Vijana fanyeni kazi. Binadamu ni wanafiki, kamwe usiwaamini watu wanakuahidi watakuinua na kukusaidia

Mboka man

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
478
1,638
Siku ya leo nataka kuzungumza na wale vijana wenzangu ambao ni jobless lakini mkoo nyumbani hamna mishe yeyote mnayofanya huku mkitegemea kuna ndugu au jamaa alikuahidi ya kwamba.

Atakufanyia mpango upate kazi kampuni flani au serikalini au kuna hela atakufanyia mpango akupatie ukupe mtaji ufanye biashara.

Nasema hivi binadamu wengi ni wanafiki kamwe usiamini kile unachosikia ila amini kile unachotendewa hawa watu ukiwaamini watakuchelewesha kutimiza ndoto zako.

Fanya kazi yeyote ile halali ya kukupatia kipato utakuja kunishukuru badae.
 
Kila binadamu ni mbinafsi kwa asili.

Matajiri wanataka kuendelea kuwa matajiri wao.

Hata mtu anayekuhimiza au kukutia moyo uendelee kupambana, pengine anatamani ufanikiwe kweli, lakini amini kwamba kamwe hataki umzidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom