Kuna suala haliko sawa TARIME, walimu wamesimamia mitihani ya mock iliyoisha tarehe 24/08/2016 lakini hadi Sasa hawajalipwa hata shilingi moja.
Porojo zimekuwa nyingi, kila siku wakifuatilia wanapigwa porojo. Lengo mwalimu akijitoa kuhoji aonekane mchochezi? Wakijikusanya kuna halmashauri kudai stahiki zao wataitwa wachochezi?
Kwa taarifa tu hata wasahihishaji hawajalipwa hadi Leo licha ya kumaliza kazi hiyo tangu Ijumaa iliyopita.
Likizo tangu Juni 2016 hazijalipwa, walimu wameenda likizo wakarejea lakini hadi sasa hawajalipwa pesa zao. Kweli hapa morali ya kufanya kazi itapatikana? ELIMU bora itatimizwa?
Wadau wa ELIMU wasaidieni walimu TARIME hawatendewi haki kabisa.