Vigogo waliopora ardhi kushtakiwa Z’bar


A

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2010
Messages
859
Points
0
A

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined Aug 31, 2010
859 0na Hassan Ali, Zanzibar


SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imetangaza mpango maalumu kwa vigogo na watendaji waliopora ardhi kuanza kunyang’anywa na kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa malengo ya kulinda na kutetea misingi ya utawala bora visiwani humo.
Mpango huo umetangazwa na msemaji mkuu wa serikali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohammed Aboud Mohammed, wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana.
Alisema kuwa kuna baadhi ya viongozi na watendaji Zanzibar wameingia katika kashfa ya kunyang’anya ardhi wananchi na kuuza kwa wawekezaji kitendo ambacho ni kinyume na sheria ya ardhi ya Zanzibar.
Waziri Aboud alisema serikali tayari imeanza kufanya uhakiki wa kuyatambua maeneo yote ya ardhi ambayo yamekumbwa na migogoro na kuwahusisha baadhi ya viongozi na watendaji ambao walipata kuwa na heshima kubwa Zanzibar.
Alisema serikali itawanyang’anya ardhi na kama watu waliouziwa wakiwa hawakuridhika, wana haki ya kufungua mashitaka dhidi ya viongozi waliohusika na kuwauzia ardhi hiyo kinyume na sheria.
“Hatuwezi kunyamaza kama serikali wakati watu wananyang’anywa ardhi na wengine ni viongozi wamenyang’anya wananchi,” alisema.
Alisema kwamba kwa mujibu wa sheria, ardhi ni mali ya serikali na mwekezaji hatakiwi kuuziwa ardhi bali anakodishwa, kwamba wawekezaji ambao wameuziwa ardhi watalazimika kunyang’anywa.
“Haiwezekani wakubwa kunyang’anya ardhi wadogo, kitendo hicho ni kinyume na misingi ya utawala wa sheria,” alisema.

 
mfianchi

mfianchi

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2009
Messages
9,014
Points
2,000
mfianchi

mfianchi

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2009
9,014 2,000
Mmm ngoja nijipitie nisje ambiwa nina akili ya samaki
 
Globu

Globu

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2011
Messages
8,107
Points
1,500
Globu

Globu

JF-Expert Member
Joined Jan 12, 2011
8,107 1,500
Wanafik tu hao, wote wezi. Hakuna wa kumnyooshea mwenziwe kidole.
 
124 Ali

124 Ali

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2010
Messages
6,978
Points
2,000
124 Ali

124 Ali

JF-Expert Member
Joined Apr 25, 2010
6,978 2,000
Mwanzo mzuri wa kujitawala! In Sha Allah(I.S.A)!
 

Forum statistics

Threads 1,285,938
Members 494,834
Posts 30,879,769
Top