewa na kuamini katika maendeleo ya majumba mazuri na sio rasilimali ardhi ambayo ndio matokeo ya kila kitu na maendeleo yaliyopo duniani,Vijana wa kitanzania huu ni muda wa kurudi vijijini na kununua ardhi ya kwa ajili ya maendeleo ya sasa na baadae, nashawishika kuyaandika haya kwa ushahidi wa kuona na kutumia msemo usemao " ukitaka mali utaikuta shambani" ambapo bila ardhi hakuna shamba na bila shamba hakuna ardhi.

Nikiwa mkoani kagera , katika maeneo mbalimbali nimekuta ardhi inauzwa kwa heka moja ni Shillingi za kitanzania 200,000 hadi 300,000/= pesa hii ni nyingi kwa mtanzania wa maisha ya kawaida lakini ni ndogo kwa maendeleo yenye uhakika, leo ardhi inapanda bei sana kila kukicha kwa sababu ardhi ni mali, ardhi ni mtaji na ardhi ni rasilimali isiyoshuka thamani bali huongezeka kila kukicha, Kijana unaweza kununua ardhi kijijini kwa kiasi unachokitaka na kuindeleza kwa kupanda miti ya mbao , miche ya matunda n.k

Baada ya miaka kuanzia 3 mpaka 5 toka upande mazao yako, yatakuwa yamekuwa na kukomaa kwa kiasi kikubwa kupitia ardhi hiyo yenye miti au miti ya machungwa itakufanya ukopesheke na benki yoyote tena pesa nyingi na kukufanya kutoka kuajiriwa na kujiajiri kupitia mtaji wako kwa amana ya shamba la miti au michungwa, pia kununua ardhi ukiwa kijana itakufanya kuweka hazina ya muda mrefu na kukuepusha kuhangaika kupata ardhi kipindi kijacho kwani halmashauri nyingi zinakuwa kwa kasi na kufanya ardhi ipande bei kila kukicha.

Leo hii kuna watu wa umri wa kati na ulioenda katika wilaya ya Missenyi mkoani Kagera wamenunua ardhi maeneno ya jirani na kiwanda cha sukari kagera (kagera sugar) , kuanzia heka 5 mpaka 50 , na kuamua kujishughulisha na kilimo cha miwa , hakika kilimo cha miwa kimewalipa sana kwani kwa heka moja iliyopanda miwa na kutunzwa vizuri ina uhakika wa kutoa Tani 35 mpaka 40, na Tani 1 ya miwa huuzwa kwa Tsh 48,500/= hii ukichukua kwa Heka 15 , kwa kila heka ukitoa Tani 35 kwa heka 15 utapata Tani 525 za miwa, ambapo ukizidisha na na Tsh 48,500*525 utapata 25,462,500/= hiki ni kiasi cha pesa utakachokipata kwa muda wa Mwaka mmoja kwani toka kuandaa shamba mpaka kuvuna zao la miwa huchukua takribani mezi 9 mpaka 15 inategemeana na aina ya mbegu na joto, unaweza kulima heka uzitakazo kulingana na ulivyojiandaa kwa mazingira hayo, umasikini utabaki historia na huwezi kutegemea kuajiriwa.

Hayo yote hayafanywi na vijana wa sasa bali ni vijana wa zamani , hivyo vijana inabidi turudi vijijini japo tunapenda mijini na kununua ardhi kwa ajili ya kufanya maendeleo endelevu yatakayotufanya kujikwamua kiuchumi na sio kutegemea kuajiriwa kwa maisha ya mjini ambayo mshahara hautoshi hata kidogo.

Katika azimio la arusha Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere, alijaribu kuelezea ili nchi iendelee inahitaji vitu gani? ambavyo alivitaja na kuviorodhesha kwa upana wake vitu hivyo ni Ardhi, Watu, Siasa safi na Utawala bora, katika kipengele cha ardhi alijua kuwa ardhi ikiwa mikononi mwa wachache maendeleo yatakuwa kwa wachache lakini kwa Tanzania kila mtu anauwezo wa kununua ardhi kwa ajili ya Maendeleo , ardhi yetu nchi zinaitamani kwani bado ina rutuba na inapatikana , hivyo basi vijana tuitumie fursa hii ya kurudi vijijini kununua ardhi na kuiendeleza ili baadae itulipwe kwa manufaa makubwa kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaunga mkono juhudi za Mh Rais Dr Magufuli za kutaka vijana wajishughulishe na kilimo, japo mazingira ya kupata ardhi ni magumu hukiwa huna fedha na nyenzo za kilimo kuna njia nyingi za kupata ardhi kama ukipitia serikali za vijiji na kuishirikisha serikali, "kuamua kufanya na kushindwa ni vizuri zaidi kuliko kuacha kufanya".

Ardhi ndio msingi wa maendeleo bila ardhi hakuna maendeleo, ardhi ni hazina vijana tutumie fursa hii ya kuitumia ardhi yetu kuharakisha maendeleo ya haraka katika Taifa letu, tukifanya hivyo maisha yatabadilika na tutaondokana na umasikini wa kujitakia.

Mwisho, nawaasa vijana kwa kusema maendeleo katika taifa lolote lile huletwa na vijana shupavu na weledi wanaoamini kuwa msingi wa Taifa kufanikiwa ni juhudi za vijana kujituma na kutambua fursa zilizopo katika Taifa.

" ARDHI NI HAZINA"

Wasaalam.

Eng. Ayubu Massau(Che Guevara)
0763188907
 
Asante enginer umetwambia ukweli ambao ktk watz 1000 ni mmoja tu atakuelewa na kuchukua hatua kwa kisingizio cha mtaji! Its really a wonderful staff! I'm looking toward to back to rural for projects bro! Thanx!
 
Haya ndio maneno mazuri tuyatakayo engineer, wenye kuelewa tumekuelwa vizuri sana. Tuombe uzima tu.
 
Kuna ukwel apo hata kama uta pata chini ya hizo 25M bado huna hasara maana huna hasara kulingana na investment yake
 
Kila siku mi napiga kelele na Wakubwa zangu kuhusu hiyo issue wanaona kama nimerogwa na sijui chochote!
 
Ardhi ukinunua Leo kesho imepanda bei lakini ukitoa hela ukanunua pikpik ukiifikisha nyumbani bei inashuka hivyo tuwekeze kwenye ardhi...
 
Kwel ww eng hujui hata wekaa aya ili kunogesha bandiko
 
Ushauri mzuri mno ila watakaosoma ni wachache,watakaotekeleza ni wachache zaidi. Yapo maeneo nchini bado unapata ekari moja kwa Sh.100,000/=.

Wasomi tunatakiwa kuthibitisha kuwa elimu ina faida vinginevyo tukiri kuwa tuna makaratasi ya kuombea kazi hatuna elimu.

Mambo aliyoyashauri mtoa mada fuatilia Wilaya ya Mfindi uone vijana walioishia darasa la saba na kidato cha nne walivyowekeza kwenye miti wanapata Sh. ngapi ambazo baadhi ya tuliyoajiriwa hatutapata hata baada ya miaka 30 ya ajira zetu.
 
tatizo bongo ukinunua ardhi ikipanda thamani wananzengo hawakawii kugawana kwakisingizio cha shamba pori. naona halihii inaongezeka kwa kasi hata Leo ITV wameonyesha uko arumeru wananchi wanagawana shamba la mtu
 
Na mie najipanga kurudi home nikaendeleze mashamba yangu kwa kupanda miti ya pines... namwomba sana Mungu niutekeleze huu mradi make ardhi ndo maisha ya uhakika zaidi, heshima sana Engineer
 
Hivi Arusha mashamba yanapatikana wapi? Na bei zikoje?
 
Miye nahitaji heka tano mpaka kumi maeneo ya kanda ya ziwa tena ningependa eneo ambalo mpunga ustawi.
 
1465572303629.jpg
 
Nimekuelewa sana, sasa ni kuchukua hatua.
 
Back
Top Bottom