Vijana mnatoa wapi ujasiri wa kuoana na mtu uliyekutana naye mtandaoni?

Ivi mnatoa wapi ujasiri wa kufunga pingu za maisha na mtu uliejuana nae kupitia social network, mbaya zaid mwanzon mnaficha ukwel mkigombana mnaweka mambo hadharan
Kwani social media zina shida mkuu? Mkishindwana msitwishe social media lawama. Wenye shida ni wahusika. Kwani hakuna wanaokutana shuleni nyumba za ibada na kazinj na bado wakashindwana?
 
Kwani social media zina shida mkuu? Mkishindwana msitwishe social media lawama. Wenye shida ni wahusika. Kwani hakuna wanaokutana shuleni nyumba za ibada na kazinj na bado wakashindwana?
Kivipi kirahisi tu awe mwenza wa maisha kupitia hii mitandao inapotokea wanachana ndio ukwel unafahamika
 
Kivipi kirahisi tu awe mwenza wa maisha kupitia hii mitandao inapotokea wanachana ndio ukwel unafahamika
Mitandao tunaisingizia tu ndg yangu. Inatusaidia tu kukutana. Ss kufahamiana zaidi ni sanaa yako ukitumia mitandao si ni ww umeamua? Au mitandao imekuteka?? Tuwe waungwana kukubali ukweli na kuwajibika kwa maamuzi yetu sio kusingizia vitu visivyo ma uwezo wankushawishi mtu
 
Sijui ni umbumbumbu wa kiasi gani yaani mtu humjui hata background yake then wewe kijana unamuona mtandaoni mnapatana na unajicomit!
Shame on you kijana wa leo unaoa mwanamke wa mtandaoni huku mtaani wapenzi wamejaa chungu nzima wakitafuta pa kutokea
Wale wa social media wanaishi wapi mkuu?

Acheni kusingizia social media, watu ni wale wale. Wakitoka maakazini wanaingia mtaani jumapili wanaenda kanisani ijumaa msikitini. Ukikutana naa mtu popote ni lazima umchunguze kabla na ndio utajua back ground yake. Au kwako mkuu ukikutana na mtu kanisani ndio tiketi ya ndoa wiki inayofuata tu?
 
Tatizo sio social media, tatizo ni nyie wahusika.
Labda kama na hizo ndoa mnafungia kwenye social networks. Hivi hata mtu unayekutana naye barabarani, unajuaje kama ni mwema au muovu? Au ukimwona tu unakuwa umejua na background yake? Tunakutana na watu huku nje na maumivu tunakula kama kawaida. Haijalishi mmekutana wapi, ila ni umekutana na mtu wa aina gani na ana nia gani
 
Tumekutana online, tumekuwa friends, tumekuwa lovers, tumechunguzana...
...tukaoana na maisha yanaendelea.

Binafsi sikumbuki lini nilikutana na mtu kanisani/njiani/harusini/kwenye basi nikamtongoza. Online dating is the best...!!
 
Back
Top Bottom