Vijana na Ndoto za Siasa Tanzania!

Gagurito

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
5,600
804
Vijana wengi hawajitambui, wanawaza siasa kwa mtazamo wa kuneemeka na maposho posho, wachache sana wanawaza siasa njia sahihi ya kuikomboa tanzania toka matatiszo yanayotukabili. we have to shape our minds, let us think the future of this country under national development perspective NOT on individual bases. VIJANA WA TANZANIA TUBADILIKE!
 
Umegusa jambo la maana sana, na huo ndio ukweli uliotawala kwenye mawazo ya vijana wengi. Mawazo ya watu wengi kuwa siasa ni sehemu ya kuchuma utajiri, ndio maana watu wapo tayari kufanya lolote hata yale yasiyofikirika ili wapate kuwa karibu na viongozi waliopo madarakani kwa kuwa hao viongozi ndicho wanachofanya wanagawa uongozi kwa watu wao wa karibu bila kujali uwezo wao. Wengine kwa kukosa hizo fursa wanakimbilia upinzani si kwa kuwa wanadhani huo mfumo wa kuendesha nchi ni mbovu, bali kwa kuwa hawakupata nafasi, wanataka nao wawe kwenye 'circle' ile ile upinzani ukitwaa nchi. Ndio maana wanapojiona hawafaidiki, wanakuwa tayari kwenda majukwaani kusema mambo ambayo hata mtu mwenye mtindio wa ubongo anajua kuwa hayana maana. Tatizo hili ni kubwa hasa kwa vijana wanaomaliza chuo, wanawaza mambo makubwa mno (nyumba nzuri, gari nzuri, starehe), bila kujua kuwa hivyo vyote haviwezi kupatikana kwa kulala na kuamka asubuhi. Tuna kazi kubwa mno ya kuelimisha jamii yetu. Tubadili fikra za jamii zetu katika kujiletea maendeleo, na sio kutegemea kusaidiwa na watu kuendelea.
 
Asante kwa mchango wenye kujenga. Nimejifunza toka kwako baadhi ya mambo kama ulivyoandika. Tuchape kazi, Mapinduzi ya kiuchumi ni mazuri zaidi ya Mapinduzi ya kisiasa tena kama watu hawajitambui.
 
Nikweli kabisa., siasa yenye kutafuta mabadiliko ya kweli inapingwa na wengi., na si rahisi ina machungu mengi siwote tunaoiwazia siasa tunafahamu gharama ya kulipa iwapo mtu anatafuta kuleta mabadiliko ya kweli katika taifa kupitia siasa.
 
tubadilike
 
Aisee ubarikiwe sana kwa fikra pevu, nadhani jamvi lipata watoa hoja mahususi kama wewe vijana wengi tutapanuka kifikra na kihisia zaidi, ule mtazamo ukimaliza chuo utapata gari,nyumba nzuri bila kujua hatima yako na ya baadae ni fikra mgando za baadhi ya vijana,endelea kupasha kwa staili hii tutafika tu japo kazi ni kubwa sana!!
 
Back
Top Bottom