Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 710
- 1,610
Hii ni zaidi fezea.
Vijana wanasema Gwajima ana sehemu nyingi kufikisha taarifa hiyo lakini kaamua kwenda kwenye media na kwa kufaanya hivyo ni kusababisha taharuki.
Wanasema pia Gwajima kuongelea kuhusu uchaguzi na utenguzi wa viongozi wa vyombo vya usalama ni utovu wa nidhamu, maana wanachaguliwa kwa kufuata katiba na si kwa upendeleo.
Wasema tunaelekea kwenye uchaguzi hivyo wanasiasa wanatakiwa kuchunga ndimi zao ili wasitoe mambo yanayoweza kuleta machafuko nchini. Wasema wanasiasa wasitumie uchonganishi kama mtaji wa kupata huruma wa kura za wananchi.
Hemedi Hassan Salim, Katibu wa Hamasa Wilaya ya Kinondoni.
"Hakuna mwananchi au kiongozi awe wa CCM au wa CHADEMA hata vyama vingine anayeunga mkono Utekaji, hiyo ni kinyume na utu wetu lakini tusitumie vitendo hivi katika mlengo wa kisiasa"
"Tunaomba Chama cha Mapinduzi kufanya maamuzi juu ya Gwajima. Hatufurahishwi na kumuona bado anakuwa M-NEC na mbunge wetu baada ya kumtukanisha Rais Samia na wananchi wake. Fanyeni maamuzi na kutuletea watu wanaofahamu miiko ya Chama chetu"
Kaijande mwananchi wa Kata ya Kunduchi
"Huku Jimboni alitoa ahadi nyingi sana hasa kwa vijana na hajatimiza hata moja. Alituita vijana akatuandikisha majina ili tuweze kujiajiri akatupikia na wali tukafurahi lakini hajawahi kutimiza. Anasema Bungeni hapewi dakika na hasikilizwi ni muongp, sisi tulitegemea aje atueleze kuhusu kwanini hajatimiza ahadi zake anaenda kumshambulia Rais"
"Mwaka 2020 Gwajima hakushinda kwa kura za maoni, hakuwa mshindi wa kwanza hata wa pili alikuwa mshindi wa tatu. Ila hivyo vyombo anavishambulia sasa hivi ndiyo vilimpa nafasi hiyo"
Wataka Gwajima afukuzwe uanachama