Uvutaji wa sigara na ulevi kiujumla haswa kwa vijana wenzetu ni suala la fikra tu.
Kivipi.
1. Mkumbo... vijana wengi wanavuta na kulewa kwa kufata mkumbo hata ukiwauliza kampani zao wengi wanavuta na kulewa.
2.hali ngum ya maisha inapelekea vijana kuona pombe na sigara kama kiburudisho cha kuwapunguzia mawazo.
3. Urahisi wa upatikanaji wa hivyo vilevi na gharama zake kuwa chini kama ulivyosema hapo juu.
Nini kifanyike .
1. serikali inapaswa kudhibiti utengenezaji holela wa vileo hivyo.
2.wazazi kubeba wajibu wa kuhakikisha kampani za watoto wao zinakuwa zenye manufaa kwa umri wao kwasababu haya mambo yanaanza chini kabisa
3. Viongozi wa dini kiujumla wanawajibu kwa nafasi zao kukemea mambo ya ulevi kwa kasi sana na sio kulea mambo yanayofanana na hayo