Vijana kutanguliza maslahi binafsi kuliko maslahi ya taifa ni zao la jamii

ndegemzungu

Member
Mar 10, 2019
92
240
Habar zenu members wa jukwaa hili.

Niende moja kwa moja kwenye mada vijana wengi hulaumiwa siku kwa kutanguliza maslahi binafsi kuliko maslahi ya taifa,wazee ndio watu hasa hutoa lawama hzi kwa vijana.

Lakini kwa maoni yangu tatzo linaanza kwenye ngazi ya familia pale mzazi anapo msisitiza mwanae asome kwa bidii ili maisha yake yaje kuwa mazuri hapo unaona kabsa mtoto anaandaliwa kuja kuwa mbinafsi yani akasome maisha yake ndio yaje kuwa mazuri sio aje kuikomboa jamii.

Mtoto akifika shule anakutana na mwalimu tena hapa ndio kwenye tatzo kubwa zaidi kwa sababu mwalimu hutumia muda mwingi kukaa na mwanafunzi kuanzia shule ya msingi,sekondari mpaka chuo kikuu lakini katka ngazi zote hzi walimj humsisitiza kijana kusoma kwa bidii ili maisha yake yaje kuwa mazuri,

Wanazidi kumhamasisha aje kuwa mbinafsi yani wanasahau kabsa kumfundisha umuhimu wa taifa lake wanashindwa kumwambia kuwa ustawi na hatma ya taifa lake unatemgemea sana yeye kama kijana

Wanashindwa kumfundisha kijana tangu akiwa mtoto namna ya kuipenda na kuithamini nchi yake,lakini humsisitiza tu asome maisha yake yaje kuwa mazuri wanamuandaa kijana kuwa mbinafsi.

Kwa iyo kijana kutanguliza maslahi binafsi mbele sio tatzo lake ndivyo jamii imemkuza awe ivyo.
 
Back
Top Bottom