Vigogo watatu Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima wang'olewa

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
Niko Wizara ya Elimu, Mkurugenzi wa Elimu wa wizara hiyo, Profesa Eustella Bilalusesa anamuagiza Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima, Fidelis Mafuniko, kuwatimua kazi Wakufunzi Wakazi (Resident Tutors) watatu kwa uzembe, kukiuka taratibu na kuwadanganya wananchi kuhusu uteuzi wa wanafunzi wanaopaswa kujiunga na elimu ya sekondari katika vituo vya Elimu ya Watu Wazima.

Wakufunzi hao ni Otugu Muganda wa Dar, Senorina Katende wa Dodoma na Stewart Ndandu wa Mwanza na Geita.

Taarifa kamili zitawajia kupitia FIKRA PEVU
 
Hivi hii taasisi na ile MEMKWA vina uhusiano? au hii taasisi ipo kwenye maandishi zaidi? nilipo kuwa mdogo nilikuwa nikiona watu wazima wakisoma lakini miaka ya karibuni sijaona kitu kama hicho. Je tunaihitaji hii taasisi kweli kwa nyakati hizi?
 
Mimi nilidhani watapongezwa kwa ubunifu wao kumbe ni kinyume chake. Mbona maelezo yao yapo clear.
 
kuna uzi jana niliona umeandikwa kesho zamu ya akinanani kutumbuliwa naona ndo hawa. Namim inauliza tena kesho itakua zamu ya akinanani angalia usiwe wewe unaesoma comment hii
 
Niko Wizara ya Elimu, Mkurugenzi wa Elimu wa wizara hiyo, Profesa Eustella Bilalusesa anamuagiza Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima, Fidelis Mafuniko, kuwatimua kazi Wakufunzi Wakazi (Resident Tutors) watatu kwa uzembe, kukiuka taratibu na kuwadanganya wananchi kuhusu uteuzi wa wanafunzi wanaopaswa kujiunga na elimu ya sekondari katika vituo vya Elimu ya Watu Wazima.

Wakufunzi hao ni Otugu Muganda wa Dar, Senorina Katende wa Dodoma na Stewart Ndandu wa Mwanza na Geita.

Taarifa kamili zitawajia kupitia FIKRA PEVU

Balalusesa ni kamishna Wa elimu si mkurugenzi...
 
kwanini hii taasisi isifutwe ? maana kuna ongezeko kubwa sana la wasiojua kusoma na kuandika , ile elimu ya Ngumbalo wamepeleka wapi ?
 
hivi watu wazima ni akina nani hao?
unawafahamu wazee wa Dar es salaam , wale walioongea na Magufuli juzi ? 90% hawajui kusoma wala kuandika na kuna uvumi kwamba kuanzishwa kwa taasisi hii kuliwalenga hawa .
 
1.jpg


Kamishna wa Elimu Awavua Madaraka Wakuu Watatu wa Vituo vya Elimu ya Watu Wazima Dar, Dodoma na Mwanza

Kamishna wa Elimu, Teknolojia, Sayansi na Ufundi, Profesa Eustella Balamsesa amemuagiza Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima, Fedelis Mafumiko kuwavua madaraka Wakuu Watatu (3) wa vituo vya Elimu ya Watu Wazima kutokana na kukiuka utaratibu wa kuchagua wanafunzi wanaojiunga kidato cha kwanza kuwaingiza katika Mfumo wa Elimu ya Watu Wazima.

Profesa Eustella ameyasema hayo leo wakati alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam .
Amesema kuwa wakufunzi hao wamekuwa wakishirikiana na Halmashauri baada ya kuchagua wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao wamefanya vizuri wao huchukua wanafunzi waliofeli na kuwapeleka katika shule za serikali wakidai kuwa wanafunzi wamechaguliwa katika chaguo la pili.

Baada ya kuchaguliwa wanafunzi hao wakifika shule wanadaiwa ada wakati serikali imesema elimu ni bure, hali inayowachanganya wazazi.

Wakuu wa vituo waliovuliwa madaraka ni Wotugu Mganda (Dar es Salaam), Senorina Kateule (Dodoma),Steward Ndandu Geita na (Mwanza).

Profesa Eustella amesema kuwa wakufunzi hao wamekuwa wakidandia matokeo ya kidato cha kwanza kwa kufanya upotoshaji kwa wazazi wakati wanafunzi wanaosoma katika elimu ya watu wazima ni hiari kutokana na sera ya elimu.

Wanafunzi ambao wamechaguliwa kwa mwaka huu wamekuwa wakidai ada ya sh. 80,000 hadi 250,000 na ndipo malalamiko yakaanza kwa wazazi baada ya kudaiwa ada hiyo.

Profesa Eustella, amesema kuwa mmoja wanafunzi katika Mkoa wa Dar es Salaam aliambiwa amefaulu katika chaguo la pili katika shule ya sekondari ya Oasterbay .Baada ya kufika shuleni, mwanafunzi huyo alikuta mambo tofauti kwa kudaiwa ada na kuambiwa awasiliane na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.
 
Kweli serikaliniii sasa hakuna security.....wakubwa wanatafuta sifa za kijinga kila kukicha
 
Back
Top Bottom