kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 17,977
- 17,380
Waambieni wazazi, viongozi na wazee wenu ndani ya chama na familia hali halisi ya kisiasa mwaka huu. Waambieni kuwa vyama vya upinzani mwaka huu ni balaa tupu ili nao wapate muda wa kujiandaa polepole na aina ya matokeo ya uchaguzi hapo October 25, badala ya kuwadanganya viongozi na wazee wenu kwa kuwapa matumaini ya uongo (false hope) kuhusu chama chenu kuwa mambo ni safi sana, mgombea wetu ni chaguo la mungu, wanaghushi tu picha za mafuriko kwenye mikutano yao, ushindi kwetu ni lazima, UKAWA itasambaratika tu kabla ya October, tutamzuia mgombea wao asigombee, hawatafika kwenye 18 zetu, n.k. huku ukijuwa wazi kuwa unawadanganya. Kufanya hivyo sio vema maana mtasababisha wazee wenu waje kufa kwa pressure (stroke) na msongo wa mawazo (depression) pale matokeo ya uchaguzi yatakapokuja kuwa mabaya kwa upande wenu. Wazee haohao watakuja kuwalaumu sana na hawatawaamini tena.
Waambieni wazee ukweli ili kama wanataka kusali, kuroga, kulia, kusikitika, kukata tamaa, au kushauri kitu wafanye hivyo mapema huku wakiendelea kukata tamaa ya ushindi polepole. Waambie kuwa njia tunayopita mwaka huu ina miba na mbigili nyingi ili nao wasisahau kuvaa viatu vyao badala ya kuwaambia njia ni safi na kuwafanya wasibebe viatu vyao.