Vigogo Benki ya Posta jela miaka mitano

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Tabora. Meneja wa Benki ya Posta tawi la Tabora, Boaz Lunyungu, mhasibu wa benki hiyo na mfanyabiashara maarufu mkoani hapa wamehukumiwa na Mahakama ya Mkoa wa Tabora kifungo cha miaka mitano jela au kulipa faini ya Sh100milioni kila mmoja.

Lunyungu pamoja na George Ngatunga (mhasibu) na Umaiya Makiliga ambaye ni mfanyabiashara walishtakiwa kwa makosa saba, likiwemo la utakatishaji fedha zaidi ya Sh700milioni.

Mbali na adhabu hiyo, baada ya kutiwa hatiani mahakama hiyo imewaamuru washtakiwa hao kulipa Sh710milioni walizoiibia benki hiyo, vinginevyo mali zao zitaifishwe na Serikali kufidia kiasi cha fedha kilichoibwa.

Uamuzi wa shauri hilo la jinai namba 154/2015 umetolewa leo Jumatano Agosti 29, 2018 na hakimu mkazi wa mahakama ya Mkoa wa Tabora, Joctan Rushwela, baada ya kuwatia hatiani washitakiwa hao kwa makosa matatu kati ya saba.

Katika hukumu hiyo iliyosomwa kwa muda wa dakika 120, Hakimu Rushwela amesema mashtaka hayo ni kula njama ya kutenda kosa la wizi, kutakatisha fedha pamoja na kosa la wizi.

Awali, upande wa mashitaka ukiongozwa na wakili mwandamizi wa Serikali, Shedrack Kimaro ulieleza mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa hayo kati ya Januari 2014 na Julai 2015 katika Benki ya Posta, Tabora.

Wakili Kimaro amedai katika shitaka la kwanza kuwa katika kipindi hicho washitakiwa kwa pamoja walikula njama ya kutenda kosa la wizi.

Amedai kuwa washitakiwa wote watatu katika tarehe tofauti kati ya Januari 2014 na Julai 2015, waliiba Sh710 milioni katika Benki ya Posta tawi la Tabora.

Katika shtaka la tatu linalomkabili meneja na mhasibu huyo, imeelezwa kuwa wakiwa ni watumishi wa Benki ya Posta, walitakatisha fedha Sh710milioni huku wakijua wamezipata kwa njia zisizo halali
Upande wa Jamhuri wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo ulileta mashahidi 16 waliotoa ushahidi na kuthibitisha washtakiwa hao kutenda kosa hilo.

Mbali na hukumu hiyo, washtakiwa hao bado wanakabiliwa na kesi nyingine ya uhujumu uchumi wakiwa na watuhumiwa wengine 13, shauri ambalo bado halijaanza kusikilizwa kwa kuwa jalada lipo kwa mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP).

Chanzo: Mwananchi
 
Awamu hii ukiwa na mali mpe mkeo na watoto
Wewe weka pesa mpesa kama mil 1 tu
Ili wakisema wataifishe ukutwe huna kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo mkeo akipata kiben ten,atahonga Mali zote huku papuchi ikitafunwa bila wasiwasi,ukileta maneno unapewa talaka 3 fasta.
Mwanamke wa kumilikisha Mali kwa jina lake ni Sawa na kubeep mtoa roho au upate magonjwa sugu maisha yote.
Jaribu uone!!
 
Tabora. Meneja wa Benki ya Posta tawi la Tabora, Boaz Lunyungu, mhasibu wa benki hiyo na mfanyabiashara maarufu mkoani hapa wamehukumiwa na Mahakama ya Mkoa wa Tabora kifungo cha miaka mitano jela au kulipa faini ya Sh100milioni kila mmoja.

Lunyungu pamoja na George Ngatunga (mhasibu) na Umaiya Makiliga ambaye ni mfanyabiashara walishtakiwa kwa makosa saba, likiwemo la utakatishaji fedha zaidi ya Sh700milioni.

Mbali na adhabu hiyo, baada ya kutiwa hatiani mahakama hiyo imewaamuru washtakiwa hao kulipa Sh710milioni walizoiibia benki hiyo, vinginevyo mali zao zitaifishwe na Serikali kufidia kiasi cha fedha kilichoibwa.

Uamuzi wa shauri hilo la jinai namba 154/2015 umetolewa leo Jumatano Agosti 29, 2018 na hakimu mkazi wa mahakama ya Mkoa wa Tabora, Joctan Rushwela, baada ya kuwatia hatiani washitakiwa hao kwa makosa matatu kati ya saba.

Katika hukumu hiyo iliyosomwa kwa muda wa dakika 120, Hakimu Rushwela amesema mashtaka hayo ni kula njama ya kutenda kosa la wizi, kutakatisha fedha pamoja na kosa la wizi.

Awali, upande wa mashitaka ukiongozwa na wakili mwandamizi wa Serikali, Shedrack Kimaro ulieleza mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa hayo kati ya Januari 2014 na Julai 2015 katika Benki ya Posta, Tabora.

Wakili Kimaro amedai katika shitaka la kwanza kuwa katika kipindi hicho washitakiwa kwa pamoja walikula njama ya kutenda kosa la wizi.

Amedai kuwa washitakiwa wote watatu katika tarehe tofauti kati ya Januari 2014 na Julai 2015, waliiba Sh710 milioni katika Benki ya Posta tawi la Tabora.

Katika shtaka la tatu linalomkabili meneja na mhasibu huyo, imeelezwa kuwa wakiwa ni watumishi wa Benki ya Posta, walitakatisha fedha Sh710milioni huku wakijua wamezipata kwa njia zisizo halali
Upande wa Jamhuri wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo ulileta mashahidi 16 waliotoa ushahidi na kuthibitisha washtakiwa hao kutenda kosa hilo.

Mbali na hukumu hiyo, washtakiwa hao bado wanakabiliwa na kesi nyingine ya uhujumu uchumi wakiwa na watuhumiwa wengine 13, shauri ambalo bado halijaanza kusikilizwa kwa kuwa jalada lipo kwa mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP).

Chanzo: Mwananchi
Afadhali wafungwe hao washenzi. Wanaonekana bora na wenye hela kwa wake zako na watoto wao kumbe ni mijizi makubwa hiyo!
Tena kuwekwe sheria iwe adhabu ya kifo ukipatikana na wizi wa aina hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tabora nasikia kuna gereza moja matata na tata sana. Kumbe linaitwaje.
Kukaa gerezani si kazi. Kazi kudhalilishwa siku ya kwanza unapowasili. Wanakuvua nguo zako. Kisha wanaku search mwili mzima ukiwa uchi. Wakikuhisi vibaya wanaingiza kalamu mkuu.ndu.ni kucheki kama umeficha pesa. Yote haya yanafanyika mchana kweupee mbele ya wake kwa waume. Hilo unaambiwa ni trailer.....
Tujiepushe na makosa yakutupeleks jela
 
Kama ni mimi kwa maisha haya bora jela miaka mi tano kuliko kutoa hizo milioni 100 maana hiyo miaka si mingi
Mh! Mkuu, miaka mitatu kamili kukaa ngomeni ni michache?

Kitu cha kuomba tu hapo ni M/Mungu akuepushie!

Lakini miezi 36 jela, kazi ngumu, huduma za
afya na mazingira mabovu!
Kama kuna altenertive ya fine, ni heri kutoa hiyo hela ufirisike, uwe huru kuliko kutupwa jehanamu.

Kwa hali ya sasa hivi miaka yote hiyo, kutoka ni majaaliwa ya MunyeziMungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom