Vigogo wapya wahojiwa kashfa ya UDA: Wamo KIMBISA, DK MASSABURI NA IDD SIMBA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo wapya wahojiwa kashfa ya UDA: Wamo KIMBISA, DK MASSABURI NA IDD SIMBA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Patriote, Jan 12, 2012.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160

  SAKATA la uuzaji wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), limezidi kupamba moto baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Utouh, kuwataja vigogo wapya waliohojiwa na shirika lake kutokana na kutajwa kwamba walishiriki katika mchakato wa uuzaji wa hisa za shirika hilo.Akizungumza na Mwananchi jana, Utouh aliwataja vigogo hao ambao alisema baadhi wameshahojiwa kuwa ni Mwenyekiti wa Bodi, Idd Simba na Mkurugenzi wa Kampuni ya Simon Group, Robert Kisena.
  Vigogo wengine ambao Utouh alisema wanatarajiwa kuhojiwa wakati wowote ni Meya wa jiji la Dar es Salaam Dk Didas Masaburi na mtangulizi wake, Adam Kimbisa pamoja na Meneja Mkuu wa UDA, Victor Milanzi.

  "Sisi hatufanyi kazi kisiasa, tunafuata sheria na taratibu zote zinazotakiwa katika kufuatilia suala hilo. Hivyo basi, lazima tuwe makini kwa kujiridhisha na taarifa inayotolewa," alisema CAG.Utouh alisema ili ripoti hiyo iweze kukamilika na kuondoa hofu ya kumwonea mtu, wahusika wote waliotajwa kwenye sakata hilo wanapaswa kuhojiwa.

  Agosti 13 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) Keptein mstaafu George Mkuchika, alitekeleza agizo la waziri mkuu na kumpa CAG barua ya kufanya ukaguzi wa UDA ndani ya mwezi, lakini sasa ni zaidi ya miezi minne matokeo hayajatoka. Hata hivyo, CAG Utouh akizungumzia sababu za kuchelewa kwa uchunguzi huo aliema; "Tulitaka kutoa nafasi kwa watuhumiwa kupata fursa ya kujitetea." Utouh alifafanua kwamba, lengo hilo la kutenda haki ndilo lililofanya ofisi yake kuwahoji wahusika wote waliotajwa kushiriki kwenye mchakato huo ili ripoti itakayotoka isiwe ya kumwonea mtu.

  Aliongeza kwamba kutokana na hali hiyo, wanaamini kuwa kukamilika kwa ripoti hiyo, kutaisaidia serikali kutoa uamuzi sahihi kuhusu sakata hilo na kuwaachia wale ambao wanaweza kuingizwa kwa makusudi kutokana na tofauti zao za kisiasa. Utouh alifafanua kwamba, hadi jana Kampuni ya KPMG iliyopewa jukumu la kufanya ukaguzi huo, ilikuwa ikikamilisha ripoti yake ambayo, wanaamini inaweza kutolewa mwishoni mwa mwezi huu na kuikabidhi serikalini kwa ajili ya hatua zaidi.

  Sakata lilivyokuwa

  Serikali ilibaini kuwepo kwa ukiukwaji wa kisheria katika uuzaji wa UDA Agosti mwaka jana, jambo ambalo lilisababisha kuundwa kwa tume ya uchunguzi. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliagiza kuunda tume ya kuchunguza sakata hilo huku akizitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na CAG, kuchunguza mchakato mzima wa uuzaji wa hisa za shirika hilo kwa kampuni hiyo ya Simon Group Limited.

  Habari ambazo Mwananchi limezipata zinadai kuwa tayari Takukuru pia walishawahoji baadhi ya watu kuhusu suala hilo. UDA lilikuwa linamilikiwa kwa pamoja kati ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Serikali Kuu, kupitia Hazina, wakiwa na jumla ya hisa milioni 15, kila hisa moja ikiwa na thamani ya Sh 100. 

Mchanganuo wa hisa za UDA unaonyesha kuwa, halmashauri ya jiji la Dares Salaam ilikuwa inamiliki asilimia 51 na Hazina asilimia 49 za hisa hizo.   Hata hivyo, Februari 11 mwaka jana, bodi ya wakurugenzi ya UDA, chini ya Idd Simba, ilikutana na uongozi wa Simon Group ikiongozwa na Kisena na kusaini mkataba, ambao ulithibitisha kwamba UDA ilikuwa imeiuzia Simon hisa milioni 7.8 sawa na asilimia 52.6 ya hisa zote kwa thamani ya Sh bilioni 1.142. Kwa mkataba huo, Simon Group ingekuwa mwanahisa mkubwa katika umiliki wa UDA kwa vile Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Hazina, wangebaki na hisa milioni 7.7, ambazo ni sawa na asilimia 47.4.


  Baada ya mkataba kusainiwa, kipengele cha kwanza kiliitaka Simon Group kulipa asilimia 25 ya fedha za ununuzi wa hisa za UDA , ambazo kati ya fedha jumla Sh bilioni 1.142, ni sawa na kutanguliza Sh 285.6 milioni. Fedha hizo zilipaswa kulipwa ndani ya siku 14, tangu kusainiwa mkataba huo ili kuufanya utambulike kisheria na ndipo, Simon Group ililipa fedha hizo siku hiyo hiyo.

  Ndani ya Bunge


  Uuzwaji wa UDA ulitikisa Mkutano wa nne wa bunge baada ya wabunge kutaka hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika, huku wabunge wa mkoa wa Dares Salaam wakijikuta katika malumbano na Dk Masaburi.Wakati mvutano huo ukiendelea, wamiliki wa Simon Group Ltd, walijitokeza hadharani na kuwaambia waandishi wa habari kwamba umiliki wake umekidhi vigezo vyote katika kumiliki Hisa ndani ya UDA.

  Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Simon Group, Robert Kisena alisema kampuni yake ilifuata vigezo vyote vilivyotakiwa na kwamba imejizatiti kuliendesha Uda bila wasiwasi na kwamba hadi wakati huo walikwishawekeza kiasi cha Sh760 milioni. Hata hivyo, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) kupitia kwa Mwenyekiti wake, Zitto Kabwe nayo ilisema kuwa mkataba huo ni batili kutokana na fedha zilizonunua hisa husika kuwekwa kwenye akaunti ya kada wa Chama Cha Mapinduzi na mwanasiasa wa siku nyingi, Iddi Simba.

  "Taratibu hazikufuatwa,na uamuzi wowote utakaofanyika ni batili kwa kuwa tayari sisi tumeshaanza mchakato wa kubaini kilichopo ndani ya mkataba huo ikiwa ni pamoja kumuagiza CAG na tayari Spika ana taarifa hizo,''alisema Zitto.

  Source: Mwananchi 12/01/2012

  Maoni yangu

  Kwa takwimu hizi kama ni sahihi, inaonyesha UDA ili nunuliwa kwa Tsh
  285.6 milioni in cash na kiasi kilichobakia katika 1.142 Bilioni kilikuwa ni kauli a.k.a longo longo. Ikumbukwe kuwa kiasi hicho kinausisha rasilimali zote za UDA. Kimsingi UDA ilitolewa bure maana kiasi hicho ni kiwanja kisichozidi heka Mbili Oysterbay na maeneo mengine ya ufukweni DSM tena bila mjengo.

  Ikumbukwe pia kuwa hawa wanunuzi wa kampuni ya UDA, SGL ndiyo wale wale walioshindwa kurejesha mkopo wa 5 Bilions katika bank inayoendeshwa kwa kodi zetu TIB chini ya mwana EPA aliyewekwa pale na kiongozi wa nchi kulinda na kutetea maslah ya watu wake.

  Ukilichinguza kwa makini sakata hili utaona wezi wetu siku zote ni wale wale, tena inaonyesha sio wengi mana kila tukiibiwa tunakuta ni hao hao wanahusika. Hivi nani katuroga tunashindwa kudeal na watu hawa???Mbona vyombo vya usalama vinajifanya havielewi kinachoendelea??hivi watu hawa c ndio wenzetu wa China wanawanyonga hadharan???Mi nadhani katika Katiba mpya suala la kudeal na mafisadi litazamwe kwa mapana na marefu yake. Kwa nn uharamia/ujasusi wanaofanyiwa watu wema wasifanyiwe watu hawa?? Kwa nini hadi leo wahusika wanaingia kwenye ofisi za Umma na kuendelea na kazi ili hali wanatuhumiwa???Wao hawawezi kuvuruga ushahidi?????kwanini wasisimamishwe kama ilivyokuwa kwa Jairo na wengineo wakati uchunguzi unaendelea??????

  Hivi katika Katiba yetu hakuna utaratibu tunaoweza kuutumia kuiondoa hii serekali madarakani?? Hivi wananchi tunaosifiwa kuwa ndio wenye mali na nchi hatuwezi kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali hii legelege na babaishaji iliyopo madarakani?? Hebu wataalam washeria mtupe muongozo katika hili. Hivi hakuna utaratibu wa kuitoa Serikali madarakani kihalali hadi tutumie njia za wa Misri na wa Libya???Mbona ni kama kila kiongozi ni mwizi tu????

  Je Serikali inataka tumwamini nani?? Wizi Ikulu (MaEPA, Kiwira etc), wizi kwenye nishati na madini (MaRichmond na Jairo's Stimulus Package), Wizi bungeni (via double payments za sitting allowance), Wizi makanisani, Wizi local governments (Miradi ya maendeleo), Wizi kwenye maNGOs,wizi maliasili (Twiga wetu KIA, Vitalu, Viwanja vya mahoteli mbugani e.t.c), Wizi miundombinu (Miradi ya barabara, Radar e.t.c), Wizi wzr ya ulinzi (Via Meremeta), Wizi wizara ya Fedha (MaEPA, Stilumus Package ya JK etc), list ni ndefu nimechoka, kimsingi niseme tu kuwa ni wiiiiiiiiiiiiiiiiiziiiiiiiii mtupu, wiziiii. Itoshe tu kusema kuwa tuliowaamini na kuwachagua watuongoze ni wezi!!! Sasa nini kifanyike????

   
 2. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Huyu jamaa bado hajafukuzwa kazi, Ludovick Utouh! hii ndiyo Tanzania kweli. Hakuna mwingine anayeweza hiyo kazi au akiingia mwingine ataharibu mipango!
   
 3. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Utouh Mwenyewe naye ni mpotoshaji as per ripoti ya Bunge in Jairo's Kashfa, Utouh huyo huyo aliyepoteza sifa ya kufanya kazi kwenye utumishi wa umma anaendelea kukabidhiwa kazi nyingine tena za mazingira hayo hayo!!Hii nchi jamani!! Halafu tumetega masikio tunasubiria ripoti ya maana. We must be crazy!
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Utouh alikuwa wapi anakumbuka shuka kumekucha aliacha weledi akacheza siasa zikamtokea puani...sasa anajifanya anajirekebisha too late babu,,,,,,huna tena mvuto kwa jamii....heri ungemtuma msaidizi wako atoe taarifa ila wewe umeshaisha mvuto wako na hata imani nawe haipo tena
   
 5. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndio aina ya watendaji tuliokuwa nao, amepewa mwezi mmoja yeye anajipa miezi minne
  Bungeni alipewa hadidu za rejea kumchunguza Jairo, yeye akajipa hadidu za rejea anazozijua yeye.
  Huyu babu hafai kwenye ofisi kashapitwa na muda, sasa ngoja majibu yatoke.

  OFISI YA CAG BAHADA YA KUFANYA UCHUNGUZI YAGUNDUA HAKUNA UFISADI WOWOTE ULIOFANYIKA KATIKA KUBINAFSISHA UDA
   
Loading...