Well vijana wapo jukwaa la mapenzi kulilia kupendwa.
Unashauri tuijenge vipi Africa.
Kabla ya kuanza kujenga unatakiwa ujue nini chanzo cha kutokuendelea kwa ujenzi wa africa.
Unahauri tufocus kwenye nyanja ipi ili tukuze uchumi wetu?
At least there's someone who thinks like me.
Tuanze kwa kujaza vichwa vyetu positivity yaani tuache wivu na roho mbaya unajua kuna tabia fulani ya kutopenda maendeleo ya mwengine ambalo lipo kuanzia ngazi za familia mpaka maofisini hii inarudisha sana nyuma maendeleo ifike wakati ufungue moyo na kuamini kwamba maendeleo ya mwenzako ni maendeleo yako pia hata kama hatokupa kitu wewe...
KNOWLEDGE yaani knowledge is power sana wazungu wametuletea vitu vingi vinavyotupunguzia uwezo wa kufikiri hasa Tv programs, pia baadhi ya wasanii wanapewa agenda kama vile kukaa uchi kwenye video hii imewafanya wengi kuwaza sex badala ya vitu vya msingi na mfano mzuri ni dada zetu siku hizi hawataki kazi wanawaza kudanga kwasababu vitu wanavyovitaka wameviona kwenye TV na haviendani na uwezo wao in the end wanatumia sex ambayo kimsingi Mungu aliileta kwa ajili ya Reproduction tu na sio starehe the same kwa sisi wakaka tunawaza tukipata pesa ni kugongana tu. Ukitaka kuona utofauti we ingia vijijini jaribu kuwasoma maisha yao utagundua jinsi wanawake wanavyojituma na wakaka wanavyowahi kujitegemea...
UZALENDO hapa naomba vijana waachane na propaganda za kisiasa na kuitanguliza nchi mbele na ukitaka usiendeshwe na wanasiasa we kuwa tayari kujifunza na kufuatilia habari za ulimwengu mzima kisha tulia zichakate vizuri pia usipende kuchagua upande hii inakufanya ushindwe kufikiria vizuri na kufanya maamuzi sahii. Hakikisha unapitia taarifa nyingi iwezekanavyo kabla ya kuaminishwa kitu na mwanasiasa yoyote na pia ukiwa unaijua nchi yako vizuri yaani namaanisha unasoma bajeti, uongozi na historia za viongozi, elimu, ulinzi na usalama wa nchi. Hii tabia itakuweka mahali salama....
UCHUMI hapa namaanisha ili kukuza uchumi wa nchi ni lazima tujitolee kufanya kazi kwa jasho kila mtu kwa nafasi yake bila kujali nani anafanya nini. Kwanza tujivunie nchi yetu Vijana kuna mikopo inatolewa kwa vikundi vya vijana tena ni mamilioni ya mapesa mimi nina ushahidi watu wamechukua hundreds of Millions kuanzisha miradi na sasa hivi wanamaendeleo mazuri na wanapeleka marejesho LAKINI changamoto yetu kubwa vijana hatupendi kufuatilia vitu vya msingi tunauoga wa kuongea na viongozi lakini kwenye ujinga na ushabiki tupo faster sana so tuanze kufuatilia wapi pakutoa mitaji pili tujitahidi kushirikiana kwa kuzingatia vipengele nilivyotaja hapo juu...
Mambo yapo mengi lakini tuanze taratibu na tutafika.
Mkuu umesema 'UZALENDO hapa naomba vijana waachane na propaganda za kisiasa na kuitanguliza nchi mbele'.
Naona hapo chini afisa elimu akitanguliza maslahi ya taifa mbele.
View attachment 1548498
Mkuu umesema 'UZALENDO hapa naomba vijana waachane na propaganda za kisiasa na kuitanguliza nchi mbele'.
Naona hapo chini afisa elimu akitanguliza maslahi ya taifa mbele.
View attachment 1548498
Tuanze kwa kuondoa vibabu vihafidhina kama Magufuli na Kabudi madarakani, vikongwe hivi fikra zao ni za karne ya 20 ya kupambania ukombozi, havitufai na vinaturudisha nyuma.