Vijana Rorya wamelala

Vijana Rorya wamelala

KODHLUOCH

Member
Joined
Mar 31, 2014
Posts
17
Reaction score
0
Nashangaa vijana wengi wamekuwa kimya na kutoongelea maswala makuu yanayoisibu Rorya,wamebaki kuwa watazamaji tu.

Amkeni sasa kodhluoch yuko nanyi 2015,kwa maswala yote ya kiuchumi.
 
Nashangaa vijana wengi wamekuwa kimya na kutoongelea maswala makuu yanayoisibu Rorya,wamebaki kuwa watazamaji tu.

Amkeni sasa kodhluoch yuko nanyi 2015,kwa maswala yote ya kiuchumi.
Mkuu 2015 nasimama ili kufanya yale yanatakiwa na wananchi kweli ukiangalia tuko nyuma sana kimaendeleo .bado kule anakotoka mbunge airo watu bado wanakunywa maji ya mto Maori.barabara -ndo usiseme niunge mkono tujenge rorya
 
:loco:Kuongozwa na chama cha mizigo tu kunaonesha ni namna gani watu wasivyojitambua, acheni Airo aendelee kuwapa misaada:tape:
 
Rorya kweli ni tabu tupu maana maendeleo hamna. Mfano barabara itokayo Mika kwenda Shirati imewekwa lami kidogo tu haifiki hata utegi. Hiyo barabara ni mbovu sana ina mawemawe na mashimo mengi sana. Mabadiliko yanahitajika sana Rorya maana maendeleo hamna.
 
Walioleta shida kwa kurudisha maendeleo nyuma ni OYOMBE AYILA na PHILEMON SARONGI kama Oyombe yeye alikuwa analala bungeni. Kwa hiyo chanzo ni kutoka awali.
 
mkuu 2015 nasimama ili kufanya yale yanatakiwa na wananchi kweli ukiangalia tuko nyuma sana kimaendeleo .bado kule anakotoka mbunge airo watu bado wanakunywa maji ya mto maori.barabara -ndo usiseme niunge mkono tujenge rorya

bwana sos peter jaluo,kusimama si tatizo la rorya wengi wanasimama je unanini cha kusimamia rorya. Pili ningeshauri uache hiyo jina la jaluo,rorya is multi lingual constituency hatutahitaji majina yanayoonyesha direct tribal,hiyo jina unaweza kulitumia vizuri sana kwenye matambiko yako kuomba mizimu ya kwenu, siyo kwenye jukwa la siasa kuongea maswala ya taifa.

Kodhluoch.
 
Rorya kweli ni tabu tupu maana maendeleo hamna. Mfano barabara itokayo Mika kwenda Shirati imewekwa lami kidogo tu haifiki hata utegi. Hiyo barabara ni mbovu sana ina mawemawe na mashimo mengi sana. Mabadiliko yanahitajika sana Rorya maana maendeleo hamna.

MWAKANI KWENYE KURA ZA MAONI TUNAHITAJI USHINDI WA HOJA NA VISION YA WAGOMBEA ATAKAYETUELEZA KUWA ATAFANYA NINI NA AWE MTU SAFI NA UPEO MPANA WA KULETA MAENDELEO.
PILI NINGEWAASI WANARORYA HASA VIJANA KUACHA KULALA WAAMKE WACHUE OPPORTUNITIES AMBAZO SERIKALI INATOA KUPITIA TAASISI ZAKE.TUACHE KULALAMIKA UTAFIKIRI WOTE NI WALEMAVU. MIKONO TUNAYO,AKILI TUNAYO,MIGUU TUNAYO,MACHO,MASIKIO,NA VIUNGO VINGINE SAWA, HIVYO NGUVU TUNAYO TUANZISHE CHOCHOTE NA TUTAPATA ATAKYE TUENDELEZA-

KODHLUOCH YUPO. JUST CONTACT ME. kodhluoch.rorya@gmail.com
 
mkuu 2015 nasimama ili kufanya yale yanatakiwa na wananchi kweli ukiangalia tuko nyuma sana kimaendeleo .bado kule anakotoka mbunge airo watu bado wanakunywa maji ya mto maori.barabara -ndo usiseme niunge mkono tujenge rorya

wuo jaduong nitakuunga mkono tu pale utakaponiconvince na hoja sina ushabiki, mimi ni mwana siasa na mwanarorya mwenye uchungu sana na sitahitaji na sitakuwa tiyari kushabikia tu mwenye haja ya kuwa mbuge rorya bila kunipa hoja la kunigusa ama kuwagusa wanarorya kwa ujumla.

Kodhluoch.
 
MIMI NDIYE KODHLUOCH LAZIMA NIWAAMSHE NA WAJUE KWANZA HAKI ZAO NA NAFASI ZAO KAMA VIJANA WA RORYA NA KITU GANI KINAHITAJIKA TOKA KWAO KAMA VIJANA WA RORYA NA TANZANIA, UMUHIMU WAO KWENYE JAMII NA SABABU ZA MSINGI ZINAZOHITAJI VIJANA WAAMKE KULIKO WAZEE.

KWANZA KUWA KIJANA RORYA NI HAKI YAKO YA KIMSINGI HIVYO HIYO HAKI KAMA VIJANA HAWATAITUMIA KUBADILISHA MAISHA YAO BASI NAOMBA WAAMKE NA WAMUULIZE KODHLUOCH TUFANYE NINI TUTUMIE HAKI ZETU ZA KIMSINGI KUBADILISHA MAISHA YETU NA MAISHA YA WALE WALIOKO KARIBU NASI. KODHLUOCH NIPO KWA USHAURI.
KAMA UMEJARIBU CHOCHOTE UMESHINDWA NIANDIKIE,KAMA UFANYA CHOCHOTE NA KIMEPIGWA CHINI SEMA NAMI,KAMA UNAWAZO LA KULITEKELEZA ONGEA NAMI.

EMAIL; kodhluoch.rorya@gmail.com
KODHLUOCH
 
bwana sos peter jaluo,kusimama si tatizo la rorya wengi wanasimama je unanini cha kusimamia rorya. Pili ningeshauri uache hiyo jina la jaluo,rorya is multi lingual constituency hatutahitaji majina yanayoonyesha direct tribal,hiyo jina unaweza kulitumia vizuri sana kwenye matambiko yako kuomba mizimu ya kwenu, siyo kwenye jukwa la siasa kuongea maswala ya taifa.

Kodhluoch.

Mbona na wewe unajiita KODHLUOCH? Nawe jina lako ni la kijaluo kwani yeye PETER. kafanya kosa. gani?
 
Nashangaa vijana wengi wamekuwa kimya na kutoongelea maswala makuu yanayoisibu Rorya,wamebaki kuwa watazamaji tu.

Amkeni sasa kodhluoch yuko nanyi 2015,kwa maswala yote ya kiuchumi.

Mkuu una ushawishi wa kizamani sana,kwa mtu kama mimi hujanishawishi chochote.kwa upeo wangu mdogo wewe nia yako ni uungwe mkono ugombee ubunge ki ushabiki tu wakama simba na yanga.Ni vyema ungesema mapungufu na hayo mapungufu una mikakati gani ya kuiziba na kwa njia gani?
 
Tuungane tulete maendeleo[/QUOT

KWELI KABISA TUUNGANE TULETE MAENDELEO,MUUNGANO UTAANZA KWA VIONGOZI WAUNGANISHI SIYO WATENGANISHI,NI AIBU KUWA KIONGOZI ALIYEUNGANISHA AFRICA ALITOKA MKOANI MARA LAKINI SISI TUNASHINDWA KUUNGANA KAWILAYA TU.

NYERERE ANAHESHIMIKA KWA KUUNGANISHA DUNIA NA AFRICA LAKINI HAPA RORYA TUNAJULIKANA KAMA WANAMUSOMA TUKIWA DA ES SALAAM NA MAENEO MENGINE YA TANZANIA, MUSOMA NDIYO KWAO NYERERE-KWELI NI AIBU HATUNA UMOJA NA KUENDELEA KUTUPIANA MANENO YA UKABILA,USHENZI USHENZI TU,NASEMA WENYE UKABILA WAUTUMIE KWENYE MATAMBIKO YAO SIYO RORYA. TUWE WAMOJA TUINUKE PAMOJA,TUACHE CHUKI ZA KIMASKINI MASKINI KAMA HIVYO.

KODHLUOCH.
 
mbona na wewe unajiita kodhluoch? Nawe jina lako ni la kijaluo kwani yeye peter. Kafanya kosa. Gani?

kosa la peter ni kujiita jaluo. Kodhluoch ni sifa. Jaluo ni kabila,jakine,jasurwa,jaacha. Janam ni sifa, ja mach ni sifa. Etc

kodhluoch
 
Rorya is marwa kwa thuon and oyieyo will pass through yiendambewa. So ni sisi hawahawa wa kukaa chini nakutafakari kwa kina kuhusu rorya bila hivyo tutakuwa watu wa kulalamika kila kukicha. Tuungane tuwe kitu kimoja ili tulete maendeleo Rorya bila kuwa na ubaguzi. Wa kikabila.
 
:loco:kuongozwa na chama cha mizigo tu kunaonesha ni namna gani watu wasivyojitambua, acheni airo aendelee kuwapa misaada:tape:

cmm ndiyo chama cha msingi yenye sera za kutekelezeka kinachohitajika ni uongozi bora na yenye kuleta changamoto za maendeleo.
 
mkuu una ushawishi wa kizamani sana,kwa mtu kama mimi hujanishawishi chochote.kwa upeo wangu mdogo wewe nia yako ni uungwe mkono ugombee ubunge ki ushabiki tu wakama simba na yanga.ni vyema ungesema mapungufu na hayo mapungufu una mikakati gani ya kuiziba na kwa njia gani?

mkurugenzi mimi sijakushawishi nimekwambia kuwa kuna umuhimu vijana kuamka na kutokuwa dormant kwenye maswala ya rorya,mapungufu yetu ni mengi ambayo si rahisi kuyaweka pamoja kwenye kipande hichi ila kwa kifupi najua unaelewa vijana wetu wanhitaji elimu,kazi,biashara na ushiriki mpana na wenye dira kwenye maswala mengi ya kiuchumi,jambo ambalo halipo kwa sasa kwa sababu hatujampata kiongozi aliyefikia vijana na kugusa mahitaji yao yote kwa kuyafanya. Ninamengi ya kuwapa vijana rorya,na siyo ushabiki ama kutaka kuungwa mkono. Matatizo ya vijana rorya ni makubwa kuliko kuungwa mkono tu na kushabikiwa kama yanga na simba.

Hatutahitaji ushabiki juu ya matatizo ya watu wetu.

Haya nipe mikakati yako ya kuhakikisha ujumbe wako unamfikia kila kijana wa Rorya,kagwa,kowak,waturi,Kakresu.Vijana wengi wa rorya wana uelewa mdogo,wana ushabiki wa kikanda nani wanachama wa vyama tofauti na wanapenda rushwa ndogondogo kama kununuliwa kichwa cha chengu kwa kura.
 
Back
Top Bottom