Vigogo CCM wataka Bunge kufumuliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo CCM wataka Bunge kufumuliwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 17, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mwandishi Wetu

  Toleo la 239
  16 May 2012


  [​IMG]


  • Wapendekeza kuanzishwa Baraza la Seneti na Bunge lenye mfumo mpya
  • Kikwete apigia debe urais kuhojiwa mahakamani

  KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi iliyokutana mjini Dodoma mapema wiki hii imependekeza, pamoja na mambo mengine, kufumuliwa kwa muundo wa sasa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Raia Mwemalimeelezwa.

  Muundo wa sasa ni wa wabunge wa aina tatu: wa majimboni, vitimaalumu na wanaoteuliwa na Rais kwa mujibu wa madaraka yake ya kikatiba.

  Badala yake, yameibuliwa mapendekezo kwamba lianzishwe Baraza la Seneti ambalo litaundwa na wajumbe wa aina mbili; ya kwanza ikiwa ni ya marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wale wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar..


  Aina nyingine ya wajumbe wawe ni watakaopatikana kwa njia ya kuchaguliwa, wakiwa ni mjumbe mmoja kutoka kila mkoa.


  Kwa mujibu wa vyanzo vya uhakika vya gazeti hili vilivyoshiriki vikao vya majadiliano katika Kamati Kuu, mjini Dodoma mwanzoni mwa wiki hii, utaratibu huo wa kuanzishwa kwa Baraza la Seneti unalenga kuwatumia marais wastaafu kwa maslahi ya nchi.


  "Tunakoelekea tunaweza kuwa na marais wastaafu wengi iwe kutoka CCM au kutoka vyama vingine vya siasa kama vitaweza kuchaguliwa na wananchi kuingia Ikulu.

  Busara inaelekeza kwamba marais hawa wastaafu ni vizuri kuwatumia katika kushauri namna ya kuongoza nchi. Hii ndiyo mantiki kubwa ya kupendekeza kuwapo kwa Baraza la Seneti," kilieleza chanzo chetu cha habari.


  Nchi mbalimbali zimekuwa na mabaraza ya maseneta, ikiwamo Marekani, Uingereza na hata Sri-Lanka iliwahi kuwa na Baraza la Seneti. Uzoefu katika nchi hizo unaonyesha kuwa mara nyingi unapokuwapo mfumo wa Baraza la Seneti ni lazima kuwapo na Baraza la Wawakilishi (Bunge) ambalo wajumbe wake hupatikana kwa kuchaguliwa moja kwa moja na wananchi, tofauti na ilivyo kwa Baraza la Seneti.


  Katika baadhi ya nchi, Baraza la Seneti linaundwa na wakongwe na wabobezi katika masuala mbalimbali ya utawala na utumishi wa umma lakini pia wajumbe wengine huteuliwa kuingia kwenye Baraza hilo kutoka katika Bunge au Baraza la Wawakilishi.


  Nchini Uingereza, kwa mfano, Baraza la Wawakilishi limekuwa likitambulika kama House of Lords (Bunge la Mabwanyenye) na Bunge la kawaida ambalo wabunge wake huchaguliwa, limekuwa likiitwa House of Commons (Bunge la Makabwela). Marekani pia imekuwa na Baraza la Seneti, sambamba na Baraza la Wawakilishi.


  Tofauti ya vyombo hivyo ni kwamba, Baraza la Seneti linategemewa mno katika kutoa misimamo mizito inayokidhi maslahi ya umma kwa kuzingatia kigezo cha uzoefu wa wajumbe wake. Lakini Bunge au Baraza la Wawakilishi jukumu lake ni kuwasilisha maslahi ya wananchi moja kwa moja kutoka katika majimbo.


  Kamati Kuu ya CCM pia imependekeza kwamba Katiba mpya ya Jamhuri Muungano wa Tanzania itamke idadi ya wabunge au wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ili kufuta michakato wa kuanzishwa kwa majimbo mapya ya uchaguzi mara kwa mara bila hata baadhi ya majimbo kukidhi vigezo vilivyopata kuanishwa.


  Katika suala la vitimaalumu imependekezwa kuwa kila chama kipate wabunge wa vitimaalumu kwa kuzingatia asilimia ya majimbo ya uchaguzi waliyoshinda.


  Matokeo ya urais kuhojiwa kortini

  Katika kikao hicho, taarifa zaidi zinaeleza kuwa Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti CCM na ndiye aliyekuwa akiongoza vikao vya chama hicho, alikuwa mstari wa mbele kuwashawishi wajumbe kuridhia kwamba, Katiba mpya itambue na kuruhusu mchakato wa kuhoji matokeo ya kura za urais mahakamani.

  Azimio hilo pia linatajwa kupitishwa na Kamati Kuu na kusisitizwa kuwa ni lazima uwekwe muda maalumu kwa wanaotaka kuhoji matokeo ya urais mahakamani ili kesi husika ziweze kumalizwa na Mahakama katika muda mfupi


  Lakini kwa upande mwingine, gazeti hili limeelezwa kuwa yapo mambo ambayo Kamati Kuu imependekeza yaendelee kuwapo katika Katiba mpya kama yalivyo katika Katiba ya sasa, ikiwa ni pamoja na haki ya kupiga kura na kuwapo kwa mihula ya uongozi wa kuchaguliwa na kwamba, wananchi ndiyo waachwe waamue muhula uwe wa miaka mingapi.


  Kwa sasa muhula wa uongozi wa kuchaguliwa ni miaka mitano katika nchi nyingine mihula ya kukaa madarakani inapishana kati ya miaka mine hadi saba.


  Tume ya Maadili

  Kwa mujibu wa habari hizo, CCM kupitia Kamati Kuu yake imependekeza pia kwamba Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma itambuliwe katika Katiba mpya na kwamba ijengewe mifumo huru ya kufanya kazi bila woga.

  Kwa sasa tume hiyo imekuwa ikiripoti kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na imekuwa chini ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utawala Bora kama ilivyo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).


  Utaratibu wa sasa kwa muda mrefu umekuwa ukilalamikiwa kwamba hautoi fursa kwa tume kuwa huru katika kuwashughulikia viongozi wa umma wanaokiuka sheria ya maadili na wengine wamekuwa wakishinikiza kuwapo kwa uwazi wa kisheria katika utendaji kazi wa tume hiyo.


  Ni mapendekezo ya CCM

  Hata hivyo, hayo na mengine yanatajwa kuwa ni mapendekezo tu ya CCM kama taasisi na chama tawala na kwamba, hayazuii Watanzania kwa ujumla wao kuwa na maoni mengine tofauti.

  Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, CCM kinatarajiwa kuwaelimisha wanachama wake kuhusu masuala ya msingi wanayodhani ni muhimu kuwamo katika Katiba mpya ili kupata uungwaji mkono kutoka kwa umma na hatimaye masuala hayo yawe sehemu ya Katiba mpya.


  Kudhibiti mfumuko wa bei

  Katika hatua nyingie, jana Jumanne, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM-Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, aliwaeleza waandishi wa habari kuwa vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu vimeitaka Serikali kudhibiti mfumuko wa bei za bidhaa muhimu nchini, na hasa chakula.

  "Kutokana na kuwapo kwa hali ya kupanda mno kwa bei za bidhaa nchini ambako kunasababishwa na mambo mbalimbali, ikiwamo mavuno duni na kupanda kwa bei za nishati ya mafuta duniani, Halmashauri Kuu imeamua pamoja na Serikali kuendelea kuchukua hatua za muda mrefu na wa kati kukabiliana na tatizo hili, CCM inaiagiza Serikali kuchukua hatua za haraka za muda mfupi ikiwamo kuangalia upya baadhi ya kodi katika vyakula pamoja na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) katika sukari," alisema Nape naye katika mazungumzo yake hayo na waandishi wa habari mjini Dodoma.


   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwanini CCM ndio inayotoa na kupendekeza mabadiliko?

  Fedha Za kuwalipa na kuwatunza Maseneta zitatoka Wapi na watafanya nini kwa Serikali yetu?

  Kwanini wananchi wasipewe Uwezo wa kupiga kura kuamua hilo jambo? HOJA zote kama mfano seneta, mgombea binafsi
  Iwe kwenye kura 2015
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  May 17, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,337
  Likes Received: 19,507
  Trophy Points: 280
  ulaji ulaji huo
   
 4. M

  Molemo JF-Expert Member

  #4
  May 17, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Wanaandaa ulaji wa wastaafu wao.Kamwe wananchi hatutakubali upuuzi huu
   
 5. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Wanapata wapi ujasiri wa kuongelea mambo yanayohusu nchi nzima wakati sisi watanzania tumeikataa ccm. Waunde seneti ya chama chao na si ya nchi nzima kwani sisi tutatoa maoni ya muundo tunaoutaka wa bunge kupitia tume ya kurekebisha katiba.
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  May 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo wanataka marais wastaafu wawe kwenye seneta? Kama walikuwa wezi bado wapewe nafasi ya kuendelea kutunga sheria? Ulafi wa maradara wa ccm hauna mfano.

  Na kuhusu Uiengereza, House of Lords lina historia ndefu, wengi mle ni wa kurithi - yaani mtoto anarithi kiti cha baba yake. Hawachaguliwi kwa kura yoyote, its a job for life. Miaka hii ya karibuni ndio wamebadilisha sheria (nusunusu) na hivyo Prime Minister anaweza kuteuwa watu "anaoona wanafaa' ili wawe member mle. Hata hivyo nalo hili limeleta shida sana maana unakuta Prime Minister anateua marafiki.

  Kwa kifupi, malalamiko kuhusu mfumo wa House of Lords ni mengi mno, baadhi ya wanasiasa wameshajaribu kuondoa huo mfumo wa kurithi lakini Lords kwa ndio wenye nchi. CCM inabidi wakae chini ni kujifunza badala ya kurukia kila wanaloona.

  Na kuhusu Marekani, sikumbuki ni rais gani mstaafu anayekuwa kwenye active politics kama ilivyo kwetu na wakina Mkapa na Mwinyi?
   
 7. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #7
  May 17, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  Naona kama ccm wamevunja ile sheria iliyopitishwa kwa mbwembwe na wabunge wa ccm iliyompa ulaji mzee sinde.
  wamejadili bila kuwepo wenye tume.
  NATANGAZA RASMI SIITAMBUI KATIBA MTAKAYOIANDIKA. NAJIAANDAA KWA MCHAKATO WA KATIBA MPYA BAADA YA HII MNAYODANGANYANA KUIANDIKA.
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  May 17, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,075
  Trophy Points: 280
  ....Mfa maji haishi kutapatapa
   
 9. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Moja zuri ni kupunguza ukubwa wa Bunge. Yaani inatosha sana kuwa na mbunge 1 kila mkoa basi. Marais wakikaribishwa kama Washauri (bila kuwa na uwezo wa kupiga kura) sina sida na hilo, maana inabidi tuwatumie kupata sehemu ya hekima yao. Kama mtu alikuwa kiongozi mwizi na tuna ushahidi hakuna panapozuia kumfikisha mahakamani.
   
 10. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Bora lijadiliwe linaweza kuwa na mazuri yake
   
 11. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wazo la masenator ni zuri lakini sio lazima wawe marais wastaafu. Hao bora wapumzike tu au watumiwe na vyama vyao. Bora tukaweka wafanya biashara wenye mafanikio na wasomi wenye kiwango cha juu kuwa masenator
   
 12. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  si walisema marais wastaafu hawataingia kwenye vikao vyao vya wanga? mbona naona kama bichwa la mkapa linameremeta kwenye hiyo picha!
   
 13. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mtu ashauza ardhi kaimaliza, kauza viwanda kamaliza, kauza twiga........., kauza migodi!!!!! then anaingia kwenye seneti yao ili kutetea kile alichokiuza, unadhani nani atamsema mwenzie hapo kuwa kaharibu.
  Huu ni mpango wa JK kawatumia wajumbe wake kadhaa kawaelekeza waanzishe hiyo hoja ili aendelee kutetea alivyoviuza.
   
 14. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Hili la masenator limekaa kama la CDM ukiangalia vizuri!! hapa CCM wanataka kuibadili sera za CDM!! Serikali za majimbo (say kanda ya kusini, nyanda za juu, kanda ya ziwa, kanda ya kaskazini, kanda ya kati, kanda ya pwani na zanzibar)zitakuwa na viongozi wakuu ambao ukijumlisha na wale wa serikali kuu tayari una masenator ambao ni tofauti na wabunge.
   
 15. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Naona ccm wameona hawawezi kushinda tena urais hata kwa kuchakachua sasa wanaandaa utaratibu wa kuhoji mahakamani. Wakati walipokuwa na uhakika wa ushindi, hawakulitaka kabisa hili. Ni sawa na swala la mgombea binafsi. Wakati vyama vya upinzani vilipokuwa havijaimarika, walipinga kwa nguvu kubwa swala la mgombea binafsi. Sasa cdm imeimarika na wanajua wakimkataa mgombea aliyechagulia na wananchi kwenye vikao vya dodoma, atahamia cdm. Sasa wanajipanga kuruhusu mgombea binafsi ili asipojiunga cdm, wazigawe kura! Haya yote hayatawasaidia maana wapo nyuma sana kifikra! Yote hayo tunayaona mapema kuliko wao. Cdm walipozungumzia majimbo, wakasema ni wabaguzi, sasa wao wanaanza na wawakilishi wa mikoa na baadae watakuja na majimbo! Always late!
  Kweli la kuvunda halina ubani na mfamaji haishi kutapatapa!
   
 16. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #16
  May 18, 2012
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mfumo wa Marekani wa kuwa na House of representantive(BUNGE) na Senate ni mfumo mbovu kuliko wote duniani na ndio maana hata wananchi wa marekani hawaupendi kwa kuwa unaruhusu rushwa, lobyist na special interest group kuwanunua ma senator ili waweze kupitisha interest za wenye nguvu, na utendaje wake ni mgumu sana, hivyo sheria nyingi hususani zenye maslahi kwa nchi na wananchi wa kawaida hazipiti kwenye mabunge hayo kwa haraka na urahisi.

  Leo hii Bunge la marekani na senate (CONGRESS) lina very low job (Rating) approval kutokana na maoni ya wamarekani, kura za maoni zinaonyesha CONGRESS ya marekani ina job rating of less than 18% job approval and 72% job disapproval, hivyo kutokana na mfumo huo kuwa so complicated inakuwa ngumu sana to get things done in US congress!

  Pili Masenator wote kwenye Congress either awe Junior or Senior US Senator lazima wachaguliwe na wananchi kutoka kwenye majimbo yao, sasa hili la ccm kusema maraisi wastaafu wapewe u senator ni kutaka kuididimiza zaidi nchi yetu, kama kipindi cha utawala wao hawakuweza kuikumboa nchi, iweje wakipwewa u senator ndo wawe na TIJA? hii tutalipinga kwa damu zetu, tunataka kurejesha mamlaka kwa wananchi kwa kuchagua ziongozi wao na kuwawajibisha hata kwa kuwafanyia (Recall kama hawana tija na kuchagua viongozi wengine) na sio kuteuwana, zama za uongozi wa kupeana zimekwisha!

  Hivyo ccm wasitake kuwachanganya watanzania kwa kupendekeza mfumo mgumu wa kibunge ambao hata kwenye nchi zilizo endelea haungwi mkono na wananchi wake na ume prove failure mpaka CONGRESS ya marekani imebatizwa jina la DO NOTHING CONGRESS!
   
 17. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 417,110
  Trophy Points: 280
  a ni ya wachovu wenye mawazo mgando sana.......................yawaje seneti iundwe na wastaafu..............yaani ni kichekzsho huko Uingereza nako waazungumzia kufuta nyadhifa hizo za kurithiana kulingana na cheo cha awali. Bungeni ni wawakilishi wa wananchi siyo mahali pa wastaafu kwenda kulinda dhuluma zao walizotufanyia..............pole sana ccm kweli mmechoka
   
 18. Imany John

  Imany John Verified User

  #18
  May 18, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,776
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  Napinga kwa nguvu zangu zote hoja hii,
  Hawa jamaa wanataka kubaka mchakato wote wa katiba,wanataka kujipanulia wigo wa kuhakikisha mali yatafunwa na hawa walaji wakuu wastafu.

  Kwanza wanatoa wapi mabavu ya kuchambua hoja wakati uhalali wa kulipitisha jambo hilo litawanufaisha mabwanyenye?
   
 19. s

  sawabho JF-Expert Member

  #19
  May 18, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Hili la Wabunge kutoka mikoani litapunguza ukubwa wa Bunge ikiwa ni pamoja na gharama za uendeshaji. Ila hili la Seneti Wastaafu wachwe wapumzike kwa amani kuliko kuwapeleka kusinzia Bungeni.
   
 20. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Haukuelewa? Ni hivi kila Mkoa itatoa Mbunge Mmoja kuwakilisha Mkoa kwenye Senate kwahiyo haitapunguza Gharama, itaongeza Gharama Mara dufu.

  Yeah, Tuna Dhahabu, Uranium, Coal, Iron Ore kwanini tusitumie kutushibisha Matumbo yetu na Viongozi wetu waliostaafu wafe bado wanalipwa na serikali tukufu?
   
Loading...