Vijana tubadilike

Vijana tubadilike

Joined
Jul 15, 2013
Posts
15
Reaction score
6
Naweza kusema kuna suala kubwa vijana wamejisahau nayo ni kwamba, unamfanyia campaign mwanasiasa ili yeye apate kazi wakati mwenzangu na mimi kila siku tunalia hatuna kazi, hakuna mwanasiasa yeyote atakaye kulatea kazi na msaada wowote iwe, ccm,cdm,cuf na hata wengineo.
hivi tuseme ukweli hata washike chadema au hata chama chochote pinzani wataibadilisha ikulu kuwa rangi nyingine?au itabaki kuwa nyeupe?
voting.jpg ,
ni ukweli kwamba siasa imetuingia vijana sana na hata tukaisahau uzalendo wetu,jamani ni mwanasiasa gani tuliyewachagua ikatokea siku moja akatembea nyumba hadi nyumba kujua nini matatizo ya wananchi wake?kama wanavyofanya wakati wa kuomba kura?
jamani tumejionea wanasiasa wengi waliingia kwenye siasa akiwa kachoka kama mimi na wewe lakini baada ya kushika wadhifa hali yake imebadilika na sie tukiwa vile vile?

jamani vijana tunapotea huku tukishuhudia wenyewe,tunajionea wenyewe wanasiasa walewale lakini wanabadili uniform na majina ya vyama,
alafu akiwa hana hata aibu anakuja kukuahidi yale yale ya chama kile alicho hama,

kama alishindwa kutimiza akiwa chama alichotoka,atatimiza akiwa chama kipya?

Vijana tuamke siasa haina nafasi kwetu,kwanini kila siku tuwe chambo cha wanasiasa? wakati wao na family zao wakiwa salama? vijana wezangu, wanasiasa woooooote lao moja wanayoyafanya katika ukumbi wa mikutano zao ni entertainment kuonyesha wanafanya kazi hali ya kuwa likiongelewa suala la wao kupandishwa mishahara hakuna anayepiga kelele ya ukweli wengi wao ni kujionesha na mwisho wa siku wanajiongezea mishahara na marupurupu yao,

zingatia haya:
(a)kama mwanasiasa anapenda nchi yake na kuwajali wananchi wake,basi na wao wawalete watoto wao katika shule za serikali tulizosoma sisi na hata yeye......
(b)na wao pamoja na family zao watibiwe katika hospitali tunazo tibiwa mimi na wewe.
(c)na wao wanunue vyakula katika masoko tunayo ya nunua sisi (sio katika supermarket).

Angalizo: USHABIKI WA KISIASA NI HATARI KWA MAENDELEO YA TAIFA. KUWA MAZALENDO. KEMEA MAOVU. TANZANIA ISTAWI.
 
Hizo kazi za kufanya tutapata wapi kama hao hao wanasiasa wanawagawia wale waliowasaidia kupata madaraka tu? ref; malalamiko ya upendeleo wa ajira nono kwa watoto na ndugu wa vigogo, u-DC, RC, ukurugenzi n.k Tena, tukijaribu kuwa wamachinga wanatuletea migambo yajiji wanatupora bidhaa na mitaji. Kila mahali wanakabana, sasa tufanyeje zaidi ya kuwa wapiga debe wa hao wana siasa.
 
kwa hiyo na sisi wote tuwe washabiki ili nasi tupate hizo kazi?

nadhani hiyo sio sawa,
tusimame pamoja na kuteteana katika njia ya haki, hatuwezi kuajiriwa wote,muhimu kujituma na kujiajiri katika sehemu zilizowekwa na serikali,na kama hawajatenga, tudai haki tutengewe sehemu za biashara,
ukweli ni kwamba kila mtanzania anataka kuwa boss,afanye kazi ndogo alipwe hela mingi,kijana Amka na ujitambue,siasa haina nafasi ,tutaishia kupigwa mabomu kila siku,kufungwa na kupoteza muda wakati tungehangaikia uzalishaji na kuijenga nchi yetu..
nchi ikichafuka mwanasiasa anapokewa nchi zingine na kuitwa mwanasiasa na mimi na wewe tutabaki kuwa wakimbizi na kuishi katika kambi hali ya kuwa mwanasiasa anaishi nyumba ya maana....

Amka kijana jitambue
 
Napenda ujibu threads!
Sikuungi mkono kwa hoja zifuatazo
1. Sera nying za ajira hupitiswa na wanasiasa je tusipowachagua waaminifu mambo yatakuwaje
2. Unapodai upinzan hauwez na kuwa lao 1 je chama kipi unapendekeza
3. Si kwel kuwa wanasiasa lao ni 1,kwani serikal ya ccm imekuwa ikipewa ushauri na upinzan na kuudharau mfano a-kuwakamata mafisad badala yake wanawaomba kurudisha fedha
b-kubadil mfumo wa elim ili elimu imsaidie kijana kujitegemea lakn umeona nin wanakifanya
c-kutatua migogoro ya ardhi badala yake ccm wanawapa wawekezaji maeneo ya wazawa
d-kuwakopesha zana za kilimo wananchi,utazame mpango wa kilimo kwanza waliokopeshwa ni wakina nani
e-n.k

5-serikal imekuwa ikipinga sera,hoja na mapendekezo mengi ya upinzan kuhusu vijana na ajira
6-je tusipojihusisha na siasa nani atuamulie? Tusipige kura? Je tukipiga tutawatambua vp wenye nia njema bila ushiriki wetu?
7. Vipi tukiwapigia kampen au kuacha lipi litamfanya mwanasiasa awakumbuke wananchi?
8.tujitume kutafuta walio bora tusitumike...
 
Kila kitu kinaendeshwa na siasa, mfano ili uwe na kiwanda lazima ziwepo sera zinazotungwa na wanasiasa, ili tupate maeneo ya biashara,kilimo, ufugaji n.k ni lazima ziwepo sera zao, ili kupewa vibal vya uchimbaji madin, uvuvi ni lazima zitungwe sheria, pia kumbuka kodi pia ni lazima iwepo sheria, kwa hayo tu lazima uwepo ushirik wa raia wote kwenye siasa ili kupata viongoz watakaotutetea na si kutukandamiza,hivyo ushirik wa vijana utatoa hamasa kwa viongoz juu ya sera bora, juu ya kodi n.k chukulia mfano mdogo tu bunge limepitisha kuwa kila anayemilik cm alipie line tsh 1000 kila mwez, zito na makamba wameomba wananch wapinge je vijana tukatae ombi lao kisa tutakuwa tunawapa sifa? Tujiulize tunaoumia ni sisi,ni lazima tuwachague tuwapigie kampen wenye nia njema ya kututetea haijalish wanatoka chama gani.
 
Wewe sio kijana na ndio maana hujaeleweka vizuri! Ningekuona wa maana kama ungesema vijana tuwe imara katika kuhakihisha tunawapata viongozi imara. Wewe unatoa ushauri tusijihusishe na siasa?? Nani atapiga kura kama mimi na wewe Mzee kijana hatutahusika?
 
Napenda ujibu threads!
Sikuungi mkono kwa hoja zifuatazo
1. Sera nying za ajira hupitiswa na wanasiasa je tusipowachagua waaminifu mambo yatakuwaje
2. Unapodai upinzan hauwez na kuwa lao 1 je chama kipi unapendekeza
3. Si kwel kuwa wanasiasa lao ni 1,kwani serikal ya ccm imekuwa ikipewa ushauri na upinzan na kuudharau mfano a-kuwakamata mafisad badala yake wanawaomba kurudisha fedha
b-kubadil mfumo wa elim ili elimu imsaidie kijana kujitegemea lakn umeona nin wanakifanya
c-kutatua migogoro ya ardhi badala yake ccm wanawapa wawekezaji maeneo ya wazawa
d-kuwakopesha zana za kilimo wananchi,utazame mpango wa kilimo kwanza waliokopeshwa ni wakina nani
e-n.k

5-serikal imekuwa ikipinga sera,hoja na mapendekezo mengi ya upinzan kuhusu vijana na ajira
6-je tusipojihusisha na siasa nani atuamulie? Tusipige kura? Je tukipiga tutawatambua vp wenye nia njema bila ushiriki wetu?
7. Vipi tukiwapigia kampen au kuacha lipi litamfanya mwanasiasa awakumbuke wananchi?
8.tujitume kutafuta walio bora tusitumike...

nashukuru kwa haya majibu... so sina neno tena kwani umeandika points ambazo ningeandika... perfect....
 
Wewe uliyeleta huu uzi nashindwa kukuelewa! Unataka kama siyo vijana ni akina nani wasimamie mustakabali wa mambo ya taifa?? nadhani una lengo la makusudi kuleta huu uzi na pia naweza kusema kuwa hujitambui!!!
 
Naweza kusema kuna suala kubwa vijana wamejisahau nayo ni kwamba, unamfanyia campaign mwanasiasa ili yeye apate kazi wakati mwenzangu na mimi kila siku tunalia hatuna kazi, hakuna mwanasiasa yeyote atakaye kulatea kazi na msaada wowote iwe, ccm,cdm,cuf na hata wengineo.
hivi tuseme ukweli hata washike chadema au hata chama chochote pinzani wataibadilisha ikulu kuwa rangi nyingine?au itabaki kuwa nyeupe?
View attachment 102492,
ni ukweli kwamba siasa imetuingia vijana sana na hata tukaisahau uzalendo wetu,jamani ni mwanasiasa gani tuliyewachagua ikatokea siku moja akatembea nyumba hadi nyumba kujua nini matatizo ya wananchi wake?kama wanavyofanya wakati wa kuomba kura?
jamani tumejionea wanasiasa wengi waliingia kwenye siasa akiwa kachoka kama mimi na wewe lakini baada ya kushika wadhifa hali yake imebadilika na sie tukiwa vile vile?

jamani vijana tunapotea huku tukishuhudia wenyewe,tunajionea wenyewe wanasiasa walewale lakini wanabadili uniform na majina ya vyama,
alafu akiwa hana hata aibu anakuja kukuahidi yale yale ya chama kile alicho hama,

kama alishindwa kutimiza akiwa chama alichotoka,atatimiza akiwa chama kipya?

Vijana tuamke siasa haina nafasi kwetu,kwanini kila siku tuwe chambo cha wanasiasa? wakati wao na family zao wakiwa salama? vijana wezangu, wanasiasa woooooote lao moja wanayoyafanya katika ukumbi wa mikutano zao ni entertainment kuonyesha wanafanya kazi hali ya kuwa likiongelewa suala la wao kupandishwa mishahara hakuna anayepiga kelele ya ukweli wengi wao ni kujionesha na mwisho wa siku wanajiongezea mishahara na marupurupu yao,

zingatia haya:
(a)kama mwanasiasa anapenda nchi yake na kuwajali wananchi wake,basi na wao wawalete watoto wao katika shule za serikali tulizosoma sisi na hata yeye......
(b)na wao pamoja na family zao watibiwe katika hospitali tunazo tibiwa mimi na wewe.
(c)na wao wanunue vyakula katika masoko tunayo ya nunua sisi (sio katika supermarket).

Angalizo: USHABIKI WA KISIASA NI HATARI KWA MAENDELEO YA TAIFA. KUWA MAZALENDO. KEMEA MAOVU. TANZANIA ISTAWI.

Nimeipenda, big up sana kijana! Vijana weng wamekuwa mateja wa vyama siasa bila kujijua na ukiangalia weng wao ndio hao hao wasiokuwa na ajira, labda wanafikiri hivyo vyama ndo vitawaletea ajira!
 
Kuchagua na kuchaguliwa ni haki ya kikatiba ya mwananchi ,vijana wanapaswa kujihusisha na siasa,tena mwamko bado ni mdogo sana,hii ni hatua muhimu ya kuingia kwenye maamuzi ya taifa lao,taifa lisipojengwa na vijana litajengwa na nani?
 
Siasa ina athari za moja kwa moja kwenye uchumi.. Mikataba mibovu ni matokeo ya kutokuwa na viongozi makini. Tatizo la ukosefu wa ajira linachangiwa na sera za Serikali kuruhusu makampuni kuajiri wageni ilhali wapo wa-tz wenye vigezo. kwenye ujasiriamali zipo sera nyingi tu zinazowaumiza wajasiriamali wadogo......

Matatizo ya vijana wa Tanzania kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na mfumo wa Serikali. ukisema tusishiriki kubadilisha mfumo ili tunufaike sote nashindwa kukuelewa......

Vijana tushiriki kwenye chaguzi ili tubadilishe mfumo wa uongozi tuweze kupata wawakilishi wa Umma na siyo wawakilishi wa matumbo yao binafsi....

Tanzania ni moja na watanzania ni wamoja.
Mapendo
 
Kuchagua na kuchaguliwa ni haki ya kikatiba ya mwananchi ,vijana wanapaswa kujihusisha na siasa,tena mwamko bado ni mdogo sana,hii ni hatua muhimu ya kuingia kwenye maamuzi ya taifa lao,taifa lisipojengwa na vijana litajengwa na nani?

kweli kabisa,mwamko wa vijana kwenye siasa bado ni mdogo sana... nashangaa mtu anajaribu kutukatisha tamaa eti tuachane na siasa.
 
Kuchagua na kuchaguliwa ni haki ya kikatiba ya mwananchi ,vijana wanapaswa kujihusisha na siasa,tena mwamko bado ni mdogo sana,hii ni hatua muhimu ya kuingia kwenye maamuzi ya taifa lao,taifa lisipojengwa na vijana litajengwa na nani?

Acha kuudanganya umma ww! Mimi binafsi najutia kujihusisha kwenye siasa, huo muda nilioupoteza ni bora ningeutumia kulima pengine ningeneemeka sasa hv.
 
Huo ushauri ni mzuri sana kwa Mazuzu wa Bavicha.
Sijui kama wanajitambua.
 
Napenda kujibu threads kama ifuatavyo!

1. Sera nying za ajira hupitiswa na wanasiasa je tusipowachagua waaminifu mambo yatakuwaje
( ni yupi mwanasiasa aliye mwaminifu na mwadilifu? mwananchi mzalendo ni yule anayewajulia hali jamii inayomzunguka kila siku na kwa wale walio na shida anawasaidia hata kama sio kiongozi,mimi na wewe tunafanya hivyo?.
je? tunatumia vigezo gani kuwachagua viongozi?)

2. Unapodai upinzan hauwez na kuwa lao 1 je chama kipi unapendekeza
( hakuna chama ninachopendekeza kwani wote mwisho wa siku wanajipendelea wao na family zao mimi na wewe tunakumbukwa wakati wa kura,wenye shida siku zote ni mwananchi wa hali ya chini ambaye ni mimi na wewe)
3. Si kwel kuwa wanasiasa lao ni 1,kwani serikal ya ccm imekuwa ikipewa ushauri na upinzan na kuudharau mfano (je hao unaowaita wapinzani wanatokea wapi kama sio chama tawala?na je wao walikifanya kipi bila ya kushirikisha media ili na wao wapate jina? mwalimu yule yule darasa ndio tofauti)
a-kuwakamata mafisad badala yake wanawaomba kurudisha fedha (sote tunajua kuwa viongozi wamejilimbikizia mali za umma,wawe chama tawala na hata hao wapinzani,hakuna aliye dhahir kuanika mali zake)
b-kubadil mfumo wa elim ili elimu imsaidie kijana kujitegemea lakn umeona nin wanakifanya (anaye isema serikali mwenyewe anawasomesha wanae nje...wao wanafanya nini kubadili mfumo huo kama sio kuwaumiza kwa kuwaweka juani na kuwahimiza maandamano yasiyo na maana?huku wakianza kupigwa vijana wao wanakimbia,na wakipelekwa polisi,mwanasiasa anapelekwa chumba maalum,huku kijana asiye na hatia anapelekwa sero tena kwa kipigo,.kwanini isiwe viongozi ndio wanaokamatwa na kuwajibishwa?na lini ulishawahi sikia mwanasiasa kapigwa risasi na kuuawa?
c-kutatua migogoro ya ardhi badala yake ccm wanawapa wawekezaji maeneo ya wazawa (fuatilia record yao kama hutokuta na wao wana Ardhi kibao,kama hajaandika jina lake basi la mwanae au ndugu yake)
d-kuwakopesha zana za kilimo wananchi,utazame mpango wa kilimo kwanza waliokopeshwa ni wakina nani
e-n.k (ukichunguza kwa undani kabla ruzuku haijaja kwa wanachi wao wote huanza kuwezeshana,fuatilia wanasiasa wote hakuna maskini kama mimi na wewe mwenzangu)
sio lazima uwe mwanasiasa au kiongozi ndio uweze kutoa msaada,hata mimi na wewe tunaweza....tuamke na kufanyia kazi masuala yetu wenyewe na sio mpaka ushinikizwe na mwanasiasa....

5-serikal imekuwa ikipinga sera,hoja na mapendekezo mengi ya upinzan kuhusu vijana na ajira (serikali ni mimi na wewe ndugu yangu wala sio wanasiasa, lini uliamka kijana mwenzangu na kuamua kwenda kwa kiongozi wako kama Diwani na kumuuliza alichofanya bila ya kushinikizwa na yeyote?)
6-je tusipojihusisha na siasa nani atuamulie?(tujiamulie sisi wenyewe na sio wanasiasa,hivi mwanasiasa anajua shida zako kiasi gani?) Tusipige kura,?(tunapige kura ila sio kwa ahadi za mdomo maandishi yawepo)
Je tukipiga tutawatambua vp wenye nia njema bila ushiriki wetu,(kiongozi ni wa kutoka jamii yetu na sio mambo ya kuletewa na chama )
7. Vipi tukiwapigia kampen au kuacha lipi litamfanya mwanasiasa awakumbuke wananchi (kabla ya mwanasiasa kuwakumbuka wananchi,ni muhimu sisi wenyewe kukumbukana)
8.tujitume kutafuta walio bora tusitumike...
 
Naweza kusema kuna suala kubwa vijana wamejisahau nayo ni kwamba, unamfanyia campaign mwanasiasa ili yeye apate kazi wakati mwenzangu na mimi kila siku tunalia hatuna kazi, hakuna mwanasiasa yeyote atakaye kulatea kazi na msaada wowote iwe, ccm,cdm,cuf na hata wengineo.
hivi tuseme ukweli hata washike chadema au hata chama chochote pinzani wataibadilisha ikulu kuwa rangi nyingine?au itabaki kuwa nyeupe?
View attachment 102492,
ni ukweli kwamba siasa imetuingia vijana sana na hata tukaisahau uzalendo wetu,jamani ni mwanasiasa gani tuliyewachagua ikatokea siku moja akatembea nyumba hadi nyumba kujua nini matatizo ya wananchi wake?kama wanavyofanya wakati wa kuomba kura?
jamani tumejionea wanasiasa wengi waliingia kwenye siasa akiwa kachoka kama mimi na wewe lakini baada ya kushika wadhifa hali yake imebadilika na sie tukiwa vile vile?

jamani vijana tunapotea huku tukishuhudia wenyewe,tunajionea wenyewe wanasiasa walewale lakini wanabadili uniform na majina ya vyama,
alafu akiwa hana hata aibu anakuja kukuahidi yale yale ya chama kile alicho hama,

kama alishindwa kutimiza akiwa chama alichotoka,atatimiza akiwa chama kipya?

Vijana tuamke siasa haina nafasi kwetu,kwanini kila siku tuwe chambo cha wanasiasa? wakati wao na family zao wakiwa salama? vijana wezangu, wanasiasa woooooote lao moja wanayoyafanya katika ukumbi wa mikutano zao ni entertainment kuonyesha wanafanya kazi hali ya kuwa likiongelewa suala la wao kupandishwa mishahara hakuna anayepiga kelele ya ukweli wengi wao ni kujionesha na mwisho wa siku wanajiongezea mishahara na marupurupu yao,

zingatia haya:
(a)kama mwanasiasa anapenda nchi yake na kuwajali wananchi wake,basi na wao wawalete watoto wao katika shule za serikali tulizosoma sisi na hata yeye......
(b)na wao pamoja na family zao watibiwe katika hospitali tunazo tibiwa mimi na wewe.
(c)na wao wanunue vyakula katika masoko tunayo ya nunua sisi (sio katika supermarket).

Angalizo: USHABIKI WA KISIASA NI HATARI KWA MAENDELEO YA TAIFA. KUWA MAZALENDO. KEMEA MAOVU. TANZANIA ISTAWI.

Eti na huyu ni great thinker (grit sinker).

Think twice before you start a thread.

So unatushauri tufanye nini, tushiriki vita na si siasa ....
 
kama sera zote za nchi zinatungwa na wanasiasa basi mimi na wewe hatuna haki na nchi,kwanini hatujahushishwa katika sera hizo?
 
siasa ndio chanzo cha vita,kwani inamtengeneza mwananchi kujitenga kutokana na itikadi za chama,kila mmoja anavutia upande wake hali ya kuwa sisi wote wamoja.
kwanini wanasiasa wasitutumikie sisi,na sio sisi kuwatumikia wao?
ni mawazo tu ni kiwa kama kijana mwenzio.
 
eti na huyu ni great thinker (grit sinker).

Think twice before you start a thread.

So unatushauri tufanye nini, tushiriki vita na si siasa ....

nenda ukalime ndugu!
 
Back
Top Bottom