Operesheni Kimbunga yasababisha serikali za Tanzania na Uganda, kushitakiwa mahakamani

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,308
24,200
10 October 2023
Kampala, Uganda

OPERESHENI KIMBUNGA YA TANZANIA YAFIKISHWA MAHAKAMA YA AFRIKA MASHARIKI

Operesheni Kimbunga yasababisha serikali za Tanzania na Uganda, kushitakiwa mahakamani. Mwesigwa Rukutana & Co. Advocates pamoja na OSH Advocates mawakili wa walalamikaji 1240, wamethibitisha kesi imefunguliwa katika mahakama ya Africa ya Mashariki EACJ.

Kiini cha kesi hiyo mawakili wanasema kuwa wateja wao walifukuzwa Tanzania kufuatia maazimio ya wiki mbili yaliyotolewa na Rais wa wakati huo Jakaya Kikwete Julai 29, 2013. Kikwete aliwataja kuwa ni wahamiaji wasio na vibali na kuwataka warejee katika nchi walizotoka akieleza kuwa hawakuwajali. Kanuni za kuingia na uraia wa Tanzania.

Chini ya mpango huo unaojulikana kama ‘Operesheni Kimbunga,’ mamlaka za Tanzania, ikiwa ni pamoja na polisi, idara ya uhamiaji, kitengo cha usalama wa taifa , na vijana wa eneo hilo, waliwakamata na kuwasafirisha watu wapatao 50,000 hadi kwenye vituo vya kupita karibu na mpaka wa Uganda.
Serikali zote mbili za Tanzania na Uganda awali hazikukubaliana juu ya jinsi na wapi pa kuwapa makazi mapya waliofukuzwa. Uganda ilitoa wito rasmi kwa Umoja wa Mataifa kushughulikia suala hilo.

Bw . Yoofesi Jafferson Karugaba, anaeleza kuwa waliishi katika wilaya mbalimbali za Mkoa wa Kagera kwa miaka mingi lakini walifukuzwa Tanzania kwa utaratibu kufuatia agizo la Rais. Sasa wanajikuta katika hali ya kuchanganyikiwa, kwani hakuna nchi inayowatambua kama raia.

Kwa mujibu wa ombi hilo, watu hao waliofukuzwa walikuwa ama raia wa Tanzania kwa kuzaliwa, ukoo au uraia. Baadhi walikuwa wameishi Tanzania kwa takriban miaka arobaini, huku wengine wakiwa wameoana na Watanzania na walikuwa wamedumishwa na rasilimali za Watanzania.

10 October 2023
Kampala, Uganda

Expelled Group Files Lawsuit Against Ugandan and Tanzanian Governments​

View: https://m.youtube.com/watch?v=8GCcoeXjJBE

A group comprising more than 1200 individuals who were forcibly expelled from Tanzania has taken legal action by filing a lawsuit against the Tanzanian government in the East African Court of Justice. Their grievance pertains to the unjust manner in which they were expelled from the country, as well as the destruction of their property during the process.

Simultaneously, in the same legal petition, the group has also brought a suit against the Ugandan government for its alleged failure to protect them and for not compelling the Tanzanian authorities to provide compensation.

The expulsion of these individuals occurred in 2013, during the presidency of Jakaya Kikwete. It was initiated through a presidential order known as “Operation Kimbunga,” which led to the expulsion of an estimated 50,000 people residing along the Tanzania-Uganda border, predominantly in the River Kagera basin.

The justification for this expulsion was that they were perceived as refugees from Uganda, Rwanda, Burundi, or the Democratic Republic of Congo.
The operation was carried out by the Tanzanian Joint Task Force, which included the Police Force, the Department of Immigration, the Intelligence Unit, and the Tanzania People’s Defense Forces. Many of those expelled had lived in Tanzania for decades, and their forced displacement had significant consequences on their lives and livelihoods.

The group’s legal representatives, Mwesigwa Rukutana & Co. Advocates and OSH Advocates, held a press conference to explain their clients’ plight. They asserted that for over a decade, both the Tanzanian and Ugandan governments had neglected to address their concerns, compelling them to seek justice through the court system.

Advocate Rukutana emphasized the severity of the situation, stating, “These are tens of thousands of people that were arbitrarily expelled from their lands, homes, businesses, and farms, and whose property and source of livelihood have been either seized, destroyed or converted by officials and members of the armed forces of the Tanzanian government. Despite their cries to both governments, these people have neither been resettled nor defended by the Ugandan government where the majority of them now live in destitution.”

Among those who were expelled, there were individuals who were citizens of Tanzania by descent or naturalization, as well as immigrants who had resided in Tanzania for approximately 40 years. Some were intermarried with Tanzanian citizens and had deep ties to the country. Additionally, cattle keepers from Uganda who relied on the region for water and pastures were among those affected.

Advocate Rukutana explained that prior to the expulsion, the Tanzanian government had conducted a survey that claimed a substantial portion of land that had previously been under Ugandan jurisdiction. This land was inhabited by thousands of people engaged in farming and livestock keeping. The expulsion was marked by cruel and illegal actions, including looting and property confiscation by the Tanzanian army. Homes were burnt or sold, and individuals suffered unlawful arrests, assaults, detentions without trial, torture, murder, rape, and other forms of inhumane treatment.

Yofesi Karugaba, one of the victims, described their plight, stating that they have since lived as destitutes in concentration camps in various locations. The group has been scattered across different countries in the East African region, enduring challenging living conditions and distress.

Despite numerous efforts to engage with various stakeholders, including the governments of Tanzania and Uganda and the United Nations, the group has seen no progress in resolving their situation. The Tanzanian government has refused to allow the expelled individuals to return to their land or provide compensation for their losses.

In the petition, the Ugandan government is also accused of failing to protect the rights of the expelled individuals, most of whom are Ugandan citizens. Additionally, it is alleged that the Ugandan government has not taken sufficient steps to hold Tanzania accountable for the atrocities committed during the expulsion or to resettle the expelled individuals in a dignified manner.

In their legal action, the group accuses both governments of neglecting to establish a joint verification committee aimed at addressing their predicament.
 
TOKA MAKTABA:​

Ripoti ya Gazeti Habari Leo:​

OPERESHENI KIMBUNGA YAFUMUA KIJIJI HARAMU CHENYE DOLA YAO...​

September 29, 2013

Imeandikwa tarehe 29 Septemba 2013 By Eric Anthony, Kigoma

KAMPENI ya kitaifa ya kuondoa wahamiaji haramu nchini iliyopewa jina la Operesheni Kimbunga, imefanikiwa kusambaratisha kijiji cha wahamiaji haramu wa Burundi waliokuwa wamejitengenezea dola yao nchini, kiasi cha hata kutumia sarafu ya Burundi ilihali wakiwa Tanzania.

Aidha, watoto wao wanasoma shule kwa mitaala ya Burundi, ikiwa ni pamoja na kuwafundisha kwa lugha ya Kifaransa wakiwa kijijini Nyamugali, Mvugwe wilayani Kasulu, Kigoma.

Hayo yamethibitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa, Issa Machibya katika mahojiano maalumu na gazeti hili ofisini kwake mjini hapa.

Kutokana na hatua hiyo, baadhi ya wakazi wa mkoani Kigoma, wakiwemo wa Manispaa ya Kigoma Ujiji na wilaya za Kasulu na Buhigwe, wamepongeza hatua hiyo.

Wameitaka serikali kutorudi nyuma katika kuhakikisha inawaondoa nchini wahamiaji haramu ambao wametajwa kuwa tishio kwa usalama wa nchi kutokana na kujihusisha na matukio ya ujangili, biashara ya silaha zikiwemo za kivita, na matukio mengine.

View: https://m.youtube.com/watch?v=EEql2Cm6gXg

Akizungumza mjini hapa, Machibya alisema mbali ya kutumia faranga (fedha za Burundi) kwa matumizi yao ya kawaida wakiwa nchini na kufundisha kwa mitaala ya nchi waliyotoka, wahamiaji hao walipeperusha pia bendera ya nchi yao katika sehemu mbalimbali za kijiji hicho.
“Lakini kwa sasa, wote wamekimbia na kuziacha nyumba zao. Huwezi kuamini kama ni nyumba za wahamiaji haramu, kwani walijijenga na kuishi watakavyo, tena bila ya hofu katika nchi ya kigeni.

“Hebu tafakari, ni dharau gani unaishi Tanzania, lakini hata pesa yao hutumii, badala yake unatumia faranga.Tunashukuru tumewasambaratisha, na tutaendelea na operesheni hii mpaka tuhakikishe Watanzania
wanaishi kwa amani katika ardhi yao,” alisema Machibya.

Inakadiriwa kuwa, idadi ya wahamiaji haramu waliokuwa wanaishi kijijini hapo, lakini sasa wakiwa wamekimbia mkono mrefu wa Operesheni Kimbunga, ni zaidi ya 600.

Mkoa wa Kigoma pekee umenasa wahamiaji haramu 4,365 wa Burundi katika awamu ya kwanza ya operesheni hiyo iliyosambaa katika mikoa mbalimbali nchini, lakini Machibya amewataka Wana-Kigoma kushiriki kikamilifu
katika vita dhidi ya wahamiaji haramu hasa katika awamu hii ya pili na nyinginezo.

“Tatizo lililopo ni usiri. Wengi wameshindwa kutoa ushirikiano, na kufanya wengi tuishi nao kana kwamba ni Watanzania wenzetu… Watanzania waelewe hawa si watu wema, wangekuwa wema wangefuata taratibu za kuishi nchini, lakini wamekuwa wakiishi kwa ujanja ujanja mno. Mshona nguo za RC “Miongoni mwao ndimo walimo mawakala wa silaha za kivita, mabomu ya kurusha kwa mkono na biashara nyingine haramu.

Hatuwezi kukubaliana na hali hii,” alisema Machibya na kutoa mfano unaoendelea kumshangaza hata yeye mwenyewe kuwa, fundi maarufu aliyekuwa anashona nguo za baadhi ya Wakuu wa Mkoa wa Kigoma, akiwemo yeye mwenyewe na mtangulizi wake, RC kanali mstaafu John Simbakalia ni mtuhumiwa wa uhamiaji haramu.

“Ndiyo, hata kabla yangu ndiye aliyekuwa anashona nguo za baadhi ya ma-RC (Wakuu wa Mkoa) hapa Kigoma, Simbakalia ni miongoni mwao na mimi mwenyewe amenishonea suti mbili…nikanogewa na kutaka kushona suti nyingine, sasa nikiwa na kitambaa changu, kila nikipita nakuta ofisi zimefungwa, zaidi ya mara nne nimepita... kuuliza naambiwa ni wale wale, wameamua kujisalimisha kabla ya kunaswa.

“Sasa mambo haya yanatokea hapa mjini, si huyo tu, kuna wengi wanaendelea kusombwa…lakini kama Serikali ya mkoa, tunasema wawe hapa mjini au mahali popote pale, operesheni hii itawanasa na tunamshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuunga mkono,” alisema.

Akizungumzia hatua hiyo, Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, wilayani Kasulu, Frederick Nisajile, alipongeza kazi nzuri inayofanywa na serikali, huku akishauri mianya mingine ya kuzalisha wahamiaji haramu au hata kugawa uraia kiholela kwa wakimbizi ifungwe kwa sababu za kiusalama.

“Kwa idadi hii ya wahamiaji na wakimbizi, usalama wa nchi uko hatarini. Kuna mengi ya kufanyiwa kazi ili kuhakikisha nchi haiingiliwi,” alisema Nisajile ambaye amefanya kazi na wakimbizi kwa takribani miongo miwili.
Mkazi mwingine wa mjini Kigoma, eneo la Burega ambaye hata hivyo hakuwa tayari kutajwa jina, alisema,” Kigoma imevamiwa.

Mbaya zaidi watu wanafichiana siri, lakini wahamiaji ni wengi, wakiwemo wafanyabiashara wakubwa. Nao wanaita ndugu zao na kuzidi kuijaza nchi yetu, wakiishi bila kufuata taratibu.

Naipongeza serikali kwa kuanza kukabiliana na wimbi hili la wahamiaji haramu.” Naye Kiongozi wa Timu ya Habari na Mawasiliano ya Operesheni Kimbunga, Zamaradi Kawawa, akizungumza kwa njia ya simu kutoka Biharamulo, Kagera alisema anafarijika kuona operesheni inang’ata kila sehemu, huku akiahidi kutoa taarifa ya utekelezaji wa awamu ya pili ya operesheni inayoendelea kote nchini.

Operesheni Kimbunga ilianzishwa kwa lengo la kukabiliana na vitendo vya uhalifu vilivyokithiri vikiwemo ujambazi wa kutumia silaha, ujangili, utekaji wa magari na mauaji ya kikatili pamoja na migogoro ya ardhi inayotokana na wafugaji kutoka nchi jirani kuingiza mifugo yao kwa ajili ya malisho.

Ni utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya Kikwete alilolitoa Julai 29, 2013 akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Kagera, akitaka kufanyika kwa operesheni maalumu ya kuondoa uhalifu katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita ambao kwa kiasi kikubwa umechangiwa na kuwepo kwa wahamiaji haramu kutoka nchi jirani.

View: https://m.youtube.com/watch?v=hIvVrMdYY6Q

Operesheni Kimbunga inayoongozwa na Brigedia Jenerali Mathew Sukambi ilianza Septemba 6, 2013, baada ya kupita wiki mbili alizokuwa amezitoa Rais Kikwete kwa kuwataka wahamiaji wanaoishi nchini bila kufuata sheria kuondoka kwa hiari yao au kuhalalisha ukazi wao nchini.

Source: HabariLeo
 
MAENEO YA ILIYOKUWA BUGANDA KINGDOM MPAKA LEO INALETA MIZOZO AFRIKA, MIAKA 138 BAADA YA MKUTANO WA BERLIN MWAKA 1884

View: https://m.youtube.com/watch?v=75O6Pr9pCuE
Maamuzi yaliyofanyika miaka 138, wakati nchi za ulaya zilipokutana katika mkutano wa Berlin Conference 1884 kugawana mapande ya bara la Afrika kuunda nchi mpya bila kujali uwepo wa tawala kama za Buganda ambazo zilikuwa na mipaka yake wenyeji waliitambua Kagera Kiziba Kizinja Bukoba Tanganyika kuwepo ndani ya Buganda
1697016613624.png

The exact cause of former President Idi Amin’s annexation of the Kagera salient — a 1,800 square kilometre strip of land bestriding the Kagera River, in the corridor between Rwanda and Lake Victoria in Tanzania has for long spells remained a subject of debate. While the incident 42 years ago, was pivotal in Amin’s downfall in April 1979, following the Tanzanian People’s Defence Force's resolute counterattack, it also renewed another problem — a long-standing, low-level, boundary dispute between Uganda and her southern neighbour in which hundreds of thousands of people are caught up. In Panorama tonight, we look at this problem that was created 138 years ago, when European powers convened for the famous Berlin Conference.
 
01 December 2023

Hofu yatanda tena katika jamii, sababu ni waraka. Waomba serikali ikanushe

View: https://m.youtube.com/watch?v=tar6iImrwac

Tundu Lissu afunguka mazito kuhusu waraka unaosambaa mitandaoni wenye maagizo mazito kutoka wenye mamlaka na unaotembea mitandaoni kwa kasi kuhusu operesheni itakayopelekea majeshi ya ulinzi na usalama kukabiliana na raia kwa kuwelekeza bunduki, drones n.k

Huko nyuma operesheni kama Operesheni Kimbunga, Operesheni Tokomeza n.k hizo zote zilifanyika na kusababisha raia kuwa kunyang'anywa uraia wao/ kuporwa utaifa wao / kuwa state less, mali kutaifishwa n.k

Waitaka serikali itoe ufafanuzi ili kuondoa hofu kuwa ipo operesheni inakuja ...
 
Wanataka tu kuzulumu Mifugo ya Watu CCM Nchi imeshawashinda hii.
 
10 October 2023
Kampala, Uganda

OPERESHENI KIMBUNGA YA TANZANIA YAFIKISHWA MAHAKAMA YA AFRIKA MASHARIKI

Operesheni Kimbunga yasababisha serikali za Tanzania na Uganda, kushitakiwa mahakamani. Mwesigwa Rukutana & Co. Advocates pamoja na OSH Advocates mawakili wa walalamikaji 1240, wamethibitisha kesi imefunguliwa katika mahakama ya Africa ya Mashariki EACJ.

Kiini cha kesi hiyo mawakili wanasema kuwa wateja wao walifukuzwa Tanzania kufuatia maazimio ya wiki mbili yaliyotolewa na Rais wa wakati huo Jakaya Kikwete Julai 29, 2013. Kikwete aliwataja kuwa ni wahamiaji wasio na vibali na kuwataka warejee katika nchi walizotoka akieleza kuwa hawakuwajali. Kanuni za kuingia na uraia wa Tanzania.

Chini ya mpango huo unaojulikana kama ‘Operesheni Kimbunga,’ mamlaka za Tanzania, ikiwa ni pamoja na polisi, idara ya uhamiaji, kitengo cha usalama wa taifa , na vijana wa eneo hilo, waliwakamata na kuwasafirisha watu wapatao 50,000 hadi kwenye vituo vya kupita karibu na mpaka wa Uganda.
Serikali zote mbili za Tanzania na Uganda awali hazikukubaliana juu ya jinsi na wapi pa kuwapa makazi mapya waliofukuzwa. Uganda ilitoa wito rasmi kwa Umoja wa Mataifa kushughulikia suala hilo.

Bw . Yoofesi Jafferson Karugaba, anaeleza kuwa waliishi katika wilaya mbalimbali za Mkoa wa Kagera kwa miaka mingi lakini walifukuzwa Tanzania kwa utaratibu kufuatia agizo la Rais. Sasa wanajikuta katika hali ya kuchanganyikiwa, kwani hakuna nchi inayowatambua kama raia.

Kwa mujibu wa ombi hilo, watu hao waliofukuzwa walikuwa ama raia wa Tanzania kwa kuzaliwa, ukoo au uraia. Baadhi walikuwa wameishi Tanzania kwa takriban miaka arobaini, huku wengine wakiwa wameoana na Watanzania na walikuwa wamedumishwa na rasilimali za Watanzania.

10 October 2023
Kampala, Uganda

Expelled Group Files Lawsuit Against Ugandan and Tanzanian Governments​

View: https://m.youtube.com/watch?v=8GCcoeXjJBE

A group comprising more than 1200 individuals who were forcibly expelled from Tanzania has taken legal action by filing a lawsuit against the Tanzanian government in the East African Court of Justice. Their grievance pertains to the unjust manner in which they were expelled from the country, as well as the destruction of their property during the process.

Simultaneously, in the same legal petition, the group has also brought a suit against the Ugandan government for its alleged failure to protect them and for not compelling the Tanzanian authorities to provide compensation.

The expulsion of these individuals occurred in 2013, during the presidency of Jakaya Kikwete. It was initiated through a presidential order known as “Operation Kimbunga,” which led to the expulsion of an estimated 50,000 people residing along the Tanzania-Uganda border, predominantly in the River Kagera basin.

The justification for this expulsion was that they were perceived as refugees from Uganda, Rwanda, Burundi, or the Democratic Republic of Congo.
The operation was carried out by the Tanzanian Joint Task Force, which included the Police Force, the Department of Immigration, the Intelligence Unit, and the Tanzania People’s Defense Forces. Many of those expelled had lived in Tanzania for decades, and their forced displacement had significant consequences on their lives and livelihoods.

The group’s legal representatives, Mwesigwa Rukutana & Co. Advocates and OSH Advocates, held a press conference to explain their clients’ plight. They asserted that for over a decade, both the Tanzanian and Ugandan governments had neglected to address their concerns, compelling them to seek justice through the court system.

Advocate Rukutana emphasized the severity of the situation, stating, “These are tens of thousands of people that were arbitrarily expelled from their lands, homes, businesses, and farms, and whose property and source of livelihood have been either seized, destroyed or converted by officials and members of the armed forces of the Tanzanian government. Despite their cries to both governments, these people have neither been resettled nor defended by the Ugandan government where the majority of them now live in destitution.”

Among those who were expelled, there were individuals who were citizens of Tanzania by descent or naturalization, as well as immigrants who had resided in Tanzania for approximately 40 years. Some were intermarried with Tanzanian citizens and had deep ties to the country. Additionally, cattle keepers from Uganda who relied on the region for water and pastures were among those affected.

Advocate Rukutana explained that prior to the expulsion, the Tanzanian government had conducted a survey that claimed a substantial portion of land that had previously been under Ugandan jurisdiction. This land was inhabited by thousands of people engaged in farming and livestock keeping. The expulsion was marked by cruel and illegal actions, including looting and property confiscation by the Tanzanian army. Homes were burnt or sold, and individuals suffered unlawful arrests, assaults, detentions without trial, torture, murder, rape, and other forms of inhumane treatment.

Yofesi Karugaba, one of the victims, described their plight, stating that they have since lived as destitutes in concentration camps in various locations. The group has been scattered across different countries in the East African region, enduring challenging living conditions and distress.

Despite numerous efforts to engage with various stakeholders, including the governments of Tanzania and Uganda and the United Nations, the group has seen no progress in resolving their situation. The Tanzanian government has refused to allow the expelled individuals to return to their land or provide compensation for their losses.

In the petition, the Ugandan government is also accused of failing to protect the rights of the expelled individuals, most of whom are Ugandan citizens. Additionally, it is alleged that the Ugandan government has not taken sufficient steps to hold Tanzania accountable for the atrocities committed during the expulsion or to resettle the expelled individuals in a dignified manner.

In their legal action, the group accuses both governments of neglecting to establish a joint verification committee aimed at addressing their predicament.

hao waliofukuzwa walikuwa watanzania au wanyarwanda? kama walikuwa watanzania ilikuwaje wakawa na nchi ya kukimbilia kama kwao walipofukuzwa? waliishi nchini kihalali? tungeomba tuwajue ili tuwakamate tuwashtaki kwa kuishi nchini bila kibali. tuanzie hapo.
 
Ni sawasawa kuwafukuza Maasai na kusema asili yao ni Kenya?
 
dvocate Rukutana emphasized the severity of the situation, stating, “These are tens of thousands of people that were arbitrarily expelled from their lands, homes, businesses, and farms, and whose property and source of livelihood have been either seized, destroyed or converted by officials and members of the armed forces of the Tanzanian government. Despite their cries to both governments, these people have neither been resettled nor defended by the Ugandan government where the majority of them now live in destitution.”

anasema watu waliofukuzwa walikuwa wahamiaji walioishi miaka mingi Tanzania,walimiliki ardhi, majumba, biashara, mashamba na mifugo n.k. swali najiuliza, mhamiaji haramu au niseme mtu asiye mtanzania, anaweza kumiliki ardhi Tanzania? mtu ambaye sio raia anaweza kufanya biashara bila vibali vinavyomwonyesha yeye sio raia, mtu asiye raia anaweza kumiliki nyumba Tanzania. angewahusisha mawakili wa kitanzania wamsaidie sheria za Tanzania basi. halafu niseme ukweli, operation kimbunga wa kulaumiwa ni Kagame, ndio alianzisha ugomvi kwa kumtishia kikwete, na ninaamini ni operation iliyotuheshimisha sana.
 
Ni sawasawa kuwafukuza Maasai na kusema asili yao ni Kenya?
kama wakijulikana ni wakenya,wanatakiwa kufukuzwa au la waishi kwa permit hapa bongo. ndivo sheria inavyotaka. hata hao masai hawafukuzwi kwasababu hawajajulikana tu, wakijulikana kuwa masai huyu au yule si raia maafisa uhamiaji wanamdaka fasta. kama unamjua masai yeyote mkenya weka jina hapa tuwatonye uhamiaji wamrukie fasta. kwa wale wanyarwanda, walikuwa wengi sana, mang'ombe mengi kweli kanda ile na ilionekana kama rwanda ardhi ni ndogo hivyo wanakuja kuswaga ng'ombe wao huku. zamani tuliwachukulia kama ndugu na tuliowaonea huruma kwasababu ya vita zao na ukimbizi wao, ila walipoleta jeuri tukaamua kuwatimua. tulikuwa sahihi. ukija kwa fujo utaondoka kwa fujo, ukija kwa amani utaondoka kwa amani.
 
17 November 2023
Kakonko, Kigoma
Tanzania

Zitto Kabwe - Uhamiaji Acheni Ushamba, Mnasumbua Raia Wa Mipakani

View: https://m.youtube.com/watch?v=y029v2CB8iI

Hii ni baada ya raia mmoja mtanzania kupoteza maisha alipokuwa mikononi mwa idara ya uhamiaji na jeshi la polisi kufuatia tuhuma za kuwa siyo raia wa Tanzania

Kiongozi huyo wa ACT Wazalendo akemea tabia ya kuwaona watu wa Kigoma siyo raia wa Tanzania. Aongeza kuna wakati walimtetea na kumkingia kifua makamu wa rais Mh. Dr. Philip Mpango aliposakamwa na baadhi ya watu wenye nongwa kuwa makamu wa rais siyo raia wa Tanzania bali ni mBurundi ...

Back
Top Bottom