Vijana tubadilike

Vijana tubadilike

Wewe uliyeleta huu uzi nashindwa kukuelewa! Unataka kama siyo vijana ni akina nani wasimamie mustakabali wa mambo ya taifa?? nadhani una lengo la makusudi kuleta huu uzi na pia naweza kusema kuwa hujitambui!!!

ninajitambua vizuri ndio maana nikakwambia vijana tusimame wenyewe na sio mpaka tushinikizwe na vyama vya siasa,

serikali ni yetu sote,na wala sio ya ccm wala chadema.
 
Napenda ujibu threads!
Sikuungi mkono kwa hoja zifuatazo
1. Sera nying za ajira hupitiswa na wanasiasa je tusipowachagua waaminifu mambo yatakuwaje
2. Unapodai upinzan hauwez na kuwa lao 1 je chama kipi unapendekeza
3. Si kwel kuwa wanasiasa lao ni 1,kwani serikal ya ccm imekuwa ikipewa ushauri na upinzan na kuudharau mfano a-kuwakamata mafisad badala yake wanawaomba kurudisha fedha
b-kubadil mfumo wa elim ili elimu imsaidie kijana kujitegemea lakn umeona nin wanakifanya
c-kutatua migogoro ya ardhi badala yake ccm wanawapa wawekezaji maeneo ya wazawa
d-kuwakopesha zana za kilimo wananchi,utazame mpango wa kilimo kwanza waliokopeshwa ni wakina nani
e-n.k

5-serikal imekuwa ikipinga sera,hoja na mapendekezo mengi ya upinzan kuhusu vijana na ajira
6-je tusipojihusisha na siasa nani atuamulie? Tusipige kura? Je tukipiga tutawatambua vp wenye nia njema bila ushiriki wetu?
7. Vipi tukiwapigia kampen au kuacha lipi litamfanya mwanasiasa awakumbuke wananchi?
8.tujitume kutafuta walio bora tusitumike...

Mkuu maelezo kibao unajichosha tu. Ukweli hakuna mwanasiasa anayetizama kukusaidia mara ngapi wabunge wanalilia kura but hakuna kitu. Jimboni kwangu tushabadilisha wabunge kibao wa vyama tofauti lakin hamna jipya. Ukitaka maendeleo jitoe mwenyewe sio kumtazama mwanasiasa
 
Wewe sio kijana na ndio maana hujaeleweka vizuri! Ningekuona wa maana kama ungesema vijana tuwe imara katika kuhakihisha tunawapata viongozi imara. Wewe unatoa ushauri tusijihusishe na siasa?? Nani atapiga kura kama mimi na wewe Mzee kijana hatutahusika?

Tanzania hata tungeloga hakuna kiongozi imara.
 
Huo ushauri ni mzuri sana kwa Mazuzu wa Bavicha.
Sijui kama wanajitambua.

Kama kuna watu wasio na akili na wewe ni moja wapo! Thread hii inatoka pale Lumumba mambo ya sizitaki mbichi hizi baada ya kuona vijana hawana muda na ccm kwa sasa! Wewe na mwenzako mnataka tuache kufatilia siasa tumwachie nani? MaCcm? Hamnazo nyie! Kwanza baada ya kuwahamasisha vijana sasa tunahamia kwa mama zetu tutawanunulia kanga na vitambaa vya chadema maana mmewafanya mazuzu miaka 50 ya uhuru! Mimi wazazi wangu nimewapiga stop kushabikia ccm kule kijini na kama watakiuka basi na mimi sipeleki msaada maana mimi naumia kutafuta chakula nakatwa kodi kubwa lakini hamna huduma yoyote wanayopewa wazazi wangu huko kijijini! Nimewambia 2014/2015 ni chadema na kama hawaitaki basi wasiende kupiga kura kabisa lasivyo tutaonana wabaya ebo!


Tuitoe kwanza CCM ndiyo vijana tuache siasa baada ya nchi kuwa kwenye mikono salama! Hata chadema wakiharimu tunawatoa tu maana ni lazima tuwe na uongozi unaowaheshimu wananchi kwanza! Katiba mpya itakuwa hamna cha kusubiri mpaka miaka mitano ni immediate ukichemka unawekwa pembeni! Vijana ndiyo nguvu ya taifa lolote wasiposhiriki kwenye siasa nani sasa atafanya maana maana maendeleo ya nchi za kidemokrasia yanaletwa na siasa! Kasome vitabu vya mwlimu kuhusu ili tuendelee tunahitaji nini utakuta ni siasa safi na uongozi bora. Tatitzo la tanzania tumekosa hivi vitu kwa sababu ya ccm uongozi zero siasa chafu kila siku sasa utaendelea wapi! Nilazima ccm ipishe wajaribu na wengine na vijana ndiyo tutakao ifulumusha ccm kwa taarifa yako! Nyie endeleeni kuchukua buku saba pale lumumba sisi tunasongambele hatuachi siasa mpaka ccm kwanza itupishe wajaribu wengine ebo!
 
Back
Top Bottom