Vigezo vya Ugawaji wa Majimbo ya Uchaguzi Tanzania.

Mwakaboko King

JF-Expert Member
Apr 22, 2015
1,099
207
Ndugu wanajamvi karibuni kwenye Mada inayohusu Ugawaji wa Majimbo ya Uchaguzi Tanzania. Nikiwa mdau wa Siasa za Tanzania najua na hata wewe unajua kuwa mwaka 2020 ambao ni mwaka tutakaofanya Uchaguzi Mkuu hauko mbali, tukiwa tunaendelea kujiandaa na Uchaguzi huo ni vyema tukaelimishana juu ya baadhi ya mambo ambayo huwa yanafanyika kwa kuzingatia sheria.

Ibara ya 74(6) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, imeipa Tume ya Taifa ya Uchaguzi jukumu la kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya Uchaguzi wa Wabunge. Aidha, Ugawaji huo wa Majimbo ya Uchaguzi wa wabunge hufanyika kwa kushirikiana na mamlaka inayohusika na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -TAMISEMI kwa kuzingatia vigezo mbalimbali.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 75(3) na (4) imeainisha vigezo vifuatavyo vinavyohusika na ugawaji wa majimbo ya uchaguzi
  1. Idadi ya watu katika eneo linalokusudiwa. Hiki ni kigezo muhimu sana kwa kuwa wananchi ndiyo msingi wa demokrasia ya uwakilishi. Kwa kawaida, idadi ya watu inatakiwa iwe sawa kwa kila jimbo. Hata hivyo, kutokana na ugumu wa kuwa na idadi ya watu inayofanana katika majimbo yote, Tume huzingatia idadi ya wapiga kura badala ya idadi ya watu na utaratibu unaotumika ni kwa majimbo ya uchaguzi kugawanywa kwa kigezo cha idadi sawa ya wapiga kura kwa kila jimbo.
  2. Upatikanaji wa njia za mawasiliano; Hapa unaangaliwa urahisi wa mwakilishi kuwafikia/ kuwasiliana na wananchi anaowawakilisha katika maana ya Barabara, Simu, Vyombo vya Habari.
  3. Hali ya kijiografia ya eneo linalokusudiwa kugawanywa; hapa yanazingatiwa masuala ya sura ya nchi kama mito, milima na misitu ambavyo ni muhimu kuzingatia katika kuweka mipaka ya majimbo, mahali pengine matokeo ya kuwepo mto/mlima kunaweza kuwa ndiyo alama ya mpaka kati ya jimbo moja na jingine.
Hata hivyo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekuwa ikiongeza vigezo au kuzingatia vigezo vingine ambavyo ni; -
  1. Hali ya Kiuchumi: Hii huangalia hali ya ukusanyaji wa mapato katika Jimbo husika. Lengo ni kuona kuwa maeneo yaliyopo juu kiuchumi hayamezi kiuwakilishi maeneo yaliyo chini kiuchumi. Takwimu zinazotumika katika kigezo hiki zinapatikana ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI);
  2. Ukubwa wa Eneo la Jimbo husika: Hapa huangaliwa eneo la mita za mraba za jimbo husika;
  3. Mipaka ya kiutawala: Katika kugawa Majimbo Tume huzingatia mipaka ya kiutawala. Pale ambapo mipaka ya kiutawala inabadilika kabla ya Tume kufanya Ugawaji wa Majimbo, Tume itatilia maanani mabadiliko hayo;
  4. Mpangilio wa maeneo ya Makazi ya watu yaliyopo: Kigezo hiki kinaangalia zaidi mpangilio wa makazi ya watu katika jimbo husika.
  5. Mazingira ya Muungano: Tanzania ni nchi inayounganisha sehemu mbili, kwahiyo ugawaji wa majimbo unazingatia upekee wa mazingira ya Muungano;
  6. Uwezo wa Ukumbi wa Bunge: Katika kugawa majimbo, Tume inazingatia uwezo wa ukumbi wa Bunge ili kuepuka kuzidisha idadi ya Wabunge kupita nafasi iliyopo katika ukumbi wa Bunge; na
  7. Idadi ya Viti Maalum vya Wanawake: Katiba ya nchi inatenga kiasi cha asilimia 30 kwa ajili ya Wabunge Wanawake wa Viti Maalum, ili kuleta usawa wa kijinsia. Hivyo katika kugawa na kuongeza Majimbo, Tume inazingatia idadi ya Wabunge wa Viti Maalum.
Utaratibu wa kugawa majimbo ya Uchaguzi

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inao utaratibu wa kuchunguza mipaka na kugawa majimbo ya Uchaguzi kama ifuatavyo:-

(i) Kufanya mikutano na wadau kwa kujadili vigezo na utaratibu unaotumika katika kuchunguza Mipaka na kugawa Majimbo;

(ii) Kutangaza kwa Wadau mbalimbali na Wananchi kwa ujumla kuhusu nia ya kufanya zoezi la kuchunguza mipaka na kugawa Majimbo, katika matangazo hayo vigezo na utaratibu unaotumika vinaelezwa;

(iii) Kupokea maombi na mapendekezo ya kugawa, kurekebisha mipaka au kubadili majina ya Majimbo kutoka kwa wadau mbalimbali na kuyachambua;

(iv) Kuainisha maombi ambayo yametimiza vigezo;

(v) Kutembelea maeneo ambayo yanakusudiwa kugawanywa; kukutana na wadau wa maeneo hayo wakiwemo wa ngazi za Kata, Mitaa, Vijiji na Vitongoji ili kujadiliana na kukubaliana kuhusu namna ya kufanya ugawaji,matayarisho ya ramani na majina ya Majimbo mapya;

(vi) Kuandaa taarifa ya mapendekezo ya ugawaji wa majimbo na kuiwasilisha kwa Mhe. Rais kwa mujibu wa ibara 75(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977; na

(vii) Kutangaza Majimbo kama yalivyogawanywa/yalivyorekebishwa mipaka au kubadilishiwa majina katika Gazeti la Serikali.

Jinsi ya uwasilishaji wa maombi

Maombi ya kugawa Majimbo au kurekebisha mipaka yanayoshughulikiwa na Tume ni yale yanayowasilishwa kwa kufuata utaratibu ufuatao:

(i) Maombi/mapendekezo ya kugawa Majimbo au kurekebisha mipaka huwasilishwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri husika ambapo hujadiliwa katika vikao rasmi pia inashauriwa vikao hivyo kuwashirikisha wadau mbalimbali.

(ii) Mkurugenzi wa Halmashauri atawasilisha maombi/mapendekezo kwa Katibu Tawala wa Mkoa (RAS)

(iii) Katibu Tawala wa Mkoa atawasilisha maombi/mapendekezo katika kikao cha Kamati ya ushauri ya Mkoa ili kupata maoni pia.

(iv) Katibu Tawala wa Mkoa atawasilisha mapendekezo Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Nawatakia siku njema!
 
Tunashukuru kwa elimu hii muhimu, nina maswali yafuatayo:-

1. Je ni kwanini majimbo ya Mbeya mjini, Arusha Mjini, Kyela, Mbarali na Mbeya vijijini hayajagawanywa mpaka sasa ijapokuwa hayo majimbo yana vigezo karibu vyote vilivyotajwa kwenye sheria husika?

2. Kwakuwa NEC ni tawi la ccm je ndio sbb inayofanya hayo majimbo yasigawanywe kuhofia kuongeza viti vya CDM bungeni?

Naomba majibu kwa anayejua.
 
Swali zuri Mkuu, kama umesoma vizuri jinsi ya uwasilishaji wa maombi kipengele cha kwanza hadi cha nne kimeweka wazi kabisa taratibu za kupitia. Kuwa na vigezo sio sababu, issue ni kwamba Je Maombi au mapendekezo ya kugawa majimbo au kurekebisha mipaka ya maeneo uliyoyataja hapo juu yamejadiliwa na vikao rasmi vya wadau wanaohusika na kufuata mtiririko unaotakiwa? Jambo la pili Je wadau wanaohusika wameafiki na kukubaliana pasipo shaka kuwa maeneo yao yagawanywe?

Kama hatua zote zimefuatwa NEC haina kizuizi gani cha kushindwa kukubali mapendekezo hayo na Kama wadau wa maeneo husika bado wanaendelea kuvutana kwa maslahi yao hakuna namna maeneo yao yataendelea kuwa hivyo mpaka pale wadau husika watakapokubaliana.NEC haiwezi kuridhia kugawa jimbo ambalo wadau wake bado wanavutana, vigezo na masharti lazima vizingatiwe!

Jambo la Pili, NEC sio chama cha Siasa wala tawi la chama chochote cha siasa ieleweke hivyo, mimi ni mdau wa siasa za Tanzania unaposema NEC ni tawi la chama fulani huwatendei haki watanzania basi hata Uchaguzi Mkuu uliopita wa 2015 usingefanyika na wala wananchi wa vyama tofauti wasingejitokeza kupiga kura kwa wingi ule.

Ni vyema ukaelewa kuwa NEC ilianzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 74 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977,Pia Ibara ya 74(7) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema Tume ni Idara huru inayojitegemea, ukisoma Ibara ya 74 (11) ya Katiba imeweka wazi kabisa kuwa Tume katika kutekeleza majukumu yake ya Kikatiba haitalazimika kupokea maelekezo au amri kutoka kwa mtu yeyote au Idaya yeyote ya Serikali au kufuata maoni ya Chama chochote cha siasa.
 
Ndugu wanajamvi karibuni kwenye Mada inayohusu Ugawaji wa Majimbo ya Uchaguzi Tanzania. Nikiwa mdau wa Siasa za Tanzania najua na hata wewe unajua kuwa mwaka 2020 ambao ni mwaka tutakaofanya Uchaguzi Mkuu hauko mbali, tukiwa tunaendelea kujiandaa na Uchaguzi huo ni vyema tukaelimishana juu ya baadhi ya mambo ambayo huwa yanafanyika kwa kuzingatia sheria.

Ibara ya 74(6) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, imeipa Tume ya Taifa ya Uchaguzi jukumu la kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya Uchaguzi wa Wabunge. Aidha, Ugawaji huo wa Majimbo ya Uchaguzi wa wabunge hufanyika kwa kushirikiana na mamlaka inayohusika na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -TAMISEMI kwa kuzingatia vigezo mbalimbali.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 75(3) na (4) imeainisha vigezo vifuatavyo vinavyohusika na ugawaji wa majimbo ya uchaguzi
  1. Idadi ya watu katika eneo linalokusudiwa. Hiki ni kigezo muhimu sana kwa kuwa wananchi ndiyo msingi wa demokrasia ya uwakilishi. Kwa kawaida, idadi ya watu inatakiwa iwe sawa kwa kila jimbo. Hata hivyo, kutokana na ugumu wa kuwa na idadi ya watu inayofanana katika majimbo yote, Tume huzingatia idadi ya wapiga kura badala ya idadi ya watu na utaratibu unaotumika ni kwa majimbo ya uchaguzi kugawanywa kwa kigezo cha idadi sawa ya wapiga kura kwa kila jimbo.
  2. Upatikanaji wa njia za mawasiliano; Hapa unaangaliwa urahisi wa mwakilishi kuwafikia/ kuwasiliana na wananchi anaowawakilisha katika maana ya Barabara, Simu, Vyombo vya Habari.
  3. Hali ya kijiografia ya eneo linalokusudiwa kugawanywa; hapa yanazingatiwa masuala ya sura ya nchi kama mito, milima na misitu ambavyo ni muhimu kuzingatia katika kuweka mipaka ya majimbo, mahali pengine matokeo ya kuwepo mto/mlima kunaweza kuwa ndiyo alama ya mpaka kati ya jimbo moja na jingine.
Hata hivyo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekuwa ikiongeza vigezo au kuzingatia vigezo vingine ambavyo ni; -
  1. Hali ya Kiuchumi: Hii huangalia hali ya ukusanyaji wa mapato katika Jimbo husika. Lengo ni kuona kuwa maeneo yaliyopo juu kiuchumi hayamezi kiuwakilishi maeneo yaliyo chini kiuchumi. Takwimu zinazotumika katika kigezo hiki zinapatikana ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI);
  2. Ukubwa wa Eneo la Jimbo husika: Hapa huangaliwa eneo la mita za mraba za jimbo husika;
  3. Mipaka ya kiutawala: Katika kugawa Majimbo Tume huzingatia mipaka ya kiutawala. Pale ambapo mipaka ya kiutawala inabadilika kabla ya Tume kufanya Ugawaji wa Majimbo, Tume itatilia maanani mabadiliko hayo;
  4. Mpangilio wa maeneo ya Makazi ya watu yaliyopo: Kigezo hiki kinaangalia zaidi mpangilio wa makazi ya watu katika jimbo husika.
  5. Mazingira ya Muungano: Tanzania ni nchi inayounganisha sehemu mbili, kwahiyo ugawaji wa majimbo unazingatia upekee wa mazingira ya Muungano;
  6. Uwezo wa Ukumbi wa Bunge: Katika kugawa majimbo, Tume inazingatia uwezo wa ukumbi wa Bunge ili kuepuka kuzidisha idadi ya Wabunge kupita nafasi iliyopo katika ukumbi wa Bunge; na
  7. Idadi ya Viti Maalum vya Wanawake: Katiba ya nchi inatenga kiasi cha asilimia 30 kwa ajili ya Wabunge Wanawake wa Viti Maalum, ili kuleta usawa wa kijinsia. Hivyo katika kugawa na kuongeza Majimbo, Tume inazingatia idadi ya Wabunge wa Viti Maalum.
Utaratibu wa kugawa majimbo ya Uchaguzi

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inao utaratibu wa kuchunguza mipaka na kugawa majimbo ya Uchaguzi kama ifuatavyo:-

(i) Kufanya mikutano na wadau kwa kujadili vigezo na utaratibu unaotumika katika kuchunguza Mipaka na kugawa Majimbo;

(ii) Kutangaza kwa Wadau mbalimbali na Wananchi kwa ujumla kuhusu nia ya kufanya zoezi la kuchunguza mipaka na kugawa Majimbo, katika matangazo hayo vigezo na utaratibu unaotumika vinaelezwa;

(iii) Kupokea maombi na mapendekezo ya kugawa, kurekebisha mipaka au kubadili majina ya Majimbo kutoka kwa wadau mbalimbali na kuyachambua;

(iv) Kuainisha maombi ambayo yametimiza vigezo;

(v) Kutembelea maeneo ambayo yanakusudiwa kugawanywa; kukutana na wadau wa maeneo hayo wakiwemo wa ngazi za Kata, Mitaa, Vijiji na Vitongoji ili kujadiliana na kukubaliana kuhusu namna ya kufanya ugawaji,matayarisho ya ramani na majina ya Majimbo mapya;

(vi) Kuandaa taarifa ya mapendekezo ya ugawaji wa majimbo na kuiwasilisha kwa Mhe. Rais kwa mujibu wa ibara 75(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977; na

(vii) Kutangaza Majimbo kama yalivyogawanywa/yalivyorekebishwa mipaka au kubadilishiwa majina katika Gazeti la Serikali.

Jinsi ya uwasilishaji wa maombi

Maombi ya kugawa Majimbo au kurekebisha mipaka yanayoshughulikiwa na Tume ni yale yanayowasilishwa kwa kufuata utaratibu ufuatao:

(i) Maombi/mapendekezo ya kugawa Majimbo au kurekebisha mipaka huwasilishwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri husika ambapo hujadiliwa katika vikao rasmi pia inashauriwa vikao hivyo kuwashirikisha wadau mbalimbali.

(ii) Mkurugenzi wa Halmashauri atawasilisha maombi/mapendekezo kwa Katibu Tawala wa Mkoa (RAS)

(iii) Katibu Tawala wa Mkoa atawasilisha maombi/mapendekezo katika kikao cha Kamati ya ushauri ya Mkoa ili kupata maoni pia.

(iv) Katibu Tawala wa Mkoa atawasilisha mapendekezo Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Nawatakia siku njema!
Ahsante mkuu kwa kutupa darasa la uraia
 
Tunashukuru kwa elimu hii muhimu, nina maswali yafuatayo:-

1. Je ni kwanini majimbo ya Mbeya mjini, Arusha Mjini, Kyela, Mbarali na Mbeya vijijini hayajagawanywa mpaka sasa ijapokuwa hayo majimbo yana vigezo karibu vyote vilivyotajwa kwenye sheria husika?

2. Kwakuwa NEC ni tawi la ccm je ndio sbb inayofanya hayo majimbo yasigawanywe kuhofia kuongeza viti vya CDM bungeni?

Naomba majibu kwa anayejua.

Daaa haya maswali yameulizwa kishabiki sana!!!
 
Nashukuru kwa kujibu maswali yangu hapo juu. Lkn kosa kubwa ambali tulikosea wakati wa kurejewa kwa mfumo wa vyama vingi ni kuruhusu muundo huu wa tume ya kuteuliwa na kiongozi mmoja ambaye ni mwanachama wa chama cha siasa (CCM).
 
Sasa wewe ulitaka iweje? Nenda kasome Katiba ya nchi yako vizuri ndo utaelewa afu ukamwambie mbunge wako apeleke hoja bungeni ya marekebisho ya mfumo.
 
Nashukuru kwa kujibu maswali yangu hapo juu. Lkn kosa kubwa ambali tulikosea wakati wa kurejewa kwa mfumo wa vyama vingi ni kuruhusu muundo huu wa tume ya kuteuliwa na kiongozi mmoja ambaye ni mwanachama wa chama cha siasa (CCM).

Mimi nachojua Tume inafanya shughuli zake kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 , madaraka ya kuwateua watendaji wa Tume yamewekwa wazi kama ilivyotajwa katika Katiba Ibara ya 74 (1) mpaka (5). Kwa sasa huo ndio utaratibu wa Tanzania.
 
Kigezo kilitakiwa kiwe kimoja tu, IDADI YA WATU, sio idadi ya wapiga kura, mbunge anawakilisha watu wote katika jimbo na sio wapiga kura peke yao.
 
Back
Top Bottom