Vijana kupewa mafunzo miezi 4 kabla ya kupewa mashamba na uwezeshwaji, asante Rais Samia

Mar 12, 2019
28
20
Na Mwl Udadis, Kiteto

Hatimaye kundi la kwanza la vijana 812 kutoka Mikoa yote nchini linatarajiwa kuanza mafunzo muhimu ya kilimo kwa muda wa week 16 kuanzia tarehe 17 Mwezi March. Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia itagharamia Mafunzo na gharama ya chakula na malazi.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, iliyokuwa inaonekana kama ndoto sasa inaonekana kama jambo linalowezekana. Licha ya uwepo wa rasilimali ardhi yenye ukubwa wa karibu hekta milioni 40 inayofaa kwa kilimo, kilio kikubwa imekuwa Ardhi, mafunzo & mitaji kwa vijana kujihusisha kilimo.

Vijana kupewa mashamba bure, mafunzo na pembejeo, ni jambo lililokuwa likionekana kuwa haliwezekani kwa muda mrefu. Kwa mara ya kwanza sio tu Tanzania bali Afrika, Rais wa nchi anaamua kuchukua hatua zinazolenga kumgusa kijana kwa namna ya tofauti na endelevu. Kijana anapewa Nyavu na si Samaki aliyevuliwa!

Mpango huu wa Rais Samia kuwainua vijana kupitia kilimo biashara sio tu utazalisha ajira bali utachochea ukuaji wa viwanda, kuvutia wawekezaji nchini, kuifanya Tanzania kuwa kimbilio katika hifadhi ya chakula Afrika (Food Basket) na zaidi kuimarisha uchumi wa nchi yetu.

Kama jinsi viongozi mbalimbali Afrika na Taasisi za kimataifa kama vile Benki ya Maendeleo ya Afrika, AfDB walivyoonyesha kuvutiwa na mpango wa Rais Samia, Mimi nami naungana na wote wanaoitakia kheri Afrika kumpongeza Mama yetu Samia Suluhu Hassan kwa maono haya ya aina yake.

Awamu ya sita imekuwa ni awamu ya vijana hivyo Kama vijana hamna budi kutumia fursa hii ili kuweza kukuza uchumi wa Taifa na uchumi wa mtu mmoja mmoja
 
Back
Top Bottom