Kuelekea 2025 Ni vema majimbo ya Kawe, Arusha mjini na Mbeya mjini yagawanywe kutokana na Wingi wa Wananchi na Huduma za kiuchumi!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
92,161
160,448
Baada ya ziara yangu ya kichama kutoka Arusha hadi Mbeya kupitia Babati napendekeza majimbo ya uchaguzi ya Arusha mjini na Mbeya mjini yagawanye kutokana na wingi wa Wananchi na ukuaji mkubwa wa Huduma za kiuchumi

Kadhalika Jimbo langu la Kawe nimeshaomba muda mrefu tu ligawanywe

Mungu wa mbinguni awabariki Tume Huru ya uchaguzi 🌹
 
Majimbo yakigawanywa maana yake pia idadi ya wabunge itaongezeka.

Swali la kujiuliza, je wabunge wakiongezeka kutaleta maendeleo chanya kwa majimbo husika au ndio tutaongeza idadi ya watu wa kusinzia ktk vikao vya bunge kwa kigezo cha kutuwakilisha huku wakizitafuna mil18 za mishahara pamoja na malupulupu kila mwezi?
 
Hivi mnatuonaje watanzania? Hivi umejaribu kufikiri kwa kina? Acheni kutwika gharama zisizo na msingi kwa masilahi ya hovyo kwa ajili yenu. Ebu weka hapa CV yako tuone na tuakisi uwezo wako. Honestly, watu kama ninyi hamfai hata kuongoza ngazi yoyote maana huna hoja yenye mashiko.
 
Hivi nikitu gani hasa kinaweza kizue maendeleo kwenye maeneo hayo hadi yagawanywe?kwamba kweli yamekuwa makubwa kiasi hayawezi kuongozwa na mtu mmoja? Wilaya tu Kuna wakati tunaona zimekuwa nyingi hapa nchini, bungeni kwenyewe Kuna wakati tunasema wabunge niwengi hivyo pesa nyingi zinaenda huko. Haitoshi tunatamani majimbo yagawanywe ili wabunge wazidi kuongezeka! Uzuri kwa wanaofikiria vizuri wanajua mgawanyo huu unalengo la kisiasa kuwasaidia baadhi ya watu kupita bila ushindani mkubwa
 
Baada ya ziara yangu ya kichama kutoka Arusha hadi Mbeya kupitia Babati napendekeza majimbo ya uchaguzi ya Arusha mjini na Mbeya mjini yagawanye kutokana na wingi wa Wananchi na ukuaji mkubwa wa Huduma za kiuchumi

Kadhalika Jimbo langu la Kawe nimeshaomba muda mrefu tu ligawanywe

Mungu wa mbinguni awabariki Tume Huru ya uchaguzi 🌹
Unataka kumnusuru yule kinyang'unya dhidi ya Sugu?🤣🤣🤣
 
Majimbo yakigawanywa maana yake pia idadi ya wabunge itaongezeka.

Swali la kujiuliza, je wabunge wakiongezeka kutaleta maendeleo chanya kwa majimbo husika au ndio tutaongeza idadi ya watu wa kusinzia ktk vikao vya bunge kwa kigezo cha kutuwakilisha huku wakizitafuna mil18 za mishahara pamoja na malupulupu kila mwezi?
Mkuu mbunge au Diwani haleti maendeleo,sio jukumu wala wala wajibu wake. Hilo ni jukumu la serikali basi.

Mbunge hana Bajeti ya maendeleo wala hakusanyi kodi. Uwepo wa wabunge ni kutanua wigo wa uwakilishi wa wananchi bungeni katika eneo husika.
 
Kuna viongozi wangapi kwenye hayo maeneo uliyoyataja wanaoongoza? Kwahy hao wameshindwa kuyaendeleza kwahy tulete viongozi mara mbili zaidi ya hao ndio patakuwa na maendeleo.
Yaani tuwaongezee mzigo walipa kodi. Mimi natamani majimbo yaunganishwe na tuondoe ubunge wa viti maalumu ili kubana matumizi na hiyo hela ilekezwe kwenye huduma za kijamii ka afya na elimu.
 
Baada ya ziara yangu ya kichama kutoka Arusha hadi Mbeya kupitia Babati napendekeza majimbo ya uchaguzi ya Arusha mjini na Mbeya mjini yagawanye kutokana na wingi wa Wananchi na ukuaji mkubwa wa Huduma za kiuchumi

Kadhalika Jimbo langu la Kawe nimeshaomba muda mrefu tu ligawanywe

Mungu wa mbinguni awabariki Tume Huru ya uchaguzi 🌹
Majimbo ni mengi mno, huo wote ni mzigo kwetu walipakodi

Nadhani ingrbidi mengine yaunganishwe, na mbunge afanye kazi ya ziada sio kulala tu bungeni
 
Baada ya ziara yangu ya kichama kutoka Arusha hadi Mbeya kupitia Babati napendekeza majimbo ya uchaguzi ya Arusha mjini na Mbeya mjini yagawanye kutokana na wingi wa Wananchi na ukuaji mkubwa wa Huduma za kiuchumi

Kadhalika Jimbo langu la Kawe nimeshaomba muda mrefu tu ligawanywe

Mungu wa mbinguni awabariki Tume Huru ya uchaguzi 🌹
Mkuu, pamoja na sababu ulizo zielezea, lakini msingi wako upo kwenye kuwa nusulu wagombea ubunge wa Chama fulani! ambacho umekiona hakitafanya vyema katika uchaguzi ujao kama majimbo hayo yakibaki kama yalivyo. Mkuu, usiongeze gharama zisizo kuwa za msingi.
 
Muhimu hapo ni kuongeza usambazaji wa rasilimali na sio kugawa majimbo.

Unawaza kugawa majimbo na sio distribution of resources.

Magufuli alipokuwa Rais mwaka 2015 unakumbuka alitumia muda gani bila kuteua baraza la mawaziri ?

Sehemu ambayo Ina
Mkuu wa mkoa
Ina mkuu wa wilaya
Then unataka kugawa jimbo hili kuiongezea serikali mzigo?

Think twice
 
Baada ya ziara yangu ya kichama kutoka Arusha hadi Mbeya kupitia Babati napendekeza majimbo ya uchaguzi ya Arusha mjini na Mbeya mjini yagawanye kutokana na wingi wa Wananchi na ukuaji mkubwa wa Huduma za kiuchumi

Kadhalika Jimbo langu la Kawe nimeshaomba muda mrefu tu ligawanywe

Mungu wa mbinguni awabariki Tume Huru ya uchaguzi 🌹
Acheni kutuongezea gharama za kijinga, hapo jimboni kuna DC/DAS/DED/Madiwani/Wakuu wa Idara na wataalam wengine hawa wote hawaoni kero za wananchi ni mbunge pekee anaona au mbunge anawabeba mgongoni wananchi? Wabunge wenyewe wanaenda kugonga meza, sisi tunataka majimbo yapungue
 
Back
Top Bottom