Vijana meru watakaokiuka maadili na kuiga tamaduni za nje ya nchi kuchapwa viboko 60 hadharani

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
[h=2][/h]

Na GLADNESS MUSHI, Meru
UONGOZI wa Kimila ujulikanao kama Rika la Kilovio kutoka katika kabila la Kimeru
umepitisha sheria kali ya kudhibiti maadili kwa vijana wa kike na wa kiume hasa wale ambao wanaiga tamaduni za mataifa ya nje ya nchi ambapo kwa kijana atakayebainika kuiga au kukiuka maadili ya Kitanzania basi atalazimika kuchapwa viboko 60 hadharani
Hatua hiyo inakuja mara baada ya baadhi ya vijana katika eneo hilo la Meru kuanza tabia ya kuiga tamaduni lakini hata madili ya mataifa ya nje hali ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa maadili kuendelea kuporomoka.
Hayo yameelezwa na Bw Akundaely Mbisse ambaye ni kiongozi wa marika ya vijana katika kabila hilo wajulikao kama “Kilovio”wakati wakimsimika na kumuingiza rasmi kiongozi wa vijana katika eneo hilo la Mareu Bw Herieli Mafie mapema jana.
Mbisse alisema kuwa utaratibu huo wa kuwapa vijana adhabu ya viboko 60 utaweza kurudisha maana halisi ya kijana wa kabila hilo ambapo kwa sasa jamii ya Mkoa wa Arusha bado inaonekana kuendelea kulelemewa na tatizo la vijana wengi kuiga tamaduni za nje ya nchi huku hali hiyo nayo ikichangia sana hata ubaribifu wa amani ya Kaya,hadi mkoa.
Alifafanua kuwa adhabu hiyo ya viboko 60 hadharani itaenda sanjari na vijana wote wenye tabia mbalimbali ambazo hazina tija kwenye jamii hiyo ya Meru kama vile Uzinzi, ulevi wa kupindukia saa za kazi, wizi, Mavazi yanaonesha maumbile,ukosefu wa adabu pamoja na makosa mengine ambayo chanzo chake ni kuiga maadili yasiyokuwa na tija kwennye jamii.
“Tumejipanga kuhakikisha kuwa wilaya hii ya Meru inakuwa na utofauti wa hali ya juu sana kwani tunao uwezo wa kuwaweka vijana wetu wawe katika maadili mazuri, na masuala kama vile uvaaji wa nguo za ajabu utaisha na kwa hali hiyo jamii itaweza kupungza hata ujinga unaofanywa na baadhi ya vijana wachache huku wakisingizia umaskini’aliongeza Mbisse.
Naye mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wailaya ya Meru Furaini Mungure akiongea kwa niaba ya mgeni rasmi John palangyo ambaye ni mjumbe wa kamati ya siasa mkoa wa Arusha alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa sana wa maadili ya kila kabila kurudiwa ili kuweza kuwajengea vijana uwezo wa kufanikiwa zaidi kwenye maisha yao ya kila siku.
Mungure alisema kuwa suala hilo la ulindaji wa maadili lina manufaa sana sio kwa vijana kwani hata kwa taifa kwani kwa sasa wapo baadhi ya vijana ambao wanaharib na kuvunja amani ya Nchi kwa kuwa hawana maadili ambayo yanaanzia ngazi za marika hadi taifa.
 
uko meru kweli kuna mazuzu. yani mtu aanze kunichapa hizo fimbo. nitammachame ..
 
Wajitahidi wasogee kijiji cha njani na nshupu kule vijana wa kiume ni bangi na pombe na wa kike wameishia uzinzi, hawana interest ya kusoma.
 
Serikali gani itaruhusu raia wachapane viboko 60 bila idhini ya mahakama?
 
Serikali gani itaruhusu raia wachapane viboko 60 bila idhini ya mahakama?

Viboko unavyochapwa nyumbani na baba yako ukikosea huwa anaomba kibali mahakamani? Hivyo ni viboko baba zangu wa kimeru wameandalia toto tundu zao.Na kiboko cha kimeru cha uhakika angalia kile alichoshika mwenye kikofia chekundu kwenye picha.Ukiipigwa nacho viboko sitini ukiinuka breki ya kwanza ni kulazwa mount meru hospital na kuhama Arusha na ukware wako forever.
 
Hauwezi kushindana na globalization wala culture dynamics..hakuna kitu hapo, watachemka
 
Dunia inaenda mbele mabadiliko ni lazima enzi zao wakiwa wanavaa ngozi je zilikuwa zinawastiri mwili mzima?Enyi wazee kizazi hiki sio cha kideri na loshoro maazimio ya kimila yalishapitwa na wakati ndio maana tumeachana na usafiri wa baiskeli tunapanda pikipiki ili kuwahi.
 
Kwa hiyo wale dada zao waliopo vyuo mbali mbali siku wakienda likizo makwao lazma wajiju manake maisha ya vyuoni ndo stage ya kwanza ya utandawazi wa mavazi
 
Back
Top Bottom