Waziri2025
Senior Member
- Sep 2, 2019
- 149
- 380
Askari Polisi Watatu akiwemo Mkuu wa Kituo cha Polisi Engutoto Jijini Arusha, Mkaguzi Msaidizi Mahamud Jakaya wameswekwa rumande katika Kituo Kikuu cha Polisi Arusha kwa kosa la kupora shilingi milioni 3 za Mfanyabiashara wa Mazao kutoka Mkoani Dodoma, Ramadhani Hamisi.
Inadaiwa kuwa mfanyabiashara huyo aligoma kutoa rushwa ya shilingi milioni 10 kwa kosa la kujihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya aina ya Mirungi.
Askari wengine walioko lokapu hadi sasa ni pamoja na Mkaguzi Msaidizi, Ramadhani Mcheka na Mkaguzi Msaidizi aliyetambulika kwa jina moja la Machanganya ambao ni askari viongozi wa Kitengo cha Polisi Jamii katika Wilaya ya Arusha.
Habari kutoka vyanzo vya Habari ndani ya jeshi hilo na eneo la tukio, zilisema kuwa Askari hao walifanya tukio hilo Agosti 25, 2022 majira ya saa 4 usiku eneo la kwa Morombo ndani ya Jiji la Arusha baada ya kumkamataa mfanyabiashara Hamisi kwa tuhuma za kujihushisha na utumiaji wa Mirungi.
Habari zilisema kuwa kuwa baada ya Mfanyabiashara Hamisi Kukamatwa akiwa na ndugu zake wanne akiwemo dereva, Nassibu Ngoyana wakiwa katika gari aina ya Fuso ambalo namba zake za Usajili hazijajulikana askari hao waliwashusha katika gari hilo na kufanya upekuzi katika Fuso iliyoshusha mazao jioni ya siku hiyo katika mzani wa Kwa Mrombo. Hata hivyo hawakukuta kitu chochote katika upekuzi wao.
Vyanzo vya habari viliendelea kusema kuwa baada ya kupekuwa na kutokuta kitu katika Fuso hiyo Askari hao wawili Jakaya na Mcheka walimwamuru Mfanyabiashara Hamisi kutelemka na begi lake na kuingizwa katika gari ndogo aina ya Porter iliyokuwa ikiendeshwa na Mahamudu na kudai wanawapeleka katika kituo cha Polisi Muriet kwa mahojiano zaidi.
Habari zilidai baada ya kutaka kuelekea Kituo cha polisi Muriet ghafla alijitokeza askari Machanganya akiwa na usafiri wa pikipiki na kuongoza msafara huo hadi Kituo cha Polisi Muriet lakini hawakuingia ndani baada ya askari wa pikipiki kuingia Kaunta ya Polisi Muriet na kudai kuwa hapo sio pazuri kwa kuwa kesi hiyo ni kubwa anapaswa kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi Arusha.
Vyanzo vilisema msafara ukiongozwa na pikipiki ya Mkaguzi Msaidizi Machanganya ulielekea katika Kituo Kikuu cha Polisi Arusha njiani askari Jakaya na Mcheka walimwamuru Mfanyabiashara Hamis kutoa rushwa ya shilingi milioni 10 kwa kuwa kesi inayomkabili inaweza kumpoteza gerezani hatua ambayo mfanyabiashara huyo alipinga na kudai kuwa hajawahi kutumia wala kuuza Mirungi hivyo hawezi kutoa kiasi hicho cha pesa labda yake alidai atatoa shilingi 300,000 kuepusha usumbufu.
Habari ziliendelea kusema kuwa Askari hao hawakuridhika na kauli hiyo na kuamua kupekuwa begi la Mfanyabiashara Hamis na kukuta shilingi 7,100,000 na kuchukua kibabe kiasi cha shilingi 30,000 ili waweke mafuta kwenye gari yao iliyokuwa ikiendeshwa na Askari Mahamudu bila ridhaa ya Mfanyabiashara huyo.
Vyanzo vilisema kuwa baada ya kufika Kituo Kikuu cha Polisi Arusha majira ya saa 5 usiku waliingia Kituo hapo na mtuhumiwa alifungiwa katika gari yao huku akilindwa na askari wa pikipiki na waliingia kituoni hapo na baada ya muda mfupi walitoka na kwenda katika gari na kuondoka naye kusikojulikana.
Habari zilisema kuwa baada ya kutoka kituo Kikuu cha Polisi Arusha askari waliongoza njia ya Majengo na wakiwa njiani askari hao waliamua kuchota pesa katika begi la Mfanyabiashara Hamis kiasi cha shilingi milioni 3 na kumuamuru kutosema kwa mtu yoyote na kumtaka kuondoka Jijini Arusha kurudi kwao Dodoma haraka iwezekanavyo vinginevyo watamfanya mbaya na kusindikizwa hadi nje ya Jiji la Arusha kwa kulazimishwa kuondoka.
Vyanzo vilisema askari Jakaya na Mcheka walimwomba Mfanyabiashara Hamis kuwa atakapokuja askari mwenzao Machanganya aseme kuwa ametoa shilingi milioni moja tu na sio vinginevyo ili waweze kugawana kiasi hicho na sio shilingi milioni 3.
Habari zilidai kuwa baada ya Mfanyabiashara Hamis kuachwa nje ya Jiji la Arusha aliamua kuwasiliana na mjomba wake askari wa Kituo cha Polisi Arusha aliyatembuliwa kwa jina moja la Salehe na kumweleza mkasa mzima na askari huyo alimfuata alipo na kumchukua hadi kwa ndugu zake majengo.
Vyanzo vilisema askari Salehe alifanya kila jitihada kuhakikisha askari wenzake wanarudisha pesa lakini juhudi hizo ziligonga mwamba kwa kuwa askari hao waligoma kuhusika katika tukio hilo wala hawakuhusika katika uporaji wa fedha hizo.
Baada ya hali hiyo inadaiwa kuwa askari Salehe aliamuru kulifikisha suala hilo kwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Arusha (OC CID) na Afisa huyo aliwaita askari hao na watuhumiwa waliwatambua askari Jakaya na Mcheka kuwa ndio wao waliopora kiasi hicho cha pesa na aliomba arudishiwe pesa yake kwa kuwa hahitaji kesi.
Hata hivyo habari za ndani ya Jeshi la Polisi zinasema kuwa askari hao mbele ya raia waligoma kuchukua pesa lakini katika vikao vyao vya ndani vya kikazi kilichohusisha maofisa wa Polisi Wilaya wakiongozwa na Mkuu wa Polisi Arusha (OCD) walikiri kupora pesa hizo na waliomba kurudisha shilingi milioni 1.5 hatua iliyopingwa na Mfanyabiashara Hamis.
Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Justine Msejo alipopigiwa simu yake ya kiganjani kuelezea tukio hilo alisema kuwa hana taarifa rasmi na alipobanwa zaidi alidai kuwa yuko katika kikao hawezi kuzungumza na alikata simu na alipotafutwa tena hakupokea simu.
Naye Mfanyabiashara Hamis alipotafutwa na gazeti hili alikiri kuchukuliwa pesa zake shilingi milioni 3,030,000 bila ridhaa kwani awali askari hao waliomba rushwa ya shilingi milioni 10 ili waweze kumwachia kwa makosa ya kujihushisha na utumiaji wa madawa ya kulevya aina ya Mirungi hatua ambayo alidai sio kweli.
Alisema amekuwa akiitwa kila mara na askari wakubwa pale polisi wakitaka nimalize kesi hii kwa kupewa shilingi milioni 1.5 hatua ambayo amegoma kwani askari walichukua zaidi ya shilingi milioni 3 bila ridhaa yake hivyo alihitaji kiasi hicho ili aweze kuondoka jijini Arusha.