Vijana CCM wamgeuka Kikwete! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijana CCM wamgeuka Kikwete!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by LordJustice1, Mar 30, 2011.

 1. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM), umemgeuka Rais Jakaya Kikwete.

  Unamtuhumu kushindwa kazi. Unamtaka kuachia nafasi ya uongozi katika chama chake ili kuwepo mchakato wa kukiimarisha.

  MwanaHALISI limeelezwa kuwa Baraza la Vijana limeona kuwa Kamati Kuu (CC) ya chama, ambayo huwa chini ya mwenyekiti Kikwete, imeshindwa kusimamia serikali.

  Baraza limetaka, pamoja na mambo mengine, Kikwete afanye mabadiliko kwenye muundo wa CC kwa kuwaondoa wajumbe ambao ni mawaziri ikiwa njia ya kukiimarisha chama.

  Mapendekezo ya vijana ya kumtaka Kikwete kuachia ngazi katika nafasi ya mwenyekiti, yamepangwa kuwasilishwa kwake mwenyewe Alhamisi wiki hii na viongozi wa umoja huo wakiongozwa na kamanda wao, Kingunge Ngombale Mwiru.

  “Pale Dodoma tulikubaliana kuwa na maamuzi ya aina mbili, ameeleza mjumbe mmoja wa baraza la vijana kwa sharti la kutotajwa gazetini.

  Amesema, “Kwanza ni yale ambayo yatasomwa kwa waandishi wa habari na kufahamika na umma na pili, yale ya siri ambayo tutamkabidhi rais moja kwa moja.”

  Taarifa kutoka ndani ya baraza la vijana lililokutana jijini Dodoma, Jumamosi iliyopita, zinasema uamuzi wa kumtaka Kikwete kuachia nafasi ya mwenyekiti uliibuka wakati wa mjadala juu ya ajenda ya ushiriki wa vijana katika uchaguzi mkuu uliyopita.

  Mjadala uliibuka pale baadhi ya wajumbe walipochangia kwa kudai kuwa matokeo mabaya ya uchaguzi yalitokana na Kikwete kusafiri sana nje ya nchi, jambo ambalo lilimfanya ashindwe kujenga chama chake.

  Mbali na kutaka kutenganisha kofia ya mwenyekiti na ile ya rais, UV-CCM wanaituhumu Usalama wa Taifa kwa kile unachodai “kushindwa kumsaidia rais.”

  “Idara hii imeshindwa kuisaidia serikali. Inashughulika na mambo madogo yanayohusu watu, badala ya kumshauri rais kuhusu mambo makubwa ya kitaifa yaliyo muhimu kwa wananchi,” inasema sehemu ya mapendekezo ya vijana wa CCM ambayo yatapelekwa kwa rais.

  Mapendekezo ya vijana, taarifa zimeeleza, yatawasilishwa kwa Rais Kikwete kesho. Ujumbe utakaowasilisha mapendekezo hayo umetajwa kuongozwa na kamanda wao, Kingunge Ngombale-Mwiru.

  “ Kama usalama wa taifa wangekuwa wanafanya kazi vizuri,” UV-CCM imenukuliwa ikihoji, “wangemweleza rais kuhusu makundi yaliyopo katika chama chake. Lakini badala ya kufanya kazi, wameingia katika siasa za makundi ya ndani ya CCM.”

  Wanasema, “Hawa watu (usalama), wameshindwa kufanya kazi yao kwa weledi…”

  Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja huku kukiwa na habari kuwa mnyukano mkubwa uliibuka ndani ya kikao cha baraza la vijana, kati ya makundi mawili – lile linalomuunga mkono Edward Lowassa na ile linalompinga.

  Hoja nyingine inayopelekwa kwa Kikwete inahusu “udhaifu wa mawaziri katika kutimiza kazi zao.” UV-CCM wanadai mawaziri hawafanyi maamuzi; badala yake wanategeana ili atakayethubutu kufanya maamuzi “aharibikiwe na aonekane mbaya.”

  Umoja huo umesema mawaziri wanapofanya kazi zao wanatekeleza ilani ya uchaguzi ya chama chao, lakini hilo halifanyiki kwa kuwa mawaziri wengi wamejikita katika biashara zao binafsi au wanasaka madaraka ya urais kwa mwaka 2015.

  “Mawaziri hawafanyi kazi kwa sababu hawataki kufanya maamuzi. Matokeo yake rais anaonekana hafai. Hatua ya mawaziri kuacha kufanya maamuzi mazito, imechangia kwa kiasi kikubwa rais kushambuliwa kila uchao na vyombo vya habari,” inasema sehemu ya taarifa hiyo.

  Vyanzo vya taarifa vya gazeti hili vinasema, ndani ya baraza la vijana baadhi ya wajumbe walipangwa kutetea baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi.

  Mmoja wao (jina tunalo), alinukuliwa akisema kuhusu kashfa ya Richmond na kujiuzulu kwa Lowassa kuwa, “ Kama kuwajibika katika kashfa hiyo, aliyepaswa kuwajibika ni rais mwenyewe aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la mawaziri.”

  Kauli ya mjumbe huyo kumtetea Lowassa ilifuatia mjumbe wa baraza kutoka mkoani Arusha, Mrisho Gumbo kutaka chama chake kuwatosa watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini ambao wanashilikia nafasi katika chama.

  Akichangia katika kikao hicho, Mrisho alisema, “Ukiwa kijana, na ukawa mnafiki, basi ukiwa mzee utakuwa mchawi. Kama tunataka chama hiki kijivue gamba, basi mwambieni Rais Kikwete awaondoe Lowassa, Rostam na Chenge katika vikao vya maamuzi.”

  Alisema, “Naiomba meza kuu; mpelekeeni salamu mwenyekiti. Kama anataka chama kijisafishe awaondoe Lowassa, Rostam na Chenge katika vikao vya maamuzi. Hawa ndio wanaosababisha chama chetu kitukanwe.”

  Naye Shy-Rose Banji, akizungumzia matokeo mabaya ya uchaguzi kwa chama chake alisema, “Makamba is the problem (Makamba ndiye tatizo). Tumefika hapa kwa sababu yake kushindwa kazi,” alisema Banji huku akielekeza macho yake kwa Makamba aliyekuwa miongoni mwa wajumbe wa mkutano huo.

  Alisema, “Kila kukicha katibu mkuu anaandikwa kwenye vyombo vya habari, mara hivi, mara vile. Hili ni tatizo kwa chama…”

  Lakini Makamba hakuwa na simile. Haraka aliinuka na kusema, “Shy Rose…mbona wewe unaandikwa sana . Unavaa nguo fupi na una hawara, tena mtu wa CHADEMA…?”

  Alikuwa Edwin Sanda, mjumbe Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), kupitia UV-CCM, aliyeingilia kati “mipasho” ya Makamba.

  Alisema, “… katibu mkuu anaingilia mambo binafsi ya watu. Hii si ajenda. Mjumbe amejadili tatizo la chama, linalosababishwa na mtendaji mkuu wa chama, lakini mzee Makamba unakuja kuelezea maisha binafsi ya mjumbe. Hii si sahihi.”

  Naye Husseni Bashe akitetea Makamba na kuhusu madai kuwa uongozi wake ulichangia kufanya vibaya alisema, bunge lililopita pia lina mchango mkubwa sana katika kutofanya vizuri kwa chama chetu kwenye uchaguzi huo.

  Alisema spika wa wakati huo, Samwel Sitta “aliongoza bunge ambalo lilizidisha mpasuko wa wabunge na hatimaye wana-CCM wote katika kipindi cha kuelekea uchaguzi.”

  Alitoa mfano wa kashfa ya mkataba tata wa Richmond iliyosababisha kujiuzulu kwa Edward Lowassa katika nafasi yake ya uwaziri mkuu.

  Bashe alidai ndani ya kikao kuwa ana ripoti mbili za Richmond , lakini zikizungumzia jambo moja, huku zikiwa na maudhui tofauti.

  Alisema, “Jamani watu hapa wanazungumzia habari ya Richmond , ukweli mimi ninaujua…Hii ilikuwa ni chuki binafsi kati ya Sitta na Dk. Mwakyembe dhidi ya Lowassa.”

  Kuhusu udhaifu wa Makamba, Bashe alisema, “Makamba hajajiteua. Ameteuliwa. Kama kuna makosa, basi aliyemteua ndiye awajibike” – bila shaka Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete.

  Kwa upande wake, Ridhiwani Kikwete aliasa wajumbe kujadili hoja, akisema “wenzetu wa CHADEMA wana mikakati ya kufanya vitu vyao na wana uwezo wa kuitekeleza.” Hata hivyo, hakuna aliyejali rai yake.

  Mtetezi mashuhuri wa Lowassa, James Millya alisema, “Chama hiki kinavurugwa na Sitta na Dk. Mwakyembe kwa kueneza vitu vya uwongo dhidi ya Lowassa.”

  Katika hatua nyingine UV-CCM wamemtaka Kikwete kuagiza Makamba kumfukuza Tambwe Hiza kutoka idara ya porapaganda ya chama hicho kwa kuwa “ameshindwa kazi.”


  Source: MwanaHalisi.
   
 2. s

  smz JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ehee,

  Sasa ngoma inogile, hata kuicheza sasa ni raha. "Makamba anamwambia Shyrose ana hawara CHADEMA". Huyu ni mtendaji mkuu wa ccm. Kazi kweli kweli.

  Tuone hiyo siku watakapokutana Dodoma kumvua kofia ya uenyekiti JK, watakuwa wameandika historia nji hii. Wish you all the best>
   
 3. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Wacha wachapane bakora na kunyukana wengine tulisoma alama za nyakati tukaamua kujitoa kuwa hatuna chama tunawaangalia kwanje tukicheka tu maana ni donda sugu halitibiki:lol:
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Akina Benno Malisa, sasa mbona kumbe mlikua na majibu sahihi ya ugonjwa wa Chama Cha Mapinduzi na badala yake mkaanza kwa kujiumauma, kuzunguka mbuyu na kuwachnganya zaidi Wa-Tanzania juu ya uthabiti wa msimamo na mwelekeo wenu??

  Pamoja na yote, mjue ya kwamba kutamka maneno yeye kukitakia mema CCM ni jambo moja na kuyatekeleza kwa vitendo ili matunda ya kugusika kwa mikono na kuonekana kwa macho yaje yatokee ni jambo lingine kabisa.

  Sasa mjue kwamba mpaka hapa ni kwamba Wa-Tanzaania tunajihesabilia kwamba tayari mmetuahidi juu ya mambo haya kuyafanyia kazi na kwamba tofauti na hapo basi tuwe huru kuwahamisheni rekodi zaenu kwetu toka BAD kwa sasa hadi WORST!!!!!!!!

  Ndio kama hivi UVCCM tunawasubirini na kwamba tunawafuatilieni kwa sana tu maana tumegundua kwamba pamoja na kwamba UVCCM kunejaa madalali wengi juu ya kuuza haki za wananchi kwa bei rejareja, hilo tu halituzuia kamwe kutambua ukweli kwamba vile vile kuna vijana wache humo ambao ni wazuri sana tu.

  Hata hivyo nyinyi kumuondoa tu Kikwete na sura nyinginezo hakutosaidia kitu. Huko CCM hatukimbii tu sura bali kubwa zaidi tunakimbia MFUMO WA KI-UJIMA UJIMA vile mle ndani, kwenye serikali yake na taasisi zake mbalimbali nchini.

  Fanyeni homework zaidi vijana wenzetu na kujiuliza maswali yote magumu na kuyatafutia majibu tosheleza.
   
 5. Ba Martha

  Ba Martha JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wacha wafu wawazike wafu wenzao...halafu nini kazi ya usalama wa taifa..taifa ni ccm???
   
 6. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hii movie ya ccm na uvccm inaboa!
   
 7. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Suala linaloumiza vichwa eti ni urais wa 2015! Yaani hawa jamaa wanawaza muda wote kubaki madarakani badala ya kuwaletea maendeleo wananchi, kaaaaazi kweli kweli!
   
 8. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  shy-rose anatembea na nani? Dr Slaa (dokta wa ukweli aka PhD) nini? kwa sababu naye kwa totz anaonekana hajambo, mfano kutoka kwa roze kamili to Mumbushi na sasa shy-rose? Hahaaaa.

  Halafu nashangaa mnayoione huruma CCM. Acheni tu ijiifie mara JK atakapoondoka kwani imetutenda kwa mabaya mengi. RIP CCM.
   
 9. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  CCM si chama bali ni genge la wahuni:embarassed2:
   
 10. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,061
  Likes Received: 3,089
  Trophy Points: 280
  napenda sana hzo sarakasi za ccm.,walikula ya mbuzi ...tutajua mengi watanzania.,CCM tatuka kama nguo ...tusubili kuambiwa JK alikuwa na nyumba ndogo ngapi,nani kajiuzia Ngorongoro,..Mama Salma katumia hela ya watanzania kiasi gani,n.k
   
 11. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,511
  Likes Received: 2,751
  Trophy Points: 280
  Wanaanza kuamka taratibu!!
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ngoma inayovuma sana haikawii kukasuka
  :target::target::target::target::target::target::target::target::target::target::target::target::target:
   
 13. d

  donmzushi Member

  #13
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawana jipya wanajikosha tuu hawa wavuruga amani. . .
   
 14. J

  Juma. W Senior Member

  #14
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 131
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  UV-CCM wanayaona makundi leo? Hawajui makundi yamekaa kimaslahi zaidi? Wanajifunika shuka asubuhi wakati kumekucha....
   
 15. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #15
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,144
  Likes Received: 2,178
  Trophy Points: 280
  Huo ni muonekano wako sio wake Je Ukiambiwa anatembea na Mkeo Atakuwa na Muonekano Upi Hapo!
   
 16. D

  Domo Zege JF-Expert Member

  #16
  Mar 31, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Ww nani kakuambia slaa ndo anaemchukua huyo shy rose, kwan chadema ina dr slaa tu.Jadili mambo ya msingi sio kuanza kufuatilia mambo binafis ya watu
   
 17. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #17
  Mar 31, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  "eti TISS imeshindwa kumshauri vizuri jk kuhusu mstakabari wa ccm"- usalama wa taifa kumbe kwa ccm ni usalama wa ccm". ipo kazi kweli kweli. Ni sawa na kugeuza kazi za cia za usa kuwa kazi za chama cha republican au demokratic. ccm wanaumwa donda ndugu; ndo maana wao ndo chanzo cha kuvuruga uchaguzi na amani ya nchi hii kwa kuwatumia TISS!!! Hoja ya Dr. Slaa kuwa TISS walivuruga uchaguzi sasa imethibitishwa na UV-CCM wenyewe.
   
 18. mundo

  mundo JF-Expert Member

  #18
  Mar 31, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Kwani Usalama wa Taifa(UWT) ni wa chama cha mapinduzi(CCM)?
   
 19. Mshindo

  Mshindo JF-Expert Member

  #19
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 479
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Una histrory yeyote ya head injury katika maisha yako labda? If yes,the problem is begining to surface.:fish: sorry buddy!
   
Loading...