Vigogo zaidi wa BOT watinga kortini

Waliofikishwa mahakamani ni wanne akiwamo MWanasheria Bosco KImela ambaye yumo katika kesi za EPA. Wengine ni Simon Eliezer Jengo, Kisima Thobias Mkango na Ally Farjallah Bakari
 
Je wamepewa dhamana au wameenda kunyea DEBE segerea? Nafikiri watakutana na LIYUMBA wajikumbushe walivyofanya UFISADI
 
Nasubili kwa hamu sana kuona Zakia, Mramba, Mgonja et al kuona nao wanaongezwa kwenye list hiyo vinginevyo ni kiini macho tu bora wawaachie tu waendelee kupeta uswazi kwa nini mapapa wanawaogopa? Na kuishia kukamata vidagaa tu ambavyo ni chambo?
 
Waliofikishwa mahakamani ni wanne akiwamo MWanasheria Bosco KImela ambaye yumo katika kesi za EPA. Wengine ni Simon Eliezer Jengo, Kisima Thobias Mkango na Ally Farjallah Bakari

Wanashitakiwa kwa tuhuma/Makosa gani? Mwenye details atupatupatie tafadhali.
 
Waliofikishwa mahakamani ni wanne akiwamo MWanasheria Bosco KImela ambaye yumo katika kesi za EPA. Wengine ni Simon Eliezer Jengo, Kisima Thobias Mkango na Ally Farjallah Bakari

Wanashitakiwa kwa tuhuma/Makosa gani? Mwenye details atupatie tafadhali.
 
Akikamatwa fisadi nambari one Jakaya Kikwete, itakuwa powa sana, na hakutakuwa na ufisadi tena Tanzania.
 
KUna taarifa rasmi kwamba kuna mtumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa. Taarifa zaidi baadaye.

wanne kizimbani leo kujibu mashataka ya EPA na uhujumu uchumi


MSHITAKIWA Bosco Kimela ambaye alikuwa ni ofisa wa Benki Kuu (BoT), anayekabiliwa na kesi ya wizi wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), amepandishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, akikabiliwa na tuhuma za kuhujumu uchumi.

Kimela alipandisha kizimbani jana pamoja na waliokuwa maofisa wengine wa BoT, ambao ni Simon Jengo, Kisima Mkango na Ally Bakari, ambapo walisomewa mashitaka matatu ya kuhujumu uchumi.

Aidha katika kesi hii, Kimela na wenzake wanakabiliwa na tuhuma za kughushi na kuhujumu uchumi kulikoisababishia Serikali kupata hasala ya zaidi ya Sh Bilioni 104.1.

Washitakiwa hao, walirudishwa rumande kutokna na kesi hiyo, kutoruhusu wao kupata dhamana kwa mujibu wa sheria.waliondoka mahakamani wakiwa wamesimama katika kalandinga, baada ya kukosa siti katika gari hilo la mahabusu.

Kimela alikuwa ni Kaimu mwanasheria katika BoT, wakati Jengo alikuwa Director of banking, Mkango Deputy director currency of BoT na Bakari alikuwa Director of banking.

source; Michuzi
 
ina maana walichapisha noti au waliiba noti? huyu kimela kwenye epa yupo, kuhujumu uchumi yupo kila mahali? je hizi ndiyo zile kesi alizosema kikwete zimeiva?
 
Kimela alikuwa ni Kaimu mwanasheria katika BoT, wakati Jengo alikuwa Director of banking, Mkango Deputy director currency of BoT na Bakari alikuwa Director of banking.

Wote wawili cheo kimoja? Au ilikuwa kwa nyakati tofauti?

Amandla....
 
Vigogo wengine BoT kortini wadaiwa kusababisha hasara ya Sh104 bilioni

Pauline Richard na Salim Said

VIGOGO wanne wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi, ikiwemo la kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh104 bilioni katika mkataba wa uchapishaji wa noti.

Kufikishwa mahakamani kwa vigogo hao kumekuja siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza kuwa kuna kesi tatu zitafikishwa mahakamani wakati wowote dhidi ya vigogo, ikiwa ni mwendelezo wa vita dhidi ya ufisadi.

Tayari maofisa wa BoT wameshafikishwa mahakamani kwa tuhuma za kufanikisha wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) na matumizi mabaya ya ofisi yaliyosababishia serikali hasara katika ujenzi wa majengo ya maghorofa pacha ya makao makuu ya taasisi hiyo ya fedha.

Tofauti na kesi hizo za awali, watuhumiwa hao wanne wa jana wameshtakiwa chini ya sheria ya uhujumu uchumi ya mwaka 2002.

Wakurugenzi hao wameshtakiwa kwa makosa tofauti, likiwemo la kupandisha gharama za uchapishaji noti tofauti na gharama za awali zilizo kwenye mkataba mkuu na kusababisha hasara hiyo.

Waliofikishwa mahakamani jana ni Simon Jengo, ambaye ni mkurugenzi wa huduma za benki wa BoT, Kisima Thobias Mkango (kaimu mkurugenzi wa fedha), Bosco Kimela (kaimu mkurugenzi wa huduma za sheria) na Ali Farjalah Bakari, ambaye pia ametajwa kuwa ni mkurugenzi wa huduma za benki.

Mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Benny Lincon alimwambia hakimu Samuel Maweda kuwa vigogo hao wanne, wakiwa watumishi wa umma walitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti na kuisababishia serikali hasara ya Sh 104,158,536,146.

"Kwa pamoja na kwa makusudi na kwa kushindwa kuchukua tahadhari au kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa njia inayoeleweka, waliandaa bila ya kuwa na sababu nyongeza katika mkataba wa mwaka 2001 wa gharama za juu zaidi katika uchapishaji noti kuliko ilivyokuwa kwenye mkataba mkuu na hivyo kuisababishia serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania hasara ya Sh104,158,536,146, " alidai Lincon.

Lincon aliendelea kuieleza mahakama kuwa mwaka 2004 washtakiwa Jengo na Mkango, wakiwa ndani ya jiji na mkoa wa Dar es Salaam na wakiwa wameajiriwa katika utumishi wa umma katika nyadhifa tofauti BoT, kwa pamoja na kwa makusudi, wakiwa na ufahamu na nia ya kupotosha ukweli.

Alidai kuwa watu hao kwa pamoja walifanya mahesabu ya bei kabla ya ofa iliyotolewa na msambazaji wa noti katika nyongeza ya nyaraka za mkataba wa mwaka 2004 kwa kurejea bei iliyokuwepo kwenye mkataba wa mwaka 2001 na kuituma idara ya sheria kwa ajili ya kuangaliwa upya, kitu ambacho kwa ufahamu wao kililenga kumpotosha mkuu wao.

Aidha Lincon alidai kuwa mwaka 2005, Jengo akiwa ndani ya mkoa wa Dar es Salaam na mfanyakazi wa BoT katika wadhifa wa mkurugenzi wa huduma za benki, alimpotosha mkuu wake kwa kuomba kuchapwa kiasi kikubwa cha noti za benki katika mkataba wa nyongeza wa 2005, ikilinganishwa na mkataba uliotengenezwa na kitengo cha mtumiaji, akijua anafanya hivyo kwa lengo la kumdanganya mkuu wake.

Wakili wa upande wa utetezi, Mpale Mpoki alidai baada ya kusomewa mashtaka hayo kuwa kesi hiyo imefunguliwa mahakamani hapo kimakosa kwa kuwa mahakama ya wilaya, haina mamlaka ya kisheria kusikiliza kesi kubwa kama hiyo.

Alisema kwa vile washitakiwa wote wanne wanadaiwa kuwa walifanya makosa hayo wakiwa watumishi wa BoT na hawakufanya hivyo kwa nia mbaya, sheria ya kuanzishwa kwa benki hiyo inawapa kinga ya kutoshtakiwa.

Alidai kuwa kifungu namba 65 cha sheria ya ya BoT, kinawalinda maofisa wake kushtakiwa na kwamba kama kutatokea mkanganyiko wa kisheria, kifungu cha 68 cha sheria hiyo, bado kinawalinda.

"Mheshimiwa hakimu sheria hii ya BoT iliyotungwa na wataalamu, kifungu cha 68 kinasema kama kutatokea mkanganyiko wa kisheria, basi sheria ya BoT inapaswa kufuatwa na kuachwa sheria nyingine," alisema Mpoki.

"Kifungu cha 65 cha sheria ya kuanzishwa kwa Benki Kuu kinasema: bila ya kujali sheria nyingine zote isipokuwa katiba ya nchi, sheria ya BoT ifuatwe iwapo kutatokea mkanganyiko wa sheria. Hivyo basi kesi hii iliyoletwa chini ya kifungu cha 29, haiondoi kinga ya wateja wetu."

Hoja ya wakili Mpoki iliungwa mkono na wakili mwenzake wa utetezi, Mabere Marando ambaye alimwomba hakimu kuwaachia huru wateja wao kwa sababu hawana kesi.

Alisema washtakiwa hao hawana kesi kwa kuwa walikuwa na kinga ya utumishi wa BoT na kwamba hawakufanya hivyo kwa nia mbaya.

"... kwa hiyo mheshimiwa hakimu, mahakama yako haina mamlaka ya kisheria kusikiliza kesi hii na kwa mujibu wa sheria ya BoT, si kuisikiliza tu bali hata kuipokea kwake ni ukiukwaji mkubwa wa sheria," alisema Marando.

"Naiomba mahakama yako isome vizuri vifungu mbalimbali vya sheria na hatimaye inawe mikono na kuwaachia huru wateja wetu kwa kuwarudishia Takukuru kesi yao, ili watafute watu wengine wa kuwashitaki kwa sababu hawa hawahusiki kwa vile wote walikuwa watumishi wa BoT. Tunaomba warudi wakaendelee na utumishi wao."

Akijibu hoja hizo, Hakimu Maweda alipinga hoja ya watuhumiwa hao kuachiwa huru na kusema kesi hiyo imepokelewa mahakamani hapo kwa ajili ya maandalizi ya kuipeleka Mahakama Kuu baada ya kukamilika kwa upelelezi.

Awali mwendesha mashitaka huyo wa Takukuru alidai kesi hiyo imefunguliwa kwa kifungu namba 29 cha sheria ya uhujumu uchumi kinachotoa fursa kesi zote za uhujumu uchumi kuanzia mahakama za wilaya kabla ya mahakama za ngazi ya juu zaidi.

"Sheria inaturuhusu kuanzia mahakama ya wilaya na baada ya upelelezi kukamilika kesi hii itahamishiwa katika mahakama za ngazi ya juu zaidi zenye uwezo wa kusikilzia kesi za uhujumu uchumi," alifafanua Lincon.

Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo na kurudishwa rumande hadi Septemba 18 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

Source: Gazeti la Mwananchi
 
Wote wawili cheo kimoja? Au ilikuwa kwa nyakati tofauti?

Amandla....

Ukisoma habari ya kwenye gazeti hapo juu, makosa hayo yamefanyika kati ya mwaka 2001 mpaka 2005. Kwa hiyo hao wahusika wawili walikuwa kwenye hizo nyadhifa kwa nyakati tofauti.

Huyo Ali Bakari alishastaafu kazi siku nyingi, tuko nae mtaani na wakati anastaafu alikuwa Mkurugenzi wa Tawi la BoT Arusha.
 
yetu macho na masikio tu.........hivi kesi ya zombe iliishaje?........mmh!!!
 
Hapa ndipo Ze Comedy ya PCCB inapojionyesha wazi wazi. Nina maswali machache ambayo ninajiuliza sana na sipati majibu.

Kwanza, hivi hao watumishi wa BoT wanaweza kuingia mikataba sensitive ya kuchapisha noti bila ridhaa ya Gavana na Bodi ya Wakurugenzi?

Pili, process nzima ya kumpata mchapa noti lazima ihusishe tenda (zabuni) na wachapaji hutoa gharama zao, je, ilikuwaje hao jamaa wakaongeza bei ya mkataba wa awali na malipo yakafanyika bila ya Gavana/Naibu Gavana na Bodi ya wakurugenzi kujua? Kama ingekuwa ni hasara ya few millions, ingeweza kueleweka kwamba may be kuna gharama nyingine zinaweza kuwa incurred bila Gavana ama Bodi yake kujulishwa na malipo yakafanyika, lakini bilioni 104 ni nyingi sana lazima Gavana na Bodi yake ilihusika na wali approve. Je, Bodi na Gavana walihusika vipi kwenye hiyo hasara ya bilioni 104?

Tatu, kwanini hizi kesi zinazohusu BoT zimesubiri kwanza Ballali afariki ndipo wakazipeleka mahakamani? Kuna kitu kinafichwa some where ama malengo ni nini?

Nne, mikataba mibovu na nyongeza za ajabu ajabu za kwenye mikataba ya awali inagusa kashfa nyingi, mfano TICTS. Je, PCCB wameishachunguza kwanini TICTS aliongezewa miaka 15 kabla ya kumaliza kipindi cha awali cha miaka 10? Je, walioshiriki kwenye nyongeza ya mkataba wa TICTS siyo wahujumu uchumi? Je, kesi ya akina Mramba, Yona na Mgonja, haihusiani na uhujumu wa uchumi? Je, definition ya uhujumu uchumi ni nini? Je, kutuingiza kwenye mkenge wa Richmond, siyo uhujumu uchumi?

Mwisho, sheria ya BoT ilifanyiwa marekebisho nadhani mwaka 2006 au 2007, na ninaona mawakili wametumia sheria ya BoT ili kutetea wateja wao kwamba walifanya makosa hayo wakiwa watumishi wa BoT na hivyo hawatakiwi kushitakiwa na kwamba sheria yoyote ikipingana na na sheria ya BoT basi, sheria ya BoT inatakiwa kufuatwa, huu siyo uhuni wa kutumia vibaya hizi sheria zinazotungwa ili kuwalinda watu? Je, utawala wa Ballali uliyajua yote haya na kuamua kujiwekea kinga mapema kabla ya kufikishwa kwa pilato?
 
Haya mambo yalifanyika siku nyingi sana lakini watawala wa wakati huo na wa sasa pia kwa njia moja ama nyingine walikuwa wanajua na walineemeka kwa mambo hayo pia. Kubwa la kujiuliza inakuwaje wanashughulika na kada ya chini ambayo aidha kwa shinikizo ama kwa kutojua kwamba mambo yaliyofanyika kwa wakati huo yalikuwa ni kuvundika uchafu ambao unapoanza kunuka aliye karibu ndiye anakuwa mnukaji wa kwanza bila kujali ama kuangalia mvundikaji wa uchafu huo ni nani na yuko wapi kwa wakati huo.

Waliovundika uchafu huo kwa wakati huo hawatajwi kwa sasa, (BALALI and the others), wanaotafuta wanukaji yawezekana ndiyo waliofanya uvundikaji huo, (HOSEA and the others), kwa utaratibu huo tutafika panapotakiwa?, siku Mungu akiamua kushusha gharika ni nani atapona katika uovu huo? Kaisari wetu atakuwa na utetezi gani katika uovu huo ambao ni wazi anaujua na pengine alishiriki katika kutengeneza uvundo unaosikika kwa sasa?
 
KUna taarifa rasmi kwamba kuna mtumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa. Taarifa zaidi baadaye.

Tumesha choka na maporojo hakuna lolote linalofanyika katika mahakama za nchi hii ni mazingaumbwe wanafanyiwa Watanzania kutokana na akili zao kuwa ziko na uvivu wa kufikria kwa upeo wa mbali.kwa mfano mwengine kama vile akili za kuku ukimfukuza sasa hivi asile mpunga wako baada ya sec 2 atarudi na kuamini alifukuwa mwaka juzi.
 
vigogo wanne wa BOT wametinga kortini (mahakama ya wilaya ya ilala) kwa wizi wa bilioni 104 pamoja na kuchapisha noti nyingi bila ya kufuata utaratibu kwenye mikataba ya uchapishaji wa noti hizo. watu hao ni Bosco, ally, kisimo

haya jamani yale aliyoahidi JK ndio yanaanza kuonekana na kutekelezeka au ni kuwafurahisha wananchi na kuwafumba macho kwa ajili ya kuelekea uchaguzi 2010?

soma magazeti ya leo
 
Back
Top Bottom