Vijana: Mtego unaoiangusha CCM, CHADEMA watautegua

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,636
Wakati wa uchaguzi wa mwaka 2005, Jakaya kikwete alikuja na hatimaye kushinda kwa gear ya
kuwakwamua vijana kutoka kwenye mkwamo wa kiuchumi unaowakabili, akaenda mbele akadai
atatengeneza ajira milioni moja ndani ya miaka mitano.

wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, vijana walimgeuka Jakaya, wakamgeukia DR na chama
chake. sababu ni kwamba, achilia mbali mazingaombwe ya ufisadi, Jakaya akuweza kukidhi mahitaji
ya vijana, kuna watu wanadai hata ajira 1000 hazikutengezwa kwa ubunifu wake. mpaka wakati
kampeni zinaanza Jakaya alikuwa amepoteza kabisa kabisa uwezo wa kuwakabili na kuzungumza na
vijana wa kitanzania.

Takwimu zinaonyesha kwamba takiribani asilimia 45% ya watanzania ni vijana, kipande kingine kikubwa
ni watoto (vijana wa 2020). wakati Jakaya anatoa ahadi za peponi kwa vijana hawa mwaka 2005.
zaidi ya asilimia 80% ya vijana hawa hawakuwa na elimu ya zaidi ya form four(18M), nilikuwa najiuliza,
Jakaya anampango wa kuwapa ajira gani vijana wasio jua kusoma wala kuandika? ama mateja?
vijana waliozoea kukaa vijiweni? sikupata jibu. na ukweli ukajidhihirisha. He failed, na wao 2010 wakamfail.

Nikianzia Igunga, hata uchaguzi wa 2010 pia, ushahidi wa wazi kabisa unaonyesha vijana wamegeukia
CHADEMA, tena nadhani, kwa hasira za kudanganywa na ccm, wamegeuka kwa hasira nyingi sana,
wamechoka na hawako tayari kudanganywa tena. wao wanasema "WE NEED CHANGES". Its true,
vijana wamemwaga mboga na hawana mzaa, wanaiburuza ccm na kwa dhamira hii 2015 CCM will be no more.

Hofu yangu ni kwamba, CHADEMA wanawaandalia vijana hawa deal au wanawatumia tu? au na wao
wanafurahishwa na jinsi vijana hawa walivyoibadilikia ccm? Hawa wanataka unafuu wa maisha katika bei ya
bidhaa mbali mbali, wanataka kujenga makazi bora, wanataka elimu bora na inayopatikana kwa wote, ajira,
wanataka kuwa huru kuendesha mambo yao mbali kabisa na bureacratic system ya ccm na propaganda
za kiusalama, wanataka kuheshimiwa, wanataka mambo mengi kwa kweli ambayo hayapatikani
katika zama hizi.

Hofu nyingine ni kwamba hata CHADEMA ikishindwa kukidhi ama kujionyesha kwamba inayafanyia kazi
mambo haya inaweza kukataliwa kwa style mbaya zaidi ya babu ccm
 

peri

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
2,581
1,162
Ili cdm iweze kufanikiwa inatakiwa kujipanga zaidi ya ilivyo sasa.
Isidanganyike na umaarufu wa ghafla ilioupata la sivyo itakufa vibaya kuliko ccm.
 

Jembe Ulaya

JF-Expert Member
Oct 27, 2008
456
103
Majibu yapo. Hili swala limezungumziwa kwenye ilani ya Chadema na vilvile kwenye hotuba ya bajeti ya upinzani (Chadema).
 

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,636
tunaomba utugusie kidogo. actions with impact on youth directly.
sababu mimi hili la vijana naliona kama political bubble, na nikiangalia yaliyotokea
igunga naona kama linaglow kwa kasi sana.

natanguliza shukrani zangu.
 

Kamakabuzi

JF-Expert Member
Dec 3, 2007
2,604
1,064
Majibu yapo. Hili swala limezungumziwa kwenye ilani ya Chadema na vilvile kwenye hotuba ya bajeti ya upinzani (Chadema).
100% sahihi.
Kama ulifuatilia pia hotuba za Dr Slaa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu utakuwa ulisikia mikakati ya kupunguza matatizo uliyotaja
 

Godlisten Masawe

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
738
281
Nadhani CDM wana dhamira ya dhati ya kutukomboa vijana na wanafahamu kwamba kwa sasa hivi sisi ndio mtaji wao.
 

Chakunyuma

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
810
151
Tukune vichwa kuweza kushauri mikakati ya kuongeza ajira, mi ninayo ifuatayo kwanza kuwe na mradi wa nchi nzima wa kuunganisha vijiji kwa kiwango cha changarawe hii iwe standard kweli kweli yaani hadi mifereji ya kupitisha maji ya kudumu na makandarasi wawekewe sheria ya kuwaajiri locals kwa mambo yanasiyo hitaji shule hii itatoa ajira kwa vijana wa vijiji husika, pili kujenga nyuma za walimu/manesi kila kijiji. Tatu kupeleka umeme vijiji hii itatoa fursa zinazopatikana mijini zipatikane vijijini, nne kuimarisha soko la mazao kwa kuweka sera zitakazowezesha uanzishwaji viwanda vya kusindika.
 

mpiganiahaki

Senior Member
Apr 28, 2011
170
67
chadema wanatakiwa wajikite zaid kwenye kuongeza vyuo bora na kisasa vya ufundi ili kuwapa ujuz vijana pia serikali ya chadema lazima isimame kidete kuhakikisha kuwa inaweka na kusimamia umri kikomo wa kustaafu kwa mashirika ya serikal
Pia waweke sheria kali itakayo walazisha makampuni yote ya uwekezaji kuwapa ujuzi wazawa
 

Shine

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
11,483
1,358
Ktk hili la kufa kwa ccm nina imani na uhakika pindi watakapoondolewa madarakani watahitalafiana wenyewe na chama kufa. Ombi langu kwa cdm pindi hawa magamba watakapohamia cdm mwakatae kwa nguvu zote kwani watakuja kuhitilafia chama chenu
 

ChiefmTz

JF-Expert Member
Apr 15, 2008
2,913
898
Tukune vichwa kuweza kushauri mikakati ya kuongeza ajira, mi ninayo ifuatayo kwanza kuwe na mradi wa nchi nzima wa kuunganisha vijiji kwa kiwango cha changarawe hii iwe standard kweli kweli yaani hadi mifereji ya kupitisha maji ya kudumu na makandarasi wawekewe sheria ya kuwaajiri locals kwa mambo yanasiyo hitaji shule hii itatoa ajira kwa vijana wa vijiji husika, pili kujenga nyuma za walimu/manesi kila kijiji. Tatu kupeleka umeme vijiji hii itatoa fursa zinazopatikana mijini zipatikane vijijini, nne kuimarisha soko la mazao kwa kuweka sera zitakazowezesha uanzishwaji viwanda vya kusindika.
Kwa ndoto mawazo haya yanawezekana. Lakini kiuhalisia uko mbali na ukweli. Na hii ni kutokana na kuto address matatizo ya kweli yanayoikabili nchi. Kwa ufupi tuna matatizo yafuatayo ambayo yanahitaji social,political na economical revolutions....2b continued....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom