Vijana na siasa ya Tanzania

Vijana na siasa ya Tanzania

anazungumza mwenyekiliti wa cdm segerea kijana mdogo, anadai kuwa ktk siasa za tanzania, hakuna chama cha siasa kinaweza kumwamini kijana mdogo kama yeye kuwa mwenyekiti wa wilaya kama yeye. hivyo cdm ni ni ya vijana
 
vijana wanahaitaji siasa za digital, siyo za kianalogia na za kizee. vijana hawatakikuendelea kutumika kwa ajili ya walio madarakani
 
Kuna jamaa mmoja siku nasa jina lake kaniboa sana anasema nchi hii hakuna Raisi ka JK eti kafichua mafisadi na wezi wa mali ya umma, nafikiri wakati anaongea alikuwa na brain concusion maana anatakiwa ajiulize tangu JK ameanza vita hivyo hatua gani imekwisha chukuliwa?
 
Ukiwa CCM NAONA HATA UWEZO WA KUFIKIRI HUWA UNAPUNGUA SANA,JAMAA STUDIO YA DAR AMBAE NI KADA WA CHAMA TAWALA NAONA UWEZO WAKE WA KUFIKIRI NI MDOGO SANA,YEYE INAONEKANA NI MZURI BUT KUJIPENDEKEZA KWA WATAWALA NDO TATIZO LINALOMKUMBA SANA.ANYWAY KILA MTU ANA UHURU WA KUONGEA
 
Wapendwa,

Jana nimefuatilia kipindi cha "MALUMBANO YA HOJA-ITV" picha ilinionesha kuna changamoto kubwa sana kwa Vijana wa nchi yetu hii na wanapaswa kufanya mageuzi makubwa kabisa ya kifikra katika nafsi zao. Hususan wasiwe AKILI TEGEMEZI na kikubwa zaidi nilichokiona vijana wengi walioshiriki kipindi hicho ni kukosa weledi wa mambo, kushindwa kugusa hisia za wanaowaona na kuwasikiliza na hata kushindwa kujieleza wao kuwa ni nani na wanataka nini (HILI LILIBAKI KWA WANAHARAKATI!!!) HAPA NINA MAANISHA VIJANA WENGI HAWAJITAMBUI, HAWATAMBUI WAJIBU WAO KWAO WAO WENYEWE WALA KWA TAIFA LAO!! Na hawa ndio wengi wao tunawatarajia kuwa viongozi wajao wa taifa hili. Hata waliokuwa wakijaribu kunukuu bado walishindwa kufikia lengo kusudiwa, Je ni nini kinawasibu hata wakashindwa namna ile? Je walitishwa ama waliogopa mic? Je pale palikuwa na umati wa kumfanya mtu atetemeke na kushindwa kupangilia dhumuni na hoja za kuonesha mapungufu?
Hili la kipindi hicho limenionesha kwamba kuna safari ndefu kwa Watanzania kufika tunakokwenda, kwani wanasiasa wajanja wataendelea kupandilia migomgo hiyo na kunufaika, huku vijana wakibaki kulalama na kulaani bahati kutokuwa upande wao.

VIJANA WASIPOBADILIKA na ikiwa hivi ndivyo tutakavyoendelea kuwa.. kwa maana tutaendelea kutegemea akili za waliomo ndani na tukiona akili hizo hazijaeleweka tutategemea akili toka ughaibuni! Na huu ndio utakuwa mwisho mbaya kuliko ule wa mwanzo!
Laiti tungelikuwa tunazitumia akili zetu vilivyo Tanzania HAINA TATIZO LA AJIRA.

Lakini kinyume chake, UVIVU wetu wa kufikiri umetupelekea kuwa WAVIVU wa kufanya kazi achilia mbali kutafuta kazi kwenyewe! na ni huohuo uvivu uliotupelekea kufika hapa tulipo hii leo.
Waliotambua mapungufu ya Watanzania walipata kuleta maneno "Nguvu kazi" Usipowajibika ole wako" "Bwana mkubwa akichelewa msimfungulie ofisi" je leo hali ikoje? Je wakati ule kulitokea badiliko kubwa? Jiulizeni ikiwa leo mtu anaetoka ofisini saa tisa ana magazeti ya kila siku yasiopungua kumi mezani pake na yote anayasoma saa za kazi je huyu mtu anawajibika?

Je ni vikongwe pekee wanaobana nafasi za vijana? Kwani je hao vikongwe wataishi milele? lakini je mbadala wake ni kubaki kulalamika na kupaaza sauti tu? naamini hakuna tatizo lisilokuwa na ufumbuzi. Kinyume na hivyo
TUMEKWISHAAA!
Maskini Tanzania!
 
Com' again mkuu...

Una hoja ila unalalamika, na kushindwa kusema unachotaka!!

In a nutshell heri yule aliyempongeza Kikwete, sio??

Baseline, tunahitaji baraza la vijana la Taifa ambalo Serikali ya CCM inakwepa kila siku, lawama zingine hazina msingi, kama wao walilalamika na wewe unaendelea kulalama hapa!!
 
Back
Top Bottom