ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,049
- 49,733
NI mwendo wa ajira, ndivyo unavyoweza kusema baada ya jana serikali kutangaza ajira mpya 8,070 za kada ya afya ambazo mchakato wake unakaribia kuiva muda wowote kuanzia sasa.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Deogratius Ndejembi, ndiye aliyetangaza neema hiyo jana bungeni, huku akitoa angalizo kwa wakurugenzi wa halmashauri kutopitisha barua za uhamisho kwa watumishi ambao hawajatimiza miaka mitatu kwenye vituo vyao vya kazi.
Ndejembi alitoa ufafanuzi huo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Minza Mjika, aliyehoji ni lini serikali itaongeza watumishi wa afya Hospitali ya Wilaya ya Meatu.
Akijibu swali hilo, Ndejembi alisema katika mwaka wa fedha wa 2022/23, serikali itaajiri watumishi wa kada ya afya 8,070 na baada ya taratibu za ajira kukamilika watumishi hao watapangwa kwenye halmashauri zote nchini, Meatu ikiwamo.
Alisema serikali imeendelea kuajiri watumishi wa kada mbalimbali za afya na katika mwaka wa fedha 2021/22 serikali iliajiri watumishi 7, 736 wa afya na Halmashauri ya Wilaya ya Meatu ilipangiwa watumishi 104 na watumishi saba walipangwa Hospitali ya Wilaya ya Meatu.
Awali, akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Liwale (CCM), Zuberi Kuchauka kuhusu kuhama kwa watumishi wanaopangwa katika maeneo mbalimbali, Naibu Waziri Ndejembi alikiri serikali inatambua tatizo hilo na tayari inaweka mikakati kwenye ajira mpya ambazo watumishi wanatarajia kuanza kazi hivi karibuni.
Kuchauka, katika swali lake, alisema kumekuwa na wimbi kubwa la watumishi wa afya kuhama kwenye halmashauri hasa za pembezoni ikiwamo ya Liwale ambayo ilipata watumishi 80 na waliobaki sasa hawafiki 15.
“Watumishi wanahama 36 wanaletwa wawili, Je? serikali ina mpango gani wa kudhibiti huu uhamaji holela?” alihoji.
Ndejembi alisisitiza kuwa; “Tutaweka mikakati ambayo itadhibiti wimbi hili la watu kuhama na nichukue nafasi hii kuwaagiza wakurugenzi wa halmashauri ambao ndiyo waajiri katika maeneo hayo wahakikishe hawapitishi barua kwa mtumishi yeyote ambaye hajathibitishwa kazini.
“Mtumishi anatakiwa akae kituo chake kipya cha ajira angalau miaka mitatu, kwa hiyo wafuate utaratibu wasipitishe barua hizi ili watumishi hawa wafanye kazi, wameajiriwa kwenda kupunguza upungufu ambao upo kwenye maeneo hayo, sasa wakipitisha barua ili hawa wahame wanazidisha upungufu kwenye maeneo hayo.”
Ndejembi alisema watumishi hao walipoomba ajira hizo walikuwa tayari kufanya kazi eneo lolote la Tanzania.
My Take
Msipotoka Kimaisha Miaka hii ya Rais Samia kuanzia mkulima Hadi msomi basi hesabu maumivu maana baada yake wanakujga wale wa roho za korosho,nawakumbusha tu.