Vijana CUF wataka mitihani Z’bar irudiwe

Vijana CUF wataka mitihani Z’bar irudiwe

Sumasuma

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2011
Posts
342
Reaction score
110
Talib Ussi, Zanzibar
JUMUIYA ya Vijana ya CUF (JUVICUF), imeelezea kusikitishwa kwake kuhusu kufutwa kwa matokeo ya mitihani ya kidato cha nne ya skuli kadhaa za Zanzibar.

Jumuiya hiyo imesema kitendo hicho kinaonyesha kuwa Serikali haina nia njema na maisha ya wanafunzi hao.

Hayo yamo katika taarifa ya chombo hicho kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Katibu Mkuu wake, Khalifa Abdallah Ali.

“Unapowafutia matokeo watoto hao unawasababishia athari kubwa za kisaikolojia na hata kushindwa la kufanya,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilisema walimu ndiyo wanaopaswa kubeba lawama kuhusu kuvuja kwa mitihani na kwamba inasikitisha kuona kuwa hawahukumiwi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo jumuiya hiyo haiamini kama msingi wa tatizo hilo ni wanafunzi pekee yao.

“CUF ilishasema kuwa inapotokea kesi kama hiyo, Baraza la Mitihani linapaswa kuwachukulia hatua wale waliosababisha kuvuja kwa mitihani na mitihani hiyo ichapishwe upya,” ilisisitiza taarifa.

“Tunaiomba wizara ihakikishe kuwa mitihani hii inarejewa ili wanafunzi walioathirika watendewe haki yao,” ilisema.

Taarifa hiyo ilisema kurejewa kwa mithani si jambo geni hasa ikizingatiwa kuwa ilishawahi kurejewa katika baadhi ya mikoa kama Dar es Salaam .:A S 465:
 
Hapo Point ni kwamba saikolojia ya mtoto inavurugika sana
 
Talib Ussi, Zanzibar
JUMUIYA ya Vijana ya CUF (JUVICUF), imeelezea kusikitishwa kwake kuhusu kufutwa kwa matokeo ya mitihani ya kidato cha nne ya skuli kadhaa za Zanzibar.

Jumuiya hiyo imesema kitendo hicho kinaonyesha kuwa Serikali haina nia njema na maisha ya wanafunzi hao.

Hayo yamo katika taarifa ya chombo hicho kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Katibu Mkuu wake, Khalifa Abdallah Ali.

"Unapowafutia matokeo watoto hao unawasababishia athari kubwa za kisaikolojia na hata kushindwa la kufanya," ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilisema walimu ndiyo wanaopaswa kubeba lawama kuhusu kuvuja kwa mitihani na kwamba inasikitisha kuona kuwa hawahukumiwi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo jumuiya hiyo haiamini kama msingi wa tatizo hilo ni wanafunzi pekee yao.

"CUF ilishasema kuwa inapotokea kesi kama hiyo, Baraza la Mitihani linapaswa kuwachukulia hatua wale waliosababisha kuvuja kwa mitihani na mitihani hiyo ichapishwe upya," ilisisitiza taarifa.

"Tunaiomba wizara ihakikishe kuwa mitihani hii inarejewa ili wanafunzi walioathirika watendewe haki yao," ilisema.

Taarifa hiyo ilisema kurejewa kwa mithani si jambo geni hasa ikizingatiwa kuwa ilishawahi kurejewa katika baadhi ya mikoa kama Dar es Salaam .:A S 465:

Naunga hoja mkono.
 
Back
Top Bottom