Vijana na siasa ya Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijana na siasa ya Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by REBEL, Dec 5, 2011.

 1. REBEL

  REBEL Senior Member

  #1
  Dec 5, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nimekuwa nikitafakari hali ya siasa na mchango wa vijana katika maendeleo ya Jamii.

  Mungu amenijalia kutembelea maeneo mengi ya nchi yetu kama mji magharibi, Unguja kusini, Mwanza, Arusha, Bukoba, Iringa,dodoma n.k .Na wimbo ni ule ule kuwa vijana hawadhaminiwi kabisa.

  Suala moja la kwanza ninalotaka kulizungumzia ni wamachinga. Kitendo cha maaskari wa mji/ jiji kuwar vijana kwa kuwaibia na kuwabughudhi wamachinga kunawarudisha nyuma kimaendeleo vijana. Kwa mfano mwezi uliopita hapa mji magharibi, Zanzibar serikali imeamua mji uwe msafi. Na wao walichoamua ni kuwa wafanyabiashara ndio wanaochafua mji na wakaanza kuwakamata na kuwaghasi.
  swali :Je hii ni haki?

  Na hili si tatizo la hapa zanzibar tu bali ni chanzo cha migogoro kote bara kuanzia Mbeya, Mwanza, Arusha na miji yote mikubwa.Ni imani yangu kuwa sheria inabidi zitungwe ili kuleta maendeleo kwa watu wake na kutambua sekta zisizo rasmi na sio kunyanyasa vijana.

  Kitu cha pili, ni wimbi la vijana wasio na kazi walio wasomi na wasio wasomi linazidi kuongezeka. Hili ni bomu ambalo serikali inalikuza kama Lowassa alivyosema. Tatizo wizara ya kazi na yule waziri mwizi wa kura Prof. Makongoro Mahanga wa jimbo la segerea hajui kuimudu wizara yake yuko tu kuuza sura.Simpendi huyu wazirikabisa kazi kukaa tu ofisini.

  Sema katika haya yote kuna vitu vinavyonipa matumaini kwa kuona vijana wanamudu siasa vyema sana sana wa NCCR- Mageuzi na ChaDEMA. Vijana hao ni Mkosamali, Kafulila, Machali, Mnyika, Lema, Silinde. Wengine ni Wenje, Halima Mdee, Regia Mtema na Sugu. Sema wakaze buti na Mungu atawasaidia. Vijana waliotuangusha ni yule katibu mwenezi wa CCM Nape Nnauye na yule zero Lusinde hata na Makamba January, na kingwangala hawako kwa ajili ya vijana na wanaboa.

  Vijana tutetee haki zetu na katiba mpya.sio tu kila siku tunaimba mapenzi tu.

  Nawasilisha.
   
 2. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kweli kabisa mkuu,
  inatakiwa kuwa taifa lisilokuwa na watu waoga!ukisahaelewa mpigania haki yoyote lazima akumbane na misukosuko basa woga unakaa pembeni kisha tunasonga mbele,hata kama chadema au NCCR wakiwa madalakani wakaleta ushenzi nao tunawang'oa tu
   
 3. M

  Mkwanda Senior Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau mjadala upo hewani sasa unaendele wale wenye acces na itv mnaweza mkaufatilia moja kwa moja.
   
 4. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  tupe updates mkuu.
   
 5. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Wanachotaka vijana ni mabadiliko ya uongozi wa serikali maana waliopo ni upuuzi mtupu! Tunataka tukibadilishe chama kinachoongoza serikali tusikilizie tena!
   
 6. T

  TAREQ AZIZ Member

  #6
  May 3, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Vjana ni taifa la leo.ila aina ya vjana kama january makamba ni janga la kitaifa
   
 7. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Wakuu hii thread ili isipoteze mvuto wekeni updates sio wote wanaoangalia TV sasa.
   
 8. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Updates plz sio mnapiga porojo hapa kama rejao, leteni updates
   
 9. A

  ACHIMIDES Member

  #9
  May 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  lazima mabadiliko--hata kiranja wa darasa hubadilika kila mwaka----acha na watu wengine wakakusanye madaftari kwani nao wanazijua ofisi za walimu zilipo.
   
 10. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Pamoja na Nape wote wana akili za kizeee. Vijana kama hao ni sawa na Masaburi
   
 11. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,796
  Likes Received: 1,338
  Trophy Points: 280
  Kuna dogo limedai huu mpango wa kila kitu kufanyia maamuzi Dar wakati akili za watu zishachoka hakuna lolote,
  Ushauri-yeye haamini kama Mungu alilazimisha Mara,Kigoma au Shinyanga ziwe Tanganyika. Anasema ni bora ziwe nchi halafu kuwe na shirikisho la Tanganyika.
  Anaunga mkono CDM
   
 12. M

  Mkwanda Senior Member

  #12
  May 3, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  memberz wengi kwenye huu mjadala wanahitaji vijana kushika hatamu ya uongozi kwani hata ukombozi kwenye nchi mbalimbali uliletwa na vijana.
   
 13. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #13
  May 3, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,796
  Likes Received: 1,338
  Trophy Points: 280
  Kuna motheri mmoja anadai nchi imeongeza vichaaa wengi kuliko zamani. Yeye toka aanze kupata akili ni majina yale yale ya viongozi waliokuwa madarakanimiaka ya sitini hadi leo ni watoto kama si wao.
  Vijana amueni, ingieni ktk siasa
   
 14. M

  Mkwanda Senior Member

  #14
  May 3, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu mdada hapa kwenye meza kuu kafunguka vizuri kwa kusema vijana waache kutumika kama makarai na waamini kua hata wao wanaouwezo wakusimama kwa miguu yao na kufanya maamuzi sahihi.
   
 15. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #15
  May 3, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,796
  Likes Received: 1,338
  Trophy Points: 280
  Mother anaendelea-vijana ni wa muhimu kwa sababu kila siku wanawaza mawazo mapya, ya nini kubaki na mizee inayosinzia ovyo halafu ikiamka inapiga mabenchi kuunga hoja bila kujua nini kiliongelewa?
   
 16. M

  Mkwanda Senior Member

  #16
  May 3, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mama anaendele kwa kusema kua hata jk nae atafute muda wakuongea na vijana sio kilasiku anaita wazee tu wanakuja kusinzia.
   
 17. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,796
  Likes Received: 1,338
  Trophy Points: 280
  nchi hii bila vijana kuacha kutumika ovyo na CCM hatutoki@wazo langu
   
 18. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #18
  May 3, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  :smile-big: Wakina Rejao, Mwita, FF, Tume ya Katiba na wengine utawamalizia wewe
   
 19. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #19
  May 3, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,796
  Likes Received: 1,338
  Trophy Points: 280
  Deodatus-UDSM
  tunahitaji mabadiliko lakini naomba madiliko haya ni lazima yawe na sura ya kuwakumbuka walemavu.
  pia naomba mafisadi washughulikiwe, juzi juzi nimesikia redioni kuna waziri kanunua nyumba kwa mil zaidi ya 600 pesa ambayo inaweza kujenga shule kigogo mwizi bado analelewa.
  Mabadiliko si lazima yaje kwa njia ya amani ni vizuri kutumia njia ya mapinduzi.
  nchi zetu za afrika wazee wameng'ang'ania madaraka wamataka wafie pale. (hayo ni maoni ya kijana wa UDSM -ni mlemavu wa macho)
   
 20. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Sasa huyo mlemavu wa Macho kafunguka, hao wenye macho wakina Rejao bado hawajafunguka na wanona kila utumbo tunaofanyiwa na Mafisadi
   
Loading...