Vigogo wa siasa Tanzania

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
8,357
2,000
Kutokuwepo Hayati Magufuli, ambaye aina ya siasa aliyoiendesha (Utashi wa Kisiasa, Uthubutu wa maamuzi magumu na kuyatekeleza, Usimamizi wa rasmali za nchi, nk) kumejitokeza uhalisia wa aina ya wanasiasa nchini (majina yao mtajaza).

Kundi la kwanza: Wanasiasa wachumia tumbo. Hawa ni wale ambao muda wote wamekuwa wanahangaika kupata uongozi kwa gharama yoyote ile.

Kundi la Pili: Wanasiasa wapambe ambao kazi yao ni kuwapigia debe wa kundi la kwanza wakiamini mafanikio yao kiasasa ndio mtaji wao.

Kundi la tatu: Wanasiasa wajasiriamali ambao siasa ndio eneo la kuwekeza mtaji. Hawa kama wako madarakani watatumia nafasi hiyo kujijenga kiuchumi.

Kundi la nne: Wanasiasa ambao hawajui kuwa hawajui. Kwa hawa wameingia kwenye siasa kwa mkumbo bila malengo. Hufanya siasa kama michezo ya kubahatisha.

Kundi la sita: Wanasiasa wapotoshaji. Hawa ni mabingwa wa kuandaa na kutoa taarifa zenye kuichanganya jamii kwa lengo la kuvuruga Serikali iliyoko madarakani. Baadhi wamedaiwa kuwa wawakilishi maslahi ya kundi katika jamii, ndani au nje ya nchi. Hawajali lolote na hudharau kila mtu. Hawa hujifanya kujua kila kitu.

Kundi la saba: Wanasiasa 'Waaminifu':
Kwa kawaida hufanya kazi zao kwa moyo wa dhati na hupanda vyeo kwa sababu ya kuwajibika na kuaminika. Hawa ni wanasiasa ambao hawapendi longolongo na huwa makini sana kwa kauli na matendo yao.

Hivyo basi malumbano yanayoendelea nchini kwenye vyombo vya habari, mitaani na hasa mitandao ya jamii, ikiwamo Bungeni, kuhusu "legacy" ya hayati Magufuli, yanawapambanua aina ya wanasiasa nchini. Katika mazingira haya, ni dhahiri amani ya nchi iko kwenye mtihani mkubwa kwani kila mwanasiasa sasa ni kambare.
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
52,553
2,000
1618676212543.png
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom